Acheni kujitoa ufahamu! Kwani mbunge wa jimbo akijiuzulu kipindi kama hiki inakuwaje? Je jimbo lake litabaki wazi hadi 2020?
Nafikiri wewe ndiye uliyejitoa ufahamu,Mh.Possi hakujiudhuru kwa hiari,amelazimishwa kujiudhuru,tamko la kujiudhuru kwake limekuja baada ya yeye kuteuliwa kuwa Balozi,na uteuzi wake katika nafasi ya ubalozi(hadi sasa bado hajapangiwa kituo cha kazi)umekuja baada ya Rais kufanya kosa la kikatiba la kuzidisha idadi ya wabunge wa kuteuliwa wa kiume wanaopendekezwa kikatiba.
Ni kosa la kimantiki kuuita uteuzi wa Kabudi na Bulembo kuwa ni uteuzi wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi,utajazaje nafasi wakati anayeishikilia nafasi hiyo bado yupo katika wadhifa wake?Kama ni kujaza nafasi,watawala walipaswa kwanza kumuondoa Mh.Possi kabla ya kufanya uteuzi mwingine ndipo waje na hoja ya kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Possi baada ya yeye kuteuliwa kuwa balozi.
Tufike mahari tuutaje Ukweli kwa rangi yake badala ya kuupindisha,Rais akubali amevunja katiba,ajitathmini na ajisahihishe na si kukimbilia kumtoa Possi kafara ili kuharalisha kosa la kikatiba alilolifanya.
Mnaojaribu kuleta utetezi mwepesi,tambueni kuwa Watanzania wote si misukule yenu,tupo tunaojitambua na ambao bado tuna uwezo wa kuyatazama mambo katika uhalisia wake,usijaribu kutulisha matango pori kwa kumtetea mvunja katiba,mwambieni ukweli ili ajisahihishe Taifa lisonge mbele,kuwaona wanaomkumbusha mkuu kuilinda katiba kuwa ni wachochezi ni uthibitisho wa nakisi ya kifikra waliyonayo watawala.