Dk. Bana awajia juu CHADEMA/CUF kuhusu M4C & V4C

  • Dk. Bana asema harakati zao hazikubaliki
  • Tendwa naye awatega kuhusu ruzuku

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetupiwa lawama kwamba harakati zake za kisiasa zinatishia usalama na amani ya nchi.

Hayo yalijitokeza jijini Dar es Salaam leo, katika Kongamano liliitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa na kuwashirikishaviongizi wa vyama vyote vya siasa.

Kongamano hilo lilikuwa likijadili umuhimu wa amani na usalama wa nchi, wajibu wa Jeshi la Polisi na vyama vya siasa katika kukuza demokrasia ya vyama vingi.

Baadhi ya wadau na vyama kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini walikitupia lawama chama hicho na kudai kuwa kimekuwa mstari wa mbele katika kuvunja sheria na maadili ya taifa.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alisema harakati zinazoendeshwa na CHADEMA, hazikubaliki na zinalenga kuvunja sheria za nchi.

Dk. Bana, alisema alikosoa kile harakati za chama hicho kupitia oparesheni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), kwa kufanya mikutano kila kona ya nchi haina tafsiri nyingine yoyote zaidi ya kutaka kuvunja amani na usalama wa nchi.

Katika mada yake, iliyohusu, Mazingira wezeshi na hatarishi katika kujenga na kukuza mfumo wa vyama vingi vya siasa, Dk. Bana, alisema, CHADEMA, ni chama kikubwa na chenye nguvu kuweza kuchukua dola, hivyo kinapaswa kuonyeshwa mfano kwa umma hasa katika kutii na kuheshimu sheria. Alisema mikutano na maandamano ya CHADEMA yanayofanyika kila mahali nchini hayana lengo zuri kwa sababu muda huu si wakati wa kampeni za uchaguzi.

Mharidhi huyo wa siasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa REDET, alisema kinachofanywa sasa na chama hicho si kueneza sera zake bali ni sawa na kampeni za uchaguzi kabla ya muda wake.

Alisema wakati huu ni wakati wa vyama vya siasa kujijenga kwa kufanya mikutano ya ndani ya chama, kuandaa viongozi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi mkuu 2015 pamoja na kuhamasisha wananchi washiriki shughuli za maendeleo na si kufanya mikutano na maandamano yanayofanana na kampeni za uchaguzi.

Alisema, kauli mbiu ya M4C, ni nzuri lakini haifai kwa wakati huu, na kusema ikitokea kila chama cha siasa kilichopata usajili kutaka kufanya siasa kwa maandamano na mikutano kama CHADEMA nchi haitatawalika. Dk. Bana, pia alizungumzia hatua ya CHADEMA kususia kongamano hilo, huku akisema si hatua nzuri kwani inaonyesha chama hicho hakina uvumilivu wa kisiasa.

"CHADEMA ni chama kikubwa ambacho kimejijengea heshima kubwa na kinatarajiwa kuchukua dola wakati wowote, kwa hiyo hakina budi kufuata na kuzingatia sheria za nchi ili kuonyesha mfano kwamba kipo tayari kuongoza umma.

"Mimi sielewi hizi harakati zao zinalenga nini, sioni umuhimu wake, vyama vya siasa baada ya uchaguzi huwa vinapata muda wa kujitathimini na kufanya mikutano ya ndani siyo vuguvugu, lakini kinachofanywa na CHADEAMA sasa ni kampeni za uchaguzi ambazo si wakati wake,

"Hii si nchi ya mabadiliko, tunayo serikali iliyowekwa madarakani na wananchi kwa mujibu wa sheria, sasa wanaandamana kupinga nini? Alisema na kuhoji Dk. Bana "Wakiendelea namna hii, nchi itapelekwa pabaya, haya maandamano na vuguvugu hizi zinaweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi, hakuna uhuru.

Tendwa naye anena
Msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa, alisema kitendo cha CHADEMA kususia kongamano hilo siyo cha kiungwana.

Alisema, kongamano hilo, lilikuwa na nia njema ya kuwaweka karibu viongozi wa jeshi la Polisi, vyama vya siasa pamoja na ofisi yake ili kutafuta muafaka wa kitaifa.
 
Masikini mzee kanywa togwa kalewa kajikojolea hivi!akipewa konywagi lazma avue nguo vodka ndio atakata gogo kabisa!poleee
sana mzee.
 
sitaki kuamini kuwa benson hajui kazi malengo ya chama chochote cha siasa. vinginevyo nabaki kuamini kuwa analinda ugali wake. Tendwa naye eti anasema CHADEMA wasichukue fedha za ruzuku,acha niamini kuwa kweli Tendwa kazeeka anastahili kupumzika kwa heshima japo hii kidogo alobakiwa nayo. haiingii akilini kauli kama hiyo kutolewa na mtu wa wadhifa wake. je anadhani CHADEMA wanapewa ruzuku kama hisani au kuonewa huruma???kama ndio na apendekeze bunge lifute rasmi ruzuku kwa vyama tuone chama chake kama kitachangiwa na wanachama wake ili kijiendeshe.
 
"Huwezi kutofautisha mwenye Masters na darasa la saba" by Rev Msigwa (19/06/2012). Huyu anayejiita msomi (BANA) ameruhusu moyo wake ufikiria badala ya kichwa. Anapoongelea CDM na CUF kwa kulaumu amesahau wajibu wa vyama vya siasa hasa katika mfumo wa vyama vingi? Analaumu M4C na V4C na kusahau "vyua Gamba vua Gwanda vaa UZALENDO?" No wonder nchi hii inaangushwa na wasomi!
 
Jamani, kama kuna mambo ya ajabu, basi mojawapo ni hili la Bana kuwa profesa. Kutokana na Bana kuwa profesa, sasa hivi sithamini tena hiyo tittle bali ili kujiridhisha kuwa anayeitwa profesa ni profesa kweli ni lazima kwanza uangalie na matendo yake maana hapa Tanzania tuna watu wanaitwa ni wasomi lakini hopeless kabisa, aheri ukatafuti ushauri kwa mzee wa kijijini ambaye hajaenda shule kabisa.

Huyu Bwana nilisoma naye pale UDSM, alikuja na qualifications za ajabu akiwa mtu mzima, na sijui alikuwa anafanya kazi wapi. Wakati ule sisi wote tulikuwa tukilazimishwa kusoma siasa za marxism na lenninism (somo la DS), huku kila mmoja akilidharau somo hilo, huyu bwana akaamua hilo kuwa ndiyo Major subject yake (kwa sababu hakukuwa na uwezekano wa mwanachuo kupata F kwenye somo hilo). Leo eti na yeye ni think tank wa nchi, maajabu makubwa!!!

Nawapa pole waliopita kwenye mikono ya huyu zezeta! Mhadhiri anazidiwa na wanafunzi wake?! AIBUUUUU! Tumweke kwenye mzani na Deus K. tuone kama huyu Dr mwenye kichwa cha kufugia nywele hajapigwa gap!!
 
images
Ndiye huyu hapa, picha yake haitofautiani sana na maneno yake!​
teh he hehe he! Mkuu baaasi. Mi nilidhani atakua hata ni mtu anayeweza kushaurika akipewa ushauri ila hawa wa dizain hii ni pasua kichwa. Tumwache atumie uhuru wake wa kikatiba huku 2015 inajongea. Even his mouth explained itself..
 
Katumwa na wanaomlipa, huyu Dr feki hasomi alama za nyakati. Anazuia mafuriko kwa mchanga! Shauri yake.
 
Bado mpaka sasa sijajua ni kwa nini msomi yoyote akiamua tu kuwa CCM hapohapo anakuwa zezeta!!

Huu ujinga alitakiwa auseme mtu mbumbumbu kama Tambwe Hiza ili tusishangae sana lakini mtu kama Dr.Benson Bana ni aibu.

Kifupi M4C itaendelea kwa kasi ya ajabu mijini na vijijini kwa kuwa watanzania waliochoshwa na utumwa wa CCM wa miaka 50 wanakiu ya mabadiliko kupitia Chadema, hivyo kama roho unamuuma sana akaungane na Mwigulu kwenye kampeni ya kuvalisha mbwa bendera.
 
CCM na serikali yake imekabwa koo, sasa inatumia vibaraka wake kuomba huruma. Aseme tu kama kuna sheria imevunjwa, vinginevyo akae kimya.

Ila CUF nao wamezidi kuiga kuliko hata mume wao CCM, walianza wote kuiga matumizi ya Helkopta, sasa leo wanaiga kuchangisha pesa(harambe),
sasa mpaka V4C .
Mkuu kwani aliyeanzisha hizi harakati ni chama gani kati ya CUF na CHADEMA?nakusudia kabla ya M4C na V4C!!
 
du, sasa nimeamini kuwa nastahili kuwa na digree moja tu, kuwa dr halafu unaishia kubaki kutokufahamu unafanya nini ni kitu cha ovyo kabisa, walisema wenyewe vyama vya upinzani ni vyama vya msimu, wakasema tena vyama upinzani havipo vijijini, CHaDEMa wameamua kufanya kazi tafiti za hao wanaojiita madocta wakabadilika na kuwa cha hai kinachofanya siasa muda wote na kufungua ofisi kila kijiji mfano lindi na mtwara du kufika moro jamaa wameananza kuua watu, nalia namkumbuka Prof, Chachage uwi!!!!
 
msajili wa vyama aliwahi kusema hatasita kuvifuta vya visivyofanya siasa,sasa huyu bana anafikiri kufanya siasa kwa sasa ni kucheza kiduku.
 
Back
Top Bottom