zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 22,840
- 36,532
Angalau umenisaidi kukionesha kile ambacho labd mimi ningekisema ningeonekana nina nongwa. Katiba ni ya wananchi si ya chama chochote cha siasa katika nchi yenye wanasiasa waungwana, wazalendo wanaoipenda nchi yao. Katika nchi ambayo wanasiasa wanajali matumbo yao, katiba ni ya kikundi ili waweze aidha kushiriki kula au iwawezeshe kuingia na kukaa madarakani.
Watanzania bado hawajaelimika na bado haijawa jamii yenye kuwajibika. Kuelimika ninakokuzungumzia mimi ni kuwa responsible, kufahamu kuwa mwananchi ndio mwenye nchi, mwenye haki ya kuhoji na kuuwajibisha uongozi. Jamii yenye kufahamu kuwa uchaguzi ni kasehemu kamoja tu ka demokrasia, afahamu kuwa demokrasia ina segmeny nyingine nyingi tu. Hatuna mtanzania anayesimamia uwazi, anayesimamia usikivu, uwajibikaji wa serikali na viongozi. Jamii ambayo haina check and balance institution katika kusimamia mambo muhimu ikidai katiba ni bure kwani bado haitaweza hata kuisimamia hiyo katiba yenyewe.
Jambo muhimu kwa sasa wacha ainyooshe nchi, wacha watu watie akili na adabu, wakitia akili na adabu watayatafuta hayo niliyoyasema hapo juu na hapo tutapata katiba ya maana.
Sipendi kujadili majina ya wanasiasa hasa hawa wanasiasa 'wachumia tumbo' wa nchi hii. Wakati katiba ikidaiwa miaka ya 1990 Lowasa alikuwepo. Lakini kwa vile kwake katiba sio ya wananchi ni ya kikundi akabaki na kikundi chake ili waendelee kutawala. Mchakato wa katiba ulipokuja alikuwepo lakini hakusema kama huo mchakato si sahihi. Kwa nini? Jibu ndio hilo hilo kwake katiba si ya wananchi bali ya kikundi cha watu. Akateuliwa kuwa mbunge katika Bunge la katiba, akakubali uteuzi na akaingia bungeni. Katika kupiga kura sina hakika kama alipiga au la lakini chama chake kilisimamia msimamo wake na kikashinda. Maisha yakaendelea, akaendelea na chama chake na akachukua fomu akiomba nafasi yakugomea urais kupitia chama chake na ofcouse baadae uenyekiti wa chama. Labda alikuwa na dhamira yakurudisha katiba ya wananchi si eti eeenh? Labda. Kilichotokea ni historia!
Swali kwa wanasiasa wengine wa upinzani! Je wao hawakujua kuwa ule mchakato si sahihi? Walilisema hilo kabla? Walipoitwa kuubariki ule mchakato wao walifanyaje? Walikimbilia zile posho au walikataa tangu mwanzo? Nani aitishe mchakato tofauti na huo? CCM? Ili iweje? Waondoke madarakani? Jamani tujitahidi kufikiri jamani!
Mimi nimekuwepo nao hao wapinzani na CCM inawajua uzuri ndio maana hawawasumbui, wanajua na kufahamu udhaifu wao, wanawapa chambo kinono, waroho wanakifuata baadae hao wanavuliwa. Mara nyingi hushtuka wakati wameshapotea na tabia hii haikuanza leo. Katika mazingira haya ya wananchi wanaofichwa ukweli na pande zote za watawala na wapinzani, katika mazingira haya ya kutotaka kuwajibika kwa mwanasiasa yeyote wa tawala wala wa upinzani, kwa kweli tumuache jamaa anyooshe nchi, watu waone umuhmu wa kuambiana ukweli pasipo kuoneana haya, umuhimu wa kuwajibika na tuache kuifanya nchi kijiwe cha Mafioso. Eti ubaya unajadiliana na wema? Wapiga dili duniani kote hawajawahi kuwa marafiki wa kweli wa wananchi, wanajipaka tu poda ya urafiki wa kinafiki. Ukiamua kufumbua macho na ukatazama kwa umakini utaona.
Mkuu mbona hatuelewani nimesema ijibu kwa mtazamo wa mwananchi wa kawaida kma mmi unawaingiza wanasiasa wa nini??? Hivi mbowe akiwa fisadi au lowasa akiwa fisadi ndio katiba mpya tusidai ama??
Hao kina mbowe walishatoka bunge kwa kuona mchakato umevurugwa ingawa walikuwa na hope kuwa labda utaenda vzuri kwa hyo kazi yao waliifanya 100% wakamaliza kishujaa sana na wananchi hawawezi kuwalaumu sasa awamu mpya imekuja na tuliomba mchakato urudiwe sasa iweje ajibu vile kna kwamba rasimu ya warioba haikuwa na miiko ya kuwabana hao watumishi wa umma unaodai wamepinda?? Wwe unataka anyooshe nchi kwanza mpaka akili zitukae sawa haya mbona zilitukaa sawa ndio tukadai katiba mpya enzo za kikwete sema mchakato ukavurugwa sasa ina maana watanzania bado tu HAWAJAELIMIKA kma unavyodai wwe??
Kma wananchi hawajelimika iweje walitoa maoni TMK na yakazaa rasimu bora zaidi i guess yenye matumaini kuwahi kutumika hapa tanzania???
Sawa lowasa hakupigania katiba kumbuka hta slaa alikuwa ccm likewise mbowe na huko nako am sure walisupport katiba iliopo....ilamindset ukibadilisha na ukaamua kuleta mabadiliko ni kosa?
Kibaki alitetea sana katiba ya enzi za kina moi iendlee coz alikuwa makam wake na aliwapinga sana kina odinga waliotaka katiba mpya ila si baadae alijiunga upinzani?? Na akajiunga na kina odinga na mwisho wa siku akaleta katiba mpya kuke kenya sasa lowasa na kibaki tofauti yao ni nini?? Lowasa angeshinda unafkiri angekataa rasimu ya warioba wakati ndio hoja ya kwanza ya UKAWA??
Cha kushangaza unajua kabisa kuwa ccm hawataki katiba mpya kwa kuwa watatoka madarakani sasa iweje unawatetea kwanni sasa unatumia nguvu nyingi sana kutaka tusiidai katiba more so reference yako ni WANASIASA
Kwanni usitoe solution for instance labda asasi za kiraia au wanazuoni kutoa elimu ya uraia na umuhim wa katiba kwa wananchi wasio na elimu kuliko wwe unakatisha tamaa tu eti WATANZANIA HAWAJASOMA sasa kwanni usitoe ushauri jinsi ya kuwaelimisha??
Hao zanzibra waliopata katiba mpya 2010 wameelimika sana kuliko huku bara?? Katiba hii ya sasa wakati inaletwa wati walikuwa wamelimika kuliko sasa???
Nakusubiri unipe majibu kuelemiika gani huk kunakofanya tusipate katiba mpya ambao wazanzibar wanayo io elimu
(Naomba usiingize wanasiasa njoo kiSOCIAL zaidi political factors achana nazo maana utaisia kwenye kujadili lowasa na sijui ufisadi wa mbowe)