Weka akiba ya maneno mheshimiwa. Mliwaponda sana CUF kwamba ni CCM 'B' na mkamwita James Mbatia ni shoga. Lakini leo hawa ndio wanaowafichia aibu. Hii nchi ni huru. Acheni watu wafanye siasa, na nyie fanyeni siasa zenu. Hasira za nini wakati watu mliwafukuza wenyewe kama wezi?
"Atamshauri Zitto agombee uenyekiti"!? Inamaana ACT haina wanachama wengine?!Au Mkumbo kazi yake ni kumshauri Zitto kila alipo?Ikitokea Zitto akahamia nchi nyingine, Kitila ataendelea kumshauri akiwa kule au ataacha kazi ya ushauri kwa sababu Zitto hagombei nchini?!
Sheria haimruhusu kabisa Kittlya kuwa mwanasiasa na wakat anatumikia umma kama mwalim, lakin kwakuwa wao waliomtuma ndio serikar utasikia hili!!
ACT? Another ghost party in favor of CCM, party of devils.
Dk. Kitila Mkumbo amejitambulisha rasmi kuwa ni mwanachama wa ACT kupitia Clouds fm leo asubuhi amesema atamshauri Zitto aje kugombea uwenyekiti.
==============
JamiiForums imefanikiwa kumtafuta Dr. Kilila Mkumbo kuthibitisha habari hii. Amekiri kuongena na Clouds FM na kwamba yeye ni Mwanachama wa Alliance for Change and Transparency (ACT).
Ni Shibuda na Alfi tu!Chadema walikurupuka bila kupima upepo. Sasa kuna wabunge 24 wa chadema wanaomuunga mkono Zitto watafuata nyayo ikiwa jamaa ataondoka CDM.
Kakoswa koswa kufukuzwa kazi kama si ma - DR wawili wa UDSM na Anthony Komu kumtetea angechomolewa UDSM mwezi wa tatu mwaka huu.Akiwa Chadema aliendelea kufundisha Chuo na hakuna kati yenu aliyesema haya. Tuwe na aibu katika baadhi na mambo ya dhahiri.
Huwezi kuendesha mapambano ukiwa na wahuni, wanafiki, wasakatonge na wajinga kama Zitto, Kitila na Mwigamba. Wahuni hao kutimuliwa ni uamuzi wa busara kuliko uamuzi wowote uliowahi kufanywa na CDM
Lakini Zitto kwa maneno yake alisema atakuwa wa mwisho kuondoka CHADEMA.