1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,802
- 10,307
waasisi wa ACT ni watatu tu - Zitto, Mkumbo na Mwigamba!!
Hiki ni chama kilichoasisiwa mahsusi kupunguza kura za CDM 2015 ili CCM ipate ahueni - nyie mtaona kama kitapigwa hata bomu moja kwenye mikutano yake!!
Nitafurahi sana siku Zitto akigombea uraisi kama mpinzani wa CCM... Msiniulize kwa nini...
Akiongea leo kwenye redio ya mawingu fm, Dr kitila amesema Mh Zitto Kabwe ni mmwanasiasa maarufu na mwenye akili nyingi na ni watu wajinga tu ndiyo watamuacha kwenye vyama vyao. Amesema atafanya kila njia ili ajiunge nao kwenye chama kipya kitakacholeta upinzani wa kweli kilichopata usajili wa kudumu hivi karibuni. :A S 39:
Kwanini Mkuu?
Halafu umepoteaa
Good luck. Ila asubiri hadi 2015 baada ya Bunge kumaliza muda wake maana Zitto akijiengua sasa ina maana ubunge wake bye bye. Dr. Kitila ameingia katika kundi lile la 'nomads' wa kisiasa!
pole sana kwa maumivu ya moyo wenzenu wanafanya siasa za ukweli wala siyo kubabaisha kama chadema hapa ndipo tutajua nani mwanaume na nani mvulani zitto na kitila ni kiboko yenu.Yap hiyo ni CCM "C". Kwa heri Zitto, kwa heri Mkumbo, kaendeleze usaliti wenu kupitia hiyo CCM "C".
Tiba
Haya maneno yanafurahisha sana. Hata CDM, CUF au NCCR - MAGEUZI zilileta na zinaendelea kuleta ushindani wa kweli. Sijui huyu Dr kama anajua ni kwanini vyama hivi vilipata na vinaendelea kupata misukosuko ili visikue! Kama hiki chama kinaongozwa na watz hawa hawa akina Dr na wenzake kama wale watz niliwaona kwenye bunge maalumu la kutunga katiba mpya, basi chama kitakuwa na kuporomoka kama vyama vingine mpaka pale watz tutakapo tambua umuhimu wa kusema ukweli na kutokuwa wanafiki na kuacha USALITI ktk harakati za kuleta mabadiliko ktk nyanja mbalimbali za kisiasa, uchumi na kijamii.
Kwenye hili Chadema walikosea...sitaki kuamini kuwa watu walio tayari kuongoza nchi walishindwa kulimaliza hilo la Zitto humo ndani ya chama kimyakimya bila kuleta sintofahamu au udhaifu wao kwa wananchi huko nje.Hapa ndipo lilipokuwa kosa la Chadema,waliweka mbele jazba kuliko busara, hilo ni kosa bila kujali kama Zitto alikuwa na makosa au hakuwa nayo.
Gwamyitu, umechemsha
..ukombozi hasa wa taif hili hautaletwa na chama cha siasa kamwe....hili jambo naona watanzania wengi(wakiwemo wasomi)bado hawajalitambua....Ukombozi wa kweli wa taifa hili utaletwa na mtu mmoja tu kwenye nafasi ya juu ya urais...mtu atakayekuwa radhi kuwageuka wenzake...washkaji na wapambe wote na kuamua kusimamia na kuipigania katiba ya nchi ..kwa kupambana na madui wote wa taifa hili...yani ubinafsi...anguko la maadili ya umma..ufisadi..rushwa...umaskni...ujinga na maradhi......rais atakaeweza kupambana na maadui hawa ndie atakuwa mkombozi wa taifa hili....na si chama cha siasa....Dk. Kitila Mkumbo amejitambulisha rasmi kuwa ni mwanachama wa ACT kupitia Clouds fm leo asubuhi amesema atamshauri Zitto aje kugombea uwenyekiti.
==============
JamiiForums imefanikiwa kumtafuta Dr. Kilila Mkumbo kuthibitisha habari hii. Amekiri kuongena na Clouds FM na kwamba yeye ni Mwanachama wa Alliance for Change and Transparency (ACT).
serikali tatu ndio kiboko yenu, ngoja aje...ubongo wa kuku. Mawazo yako sawana kuku jike
Nomads are really NOT MAD!
MAD ARE THOSE WHO MAKE THEM 'NOMADS!'
Dk. Kitila Mkumbo amejitambulisha rasmi kuwa ni mwanachama wa ACT kupitia Clouds fm leo asubuhi amesema atamshauri Zitto aje kugombea uwenyekiti.
==============
JamiiForums imefanikiwa kumtafuta Dr. Kilila Mkumbo kuthibitisha habari hii. Amekiri kuongena na Clouds FM na kwamba yeye ni Mwanachama wa Alliance for Change and Transparency (ACT).
Chadema walikurupuka bila kupima upepo. Sasa kuna wabunge 24 wa chadema wanaomuunga mkono Zitto watafuata nyayo ikiwa jamaa ataondoka CDM.