Bajeti 2022/23 inang’ata, inapuliza

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Dar es Salaam.

Ni kung’ata na kupuliza. Hizo ndizo pande mbili za bajeti ya Serikali iliyowasilishwa bungeni jana, ikiwa ni hatua za kubana matumizi ya Serikali na kuwapa unafuu wananchi.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 bungeni jijini Dodoma jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba alitaja maeneo anayokwenda kubana kwa kuwa yamekuwa yanapoteza fedha za umma.

Moja ya maeneo hayo ni viongozi wa umma walioenguliwa nafasi zao kuendelea kulipwa mishahara ya zamani, safari za ndani na nje ya nchi na matumizi ya magari aliyosema yatakatwa kutoka Sh550 bilioni hadi Sh50.5 bilioni.

Dk Mwigulu alisema waliokuwa makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi watendaji wa halmashauri, makatibu tawala wa mikoa na wilaya wanapoondolewa wanaendelea kulipwa mishahara na marupurupu wanayolipwa warithi wao na hivyo kuibebesha mzigo Serikali.

Kutokana na hali hiyo, alipendekeza pale wanapoondolewa kama wanaendelea kuwa watumishi wa umma, walipwe mishahara waliyokuwa wanalipwa kabla hawajapandishwa.

“Unaweza kukuta nchi ina wizara 25 ila ina makatibu wakuu 50 au zaidi, au halmashauri 184 lakini kuna wakurugenzi 300 au zaidi na hivyo hivyo kwa nafasi nyingine.

“Wengine wamesabaisha upotevu na hasara kwa Taifa, wote wanaendelea kuwabebesha mzigo Watanzania na wanaziba nafasi ya ajira mpya kwa vijana kwa kulipwa mshahara wa nafasi walizotolewa,” alisema.

Wakuu wa mashirika kuomba kazi

Pia alipendekeza mashirika yote ya umma yenye kufanya kazi kwa misingi ya kibiashara yafanye kazi kwa ufanisi na faida.

Katika kufanikisha hilo, alipendekeza wakuu wote wa mashirika ya umma wafanyiwe usaili kwa ushindani ambapo nafasi zianze kutangazwa punde nafasi ikiwa wazi, ili wenye sifa wajitokeze na wafanyiwe usaili na iwe hivyo hivyo kwa bodi.

Magari ya Serikali

Akieleza mikakati ya muda mrefu ya kubana matumizi, Waziri Mwigulu alipendekeza Serikali kubadili utaratibu uliopo kwa kuwakopesha magari watumishi wenye hadhi ya kuwa na gari la Serikali.

Alisema kwa sasa Serikali ina magari zaidi ya 15,742, pikipiki 14,047 na mitambo 373 na inayotumia zaidi ya Sh558.45 bilioni kwa mwaka kwa ajili ya ununuzi wa magari, ununuzi wa mafuta ya uendeshaji, vipuri na matengenezo.

“Ukiondoa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na mahakama, upande wa Serikali wabaki viongozi wakuu wa wizara, mashirika, wakala, mikoa, wilaya na miradi ambao wasimamizi watakuwa eneo la mradi (site) muda mwingi, ambapo kwenye makundi haya hawatazidi watano kwa taasisi.

Alisema kwa mpango huo, watumishi wengine wenye stahili ya gari la Serikali watakopeshwa, watumie magari yao ndipo watasimamia vizuri matumizi, matengenezo, mafuta na vipuri.

“Tutaondoa utaratibu uliozoeleka, dereva na gari anapitishwa chini, bosi anapanda ndege mpaka Mwanza au Mbeya kutoka Dar es Salaam na kurudi hivyo hivyo.

Alisema kuna utafiti wa siri ulifanywa kwa siku moja yakabainika magari ya Serikali yaliyotoka Dodoma kwenda Dar es Salaam yalikuwa 132 na yaliyokuwa yanatoka Dar es Salaam yakipishana kuja Dodoma yalikuwa 76, na mengine 8 yalikuwa yamepinduka.

“Tumezidi kupenda ubosi, magari makubwa kwa kila mtu serikalini, matumizi ya starehe, wakati katika nchi yetu bado kuna watu wanapata shida kupata mlo mmoja,” alisema.

Mbali na mgari, vilevile alisema Serikali itapunguza safari za ndani na nje, semina na kongamano na itabadili mfumo wa manunuzi ambao ulikuwa unapoteza fedha nyingine tofauti na thamani halisi ya bidhaa zinazonunuliwa.

Ili kuifanikisha hayo, ofisi ya mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) itaongezewa fungu ili ifanye kazi zake kwa ufanisi.

Kuhusu kuwadhibiti watumishi wa umma, Dk Mwigulu alibainisha kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwenye ukusanyaji wa mapato, hasa kwenye kodi kubwa, mapato ya Mamlaka za Serikali za mitaa na ardhi akisema huo ni uhujumu uchumi.

“Kuna mapato ya Serikali yanaingia kwenye mifuko ya watu binafsi. Hii inafanyika kwa kukadiria viwango vya juu ili katika majadiliano ya kwenda kwenye kodi stahiki kinapunguzwa kiasi chini ya kile kinachostahili na kilichopunguzwa kinaingia mifuko binafsi,” alisema.

Vilevile, alisema upo mtindo wa wafanyabiashara kuwajadiliana na wateja kuwauzia bidhaa kwa bei ya chini ili wasitoe risiti, masuala ambayo alisema in uhujumu uchumi.

Ahueni

Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu alisema Serikali inatarajia kufanya marekebisho kwenye sheria ya mifumo ya malipo ya Taifa kwa kupunguza tozo ya muamala wa huduma za fedha katika simu za viganjani.

“Napendekeza kupunguza tozo ya muamala kutoka kiwango kisichozidi Sh7, 000 hadi kiwango kisichozidi Sh4, 000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa.

“Punguzo hili ni sawa na asilimia 43 ya kiwango cha sasa. Sambamba na hilo, napendekeza kuongeza wigo wa tozo hiyo ili kuhusisha miamala yote ya kielektroniki.

“Lengo la hatua hii ni kupunguza makali ya maisha kwa Mtanzania hasa katika kipindi hiki cha changamoto kubwa ya kiuchumi na kuweka usawa katika utozaji wa tozo hiyo,” alisema Dk Mwigulu.

Kukuza ajira

Akieleza mikakati ya Serikali katika kukuza ajira kwa vijana, Waziri Mwigulu alisema katika miaka ya sitini, miaka ya sabini na themanini vijana walikuwa wanahudumia wazee na watoto, jambo ambalo sasa limebadilika badala yake wazee ndio wanahudumia vijana kwa kukosa ajira.

Ili kuongeza ajira kwa vijana, alisema Serikali imeongeza bajeti ya Kilimo kutoka Sh294 billioni hadi Sh954 bilioni na itaendelea kuongezeka kila mwaka.

“Ili kupunguza umaskini kwa Watanzania, Serikali inalenga kutengeneza ajira kwa vijana na wanawake zaidi ya milioni tatu katika sekta ya kilimo ifikapo mwaka 2025.

“Hii itafanyika kwa kuongeza eneo la umwagiliaji kufikia hekta 8,500,000, sawa na asilimia 50 ya eneo lote linalolimwa nchini ifikapo 2030.

Mbali na mkakati huo, alisema Serikali imenunua mashine 31 za uchunguzi wa magonjwa (CT Scan) na zinatarajiwa kufungwa katika hospitali za mikoa kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Wabunge wapongeza

Baadhi ya wabunge waliozungumza na Mwananchi baada ya Bunge kuahirishwa walipongeza bajeti hiyo.

Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula(CCM) alisema bajeti ni nzuri na inaenda kutatua matatizo ya Watanzania hasa vijana kwenye suala la ajira kupitia kilimo.

“Nafurahi shule zimefunguliwa jana (juzi) watoto wanaripoti kidato cha tano na sita, zile fedha kwa ajili ya ada zitakuwa nauli na hili jambo halipo katika ilani, haya ni mapenzi yake Rais Samia Suluhu Hassan hili ni pongezi kubwa kwake amefanya jambo la kijasiri,” alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Mjini, Alfred Kimeo (CCM) alisema suala la mafuta ya kula linawagusa Watanzania wengi japokuwa viwanda vya ndani vitaathirika kutokana na mafuta yanayotoka nje.

“Kwenye ada kidato cha tano na sita Rais ameupiga mwingi, mimi kwenye simu yangu kuna meseji za wapiga kura wangu wakiomba ada, namshukuru sana Rais kwa hili,” alisema.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Conchesta Rwamlaza alisema amefurahishwa na Serikali kubana matumizi yake.

Rwamlaza alisema kimsingi bajeti kwa mara ya kwanza imelenga kubana matumizi ya sambamba na kudhibiti matumizi ya magari makubwa pamoja na kulipana posho nyingi.

Alivyotinga bungeni

Jana Waziri huyo akiwa amevalia suti nyeusi na tai ya rangi ya bendera ya Taifa, aliondoka ofisini kwake kwa msafara wa magari mawili ulioongozwa na pikipiki tano za polisi zilizokuwa zikiwasha vimulimuli hadi kwenye viwanja vya Bunge huku ukirushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa.

Msafara huo uliingia katika viwanja vya Bunge saa 9.52 pikipiki moja ikiwa mbele ikifuatiwa na gari wazi lenye namba DFP 9562 na kufuatiwa na gari lake lililokuwa limezungukwa na pikipiki nne.

Kodi ya vileo

Mkurugenzi wa mawasiliano wa kiwanda cha bia cha Serengeti, John Wanyancha amesema bajeti ya wakati mwaka huu haikuongeza kodi kwenye vileo kama bia na pombe kali, kama ilivyozoeleka.

Alisema kwa kufanya hivyo Serikali itaendelea kupata kodi na vinywaji hivyo havitapanda bei.

“Wateja wetu wataendelea kupata bidhaa kwa bei ile ile na iliyo salama na Serikali itapata kodi,” alisema.

Kwa upande wake, mkuu wa kitengo cha uhusiano wa Multichoice, Johnson Mshana alisema kuongeza tozo kwenye ving’amuzi hakutaongeza mapato.

Alisema Serikali ilitakiwa kuongeza wigo wa wateja kwa kuondoa channel za bure.

Mshana alisema ushuru uliongezwa wa kuanzia Sh1,000 hadi Sh3,000 pale mteja anapolipia king’amuzi ugeweza kuongeza mapato ya Serikali kama channel za bure zisingekuwepo.

Mbunge wa Viti Maalumu Felister Njau alisema bajeti hiyo imebeba matumaini makubwa ya wananchi hasa kwa kujielekeza katika kubana matumizi ya Serikali.

Njau aliungana na Kunti Majala aliyesema Serikali ya awamu ya sita imesikiliza kilip cha wananchi na wabunge kwa kuwekeza fedha katika kilimo ambacho ndio shughuli ya Watanzania wengi ya kujipatia kipato.
Imeandikwa na Elias Msuya, Herieth Makweta na Ramadhan Hassan.

Mwananchi
 
Siasa tu hizo, watapoanza kuendesha grand vitara ndio ntajua kweli wapo serious. Ila kuendelea kutumia ma VX bado tabu iko pale pale na wajiandae kwa fogery ya service watumishi wataanza kufoji reciept za manunuzi na kwenda ku retire ofisini.
 
Back
Top Bottom