Dk. Masaburi ameonesha ukomavu wa kisiasa

Dk. Masaburi ameonesha ukomavu wa kisiasa

Kwa tunaomuelewa Dk Masaburi ni mtu makini sana na yupo vizuri sana up-stairs
 
suala la UDA lipo wazi Dk Massaburi ameongeza bei ya uuzwaji kutoka Bilioni 1 hadi bilioni 5.7, na akaivunja Bodi ya UDa kwa wizi, halafu akafichua Sh milioni 300 kuwa zimeingia kwenye akaunti binafsi ya Iddi Simba. Huyu ni shujaaa. Uda ilikuwa inakufa kama yalivyokufa mashirika kibao ya umma. Uda ipo mtaani na tunapanda kila siku, kosa hapo liko wapi hebu tuwe specific.
 
ALIYEKUWA Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Massaburi hivi karibuni alijitoa rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kuwaniaUspika kupitia Chama Cha Mapinduzi na bila kutafuna maneno alieleza kumuunga mkono Job Ndugai akisema ndiye kiongozi mwenye sifa.

Lakini pia Dk Massaburi alisema hatua yake hiyo ilikusudia kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama hicho ambacho kimekuwa kikikumbwa na migogoro wakati wa uchaguzi unapowadia.

Ndugai (Job) alikuwa Naibu Spika wa Bunge na sasa ameomba kugombea nafasi ya Uspika kwa hiyo katika muktadha huo huo wa kuhakikisha Bunge linakuwa na kiongozi mahiri na mzoefu nitakuwa tayari kumuunga mkono Ndugai ili aweze kushinda nafasi hiyo na kuliongoza Bunge ambalo chini ya Rais Magufuli, Watanzania wote wanahamu ya kuona kuwa anapatikana Spika anayeweza kwenda na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano,? alikaririwa Dk Massaburi.

Kuhusu nini atakifanya baadaye baada ya kujitoa na kumuunga mkono Ndugai, Dk Massaburi alisema anaweza kulitumikia Taifa akiwa nyumbani kwake Chanika na si lazima kuwa Spika au Mbunge kuwatumikiwa Watanzania.

Kwangu mimi binafsi wakati leo Bunge linapata Spika, lakini nimelazimika kumpongeza Dk Massaburi kwa hatua yake hii ambayo ni lazima iwe mfano wa kuigwa kwa wagombea wa CCM na vyama vingine kwa kutong'ang'ania madaraka.

Dk Massaburi kwa kumuunga mkono Ndugai tena kwa kueleza bayana kwamba ana uwezo mkubwa na uzoefu unaotosha katika kuongoza Bunge ni kitendo kinachomdhihirisha kuwa ni kiongozi asiye mbinafsi na anayejali maslahi mapana ya chama chake na nchi yake na si maslahi yake binafsi na familia yake.


Kapima kaona parefu analeta swaga, hahahaha,! Mleta mada unaweza kuwa ni miongoni mwa walio mlia pesa zake kipindi cha kampeni hapo ubungo. Lakn umefanya vizur angalau kumpoza, maana alipoteza pa kubwa!
 
Unaweza kumuona ni kiongozi wa aina gani kama ukitumia akili kufuatilia siasa zake. Unaweza kuona namna alivyojitoa mwanzoni na kumuunga mkono Ndugai na muda mfupi ujao Ndugai atakuwa spika, sasa mwanasiasa kama huyo si wa kumbeza kirahisi rahisi.

Yes tumeshamjua ni mtu wa aina gani pale aliponunua t.shirt za chadema na kuwavika uvccm na kuhadaa umma kuwa yale ni maandamano ya Chadema wanaopinga uongozi wao wa chama. Waandamanaji hao fake walichezea kichapo heavy hadi wakakiri kuwa hao ni waandamanaji fake.
 
Ubungo alijaribu kila hila lakini wapi maji yakawa marefu. Ngoja wazee wa kazi wafanye Uchambuzi mpya juu ya uuzaji wa hisa za UDA kwa Simon Group na mchango wa Dr. Masaburi katika kufisadi mradi wa Wana Dar es Salaam. Hana maana yeyote, ni fisadi tu.
 
suala la UDA lipo wazi Dk Massaburi ameongeza bei ya uuzwaji kutoka Bilioni 1 hadi bilioni 5.7, na akaivunja Bodi ya UDa kwa wizi, halafu akafichua Sh milioni 300 kuwa zimeingia kwenye akaunti binafsi ya Iddi Simba. Huyu ni shujaaa. Uda ilikuwa inakufa kama yalivyokufa mashirika kibao ya umma. Uda ipo mtaani na tunapanda kila siku, kosa hapo liko wapi hebu tuwe specific.

Kwani Uda ya serikali? Au ya CCM?
 
Mtu mwenye anaitwa MASABURI ...................... Hujui kwamba majina HUUMBA!
 
Mtoa mada kaleta mada kama mada nyingine zinavyokuja jambo la msingi ni kujenga nguvu ya hoja si hoja ya nguvu.
 
Hivi ukiwa mpiga dili unaweza fanya kazi na wazungu? tena Benki ya Dunia thubutuuuuuu wale sio kama Mkombozi Benki au stanibic, Dk anaaminika ni basi tu wabongo tuna wivu wa kike
 
tatizo ni hilo joina,yaani linamuaffect kweli baba wa watu,bora aje abadili tu

Asingekuwa amewahi kuwa meya wa jiji na tukam prove failure angeweza kupewa hata nafasi nyingine ya kujaribu maana siasa za Tanzania ni za majaribio kwa maandalizi ya kazi nyingine zisizo za kisiasa!
 
Huyo majeruhi wa ubungo naye aache usanii, Kama alijua kwamba Ndugai anatosha kwanini na yeye aliamua kuchukua fomu kugombea??
 
Hakika tunaitaji viongozi kama masaburi .nashangaa serikali imuache mtu kama yeye ni mtu muhimu kwa serikali ya tanzania.hakika ametumia elimu,busara yake na ukomavu wa kisiasa katika hili. Kweli ccm wana watu.

Oyaore uru, Jaduong! Umeonyesha ukomavu wa Rorya. Masaburi kiongozi shupavu, kweli?
 
Labda niulize ni Massaburi yupi maana inawezekana mnamsema mwingine! Massaburi kiongozi makini, oyayee!
 
Masaburi kaisha kisiasa.

Umeya ndio ilikuwa turufu yake na hii yote ilikuwa ni fadhili za wakubwa na kwa sababu na wao wameondoka na yeye ndio hivyo amekwisha kabisa.

Hana anachoweza kuwatumikia wananchi, sana sana awekeze kuinua chuo chake na hiyo shule.
 
Samahani,ukiwa jimboni Ubungo,Chanika inapatikana sehemu gani?
 
Back
Top Bottom