lusaka city
Senior Member
- Mar 17, 2015
- 146
- 116
ALIYEKUWA Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Massaburi hivi karibuni alijitoa rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kuwaniaUspika kupitia Chama Cha Mapinduzi na bila kutafuna maneno alieleza kumuunga mkono Job Ndugai akisema ndiye kiongozi mwenye sifa.
Lakini pia Dk Massaburi alisema hatua yake hiyo ilikusudia kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama hicho ambacho kimekuwa kikikumbwa na migogoro wakati wa uchaguzi unapowadia.
Ndugai (Job) alikuwa Naibu Spika wa Bunge na sasa ameomba kugombea nafasi ya Uspika kwa hiyo katika muktadha huo huo wa kuhakikisha Bunge linakuwa na kiongozi mahiri na mzoefu nitakuwa tayari kumuunga mkono Ndugai ili aweze kushinda nafasi hiyo na kuliongoza Bunge ambalo chini ya Rais Magufuli, Watanzania wote wanahamu ya kuona kuwa anapatikana Spika anayeweza kwenda na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano,? alikaririwa Dk Massaburi.
Kuhusu nini atakifanya baadaye baada ya kujitoa na kumuunga mkono Ndugai, Dk Massaburi alisema anaweza kulitumikia Taifa akiwa nyumbani kwake Chanika na si lazima kuwa Spika au Mbunge kuwatumikiwa Watanzania.
Kwangu mimi binafsi wakati leo Bunge linapata Spika, lakini nimelazimika kumpongeza Dk Massaburi kwa hatua yake hii ambayo ni lazima iwe mfano wa kuigwa kwa wagombea wa CCM na vyama vingine kwa kutong'ang'ania madaraka.
Dk Massaburi kwa kumuunga mkono Ndugai tena kwa kueleza bayana kwamba ana uwezo mkubwa na uzoefu unaotosha katika kuongoza Bunge ni kitendo kinachomdhihirisha kuwa ni kiongozi asiye mbinafsi na anayejali maslahi mapana ya chama chake na nchi yake na si maslahi yake binafsi na familia yake.