Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,000
- 92,691
Salamaleko!
1. Gen z bado hamjui nini kilitokea hapo nyuma. Hamjui tulieni.
2. Kama mnataka kujifunza kaeni hapa nitawafunza. Lakini nawajua kwa ubishi wenu. Mniambie mnataka style ipi.
3. Mnataka Flow ya Habil na khabil, Mzee wa pekezake kizakezake akiacha mambo zao kwa Raha zao. Au
4. Au mnataka Flow ya October 2pm, sijui mdada au mkaka wa Mayii Nye Nye Nye. Na bado.
5. Au mnataka style ya Popoma, Gentemycine, Mzee wa mitusi, short temper. Game changer, talented . Niambie Gen z mnataka flow ya style gani?
6. Au nitumie mchanganyiko? Yaani nipige miguu miwili kama Gaucho?
7. Hamjui Acha niwape. Na nitawapa kuwapa. Kwenye siasa kuna style nyingi zatumika. Zaenda naenda waenda twaenda zetu kizetu zetu.
8. Nimekumbuka style ya siasa maarufu ya Maji marefu. Mnaijua hiyo?
Mlikuwa hamjazaliwa. Vipi ya manyaunyau moja ya style hatari Sana hizo. Katika siasa.
9. Maji marefu, maji yenye kina, kilindi, mkondoni, katika siasa hatari ndio hizo.
10. Maji marefu hupendelewa na mnyama katili aitwaye Mamba. Dadeki. Hiyo style katili Sana hiyo. Watoto wa juzi lazima mpaniki. Style hiyo inahitaji wakongwe kazini, sio ze comedy za kina Masanja na Mpoki. Nazungumzia kazi KAZI sio vituko.
11. Basi Swala yeye hupendelea maji yenye mawimbi kwani ndio yenye ladha. Yaliyotulia hawapendelei. Pasipokujua mawimbi mengine yanasababishwa na mjongeo wa Mamba muuaji. Sio kila wimbi linatokana na upepo. Nilisema. Hamkusikia.
12. Maji marefu yametulia na hayanaga mwendo. Hatari Sana hayo. Gen Z tatizo mmejaa ubishi. Lakini wakubwa zenu Kila Siku tutasema.
13. Vipi Manyaunyau styles. Unaijua Hiyo?
14. Kwanza anaimba natoa Leo, natoa toa. Natoa pembe natoa toa. Manyaunyau huyo. Watu wanashangilia kama wamepagawa. Unajua nini. Hawaelewi wameingizwa kingi. Wamefungwaje wenyewe wanashangilia utadhani wamefunga wao.
15. Wanaibiwa waziwazi wanashangilia, makofi na vigelegele.
Hamuwezi nielewa mimi mtu wa zamani kidogo. Miaka hiyo ya kina Allan Quaterman ilikuwa ng'adung'adu.
16. Embu fikiria sasa. Umekaa zako. Huna hili wala lile, anatokea mtu hapo kwako anajitambulisha kwa sauti ya kujiamini; naitwa manyaunyau, mtaalam mahiri. Nimekuja kukusaidia na kukuondolea matatizo katika nyumba yako.
17. Hujakaa kidogo unashangaa huyo karuka, mara kapaa kimashoati yaani kininja wa buza.
18. Upo kwenye tahamaki unashangaa sauti ya radi paratatata paaa!
Unaingiwa na hofu, unahema kama fala.
19. Manyaumanyau anadondoka chini kwa kishindo kufumba na kufumbua yupo na pembe. Analia analia huku anajinyonga mara anajibetua chaa.
Mara anaitupa Ile pembe ailiyoitoa kwenye uwanja wako, anaitupa kwenye chungu alichokuja nacho.
20. Punde unasikia sauti kutoka kwenye chungu ikinguruma. Ngruu ngruu. Weewee (anataja jina lako) dadeki unababaika kwani hukuwatajia jina lako.
21. Wanaendelea, huna Siku nyingi weee. Weweee huna Siku nyiingi. Wanachukua wanataka damu yako. Na Leo usiku wanamaliza tambiko la mwishooo.
22. Unaanza kulia kwa kupagaawa kama lijinga sasa. Nisaidie manyaunyau. Nisaidie manyaunyau. Nifanyeje.
23. Unaijua siasa wewe. Hiyo inaitwa manyaunyau style. Yaani huna tatizo lakini unaletewa matatizo. Mengi mengine ni matatizo hewa. Matatizo ya msingi hayatatibiwa ila matatizo hewa yatatibiwa. Hiyo ni manyaunyau styles
24. Pembe wameweka wao. Hakuna anayetaka kukuua Zaidi ya manyaunyau mwenyewe. Usife miaka yote uje ufe kisa manyaunyau katoa pembe nyumbani kwako. Thubutu yake. Yeye kama sio mhusika ni nani?
25. Aliyemuambia jina lako ndiye anashirikiana naye kukuletea matatizo. Manyaunyau uwezo WA kujua jina lako Hana mpaka aaimbiwe.
Manyaunyau style kwenye siasa.
26. Mnaishi vizuri wakristo na waislam. Manyaunyau akija atakuambia wewe. Haa haa naona naona Yule jirani yako mkristo anachinja nguruwe Leo usiku. Anaweka kwenye Banda lako la mifugo.
Anachukua mafuta ya nguruwe anayaweka kwenye gari au biashara yako.
Manyaunyau huyo. Hivi Gen Z mnajua Manyaunyau styles?
27. Usile kwa muislam weee. Haaa mizimu inanionyesha hapa. Wanachukua maji ya maiti wanaweka kwenye chakula. Usile.
Hiyo ni manyaunyau styles
28. Mtibeli umevurugwa wewe. Toka hapa wewe. Kafie mbele wewe. Hueleweki wewe. Unaropoka ropoka wewe toka hapa. Unahara mashudu yako hapa. Toka.
29. Sawa natoka. Kwanza nimeshachoka.
Ila Dawa nimewachoma Gen Z.
Najua Manyaumanyau style hamuijui vizuri. Na maji marefu hamjaipata.
Mpango wangu mwaka 2026 panapo majaliwa nikawe mganga mahiri WA kienyeji alafu nione kima akinifuata fuata. Tutaonyeshana.
Acha nikalale.
Taikonmaster..
Kwa sasa Dar es salaam mbioni kujiunga na mafunzo ya uchawi, uganga, ulozi na uganguzi.