ukiwa mzee unapaswa utulie ulee wajukuu
Kijana,hujitambui sikiliza vema,
Tunaweza kutoa elimu bure,tunaweza toa matibabu bure.
wakati Tanzania inadai mapato yake kidogo,bado inatoa misamaha ya kodi kitu ambacho ulaya hakipo.wakati tunasema hatuwezi kutoa afya bure ccm hii inaendelea kuruhusu wazungu kuendelea kutunyonya kupitia mikataba.
Wakati ccm hii inaendelea kuruhusu ufisadi ukitawala,bado bajeti hiyo inategemea kwa wahisani.
Benki ya dunia iliweka masharti mwaka 1984 ikiwemo kushusha thamani ya nchi ya fedha,kuomdoa sheria za mifumo ya uingizaji bidhaa,ambapo bidhaa za zitokazo nje zimewekewa masharti ya kuingia bila kutozwa kodi.
Ni aibu kuegemea sera za IMF huku nchi yako ikiteketea, masharti hayo yaliwekwa kwa sababu nchi za afrika zilionekana kwamba rushwa ilikuwa imeongezeka,ufisadi ukitawala,mikopo iniliyotolewa ililiwa na serikali hii,kodi ilikuwa inakusanywa kwa kiwango kidogo mno na fedha nyingi kuingia mifukoni mwa viongozi wachache.
Kwa uzembe huu,wazungu wakaweka masharti hayo.usiwatoe watu kwenye mada haiwezekani maskini aendelee kukamuliwa wakati anauza vitumbua anashindwa kununua flagili ya tsh 2000 na ada ya tsh220,000/ ,huku viongozi wa ccm wakitanua kwa ufisadi mkubwa!
Tuambie nani mwenye uwezo nchi hii kuwekafedha benki za nje kwa siri kana kwamba hatuna benki,wanaficha nini?, chadema itakusanya kodi,itatumia raslimali hizi kujenga maabara si kukata mishahara ya walimu,tunatoa elimu bure fedha zipo