Dk. Bana awajia juu CHADEMA/CUF kuhusu M4C & V4C

huyu mzee Bana anazeeka vibaya..bila shaka anatamani mtabiri maarufu angekuwepo ili wasaidiane kufanya study inayopendelea magamba...mawazo ya Bana hayana tija
 
images

Ndiye huyu hapa, picha yake haitofautiani sana na maneno yake!

Asante Mkuu kwa hii picha, Jinsi jamaa alivyo na sura ya hovyo kama meno na maneno yake, itabidi ni i print ili watoto wangu wakianzia kulia niwatishie kwa picha ili wanyamaze.
 
Kwa hiyo ana kubaliana na kauli mbiu ya ccmweli ya kuwakandamiza wapinzani kwa kutumia polisi?
 
Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu 2010 ni takribani miaka 2 lakini serikali ya ccm haijatekeleza japo asilimia 10% ya ahadi zake. M4C ya Chadema na hiyo V4C ya cuf hazijaizuia ccm kutekeleza ahadi zake. Vyama vya siasa vitafanya kazi zao sambamba na serikali ikitekeleza mipango yake. Kama wameshindwa majukumu yao wasitafute kisingizio cha M4C ama V4C.
Kama vipi ccm na serikali yake waanzishe Manifesto 4 Completion.
 
du, sasa nimeamini kuwa nastahili kuwa na digree moja tu, kuwa dr halafu unaishia kubaki kutokufahamu unafanya nini ni kitu cha ovyo kabisa, walisema wenyewe vyama vya upinzani ni vyama vya msimu, wakasema tena vyama upinzani havipo vijijini, CHaDEMa wameamua kufanya kazi tafiti za hao wanaojiita madocta wakabadilika na kuwa cha hai kinachofanya siasa muda wote na kufungua ofisi kila kijiji mfano lindi na mtwara du kufika moro jamaa wameananza kuua watu, nalia namkumbuka Prof, Chachage ........daah namkumbuka pro. wa ukweli. kwake yeye chepe lilikuwa chepe tuu.R.I.P SEITH.KWELI UMETUACHIA MAKUADI WA SOKO HURIA. Viaondoka vichwa yanaachwa makombamwiko puuuuuh
 
Na Datus Boniface

Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana amevijia juu vyama vya siasa na kukosoa kauli mbiu zao ikiwemo ya Movement for Change (M4C), inayotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo na V4C ambayo inatumiwa na chama cha Wananchi CUF, kuwa siyo wakati wake kwa sasa.

Hivyo,waiache serikali iliyoko madarakani chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza ahadi na ilani zake kwa Wananchi.

Dk. Bana alisema hayo jijini Dar es Salaam leo katika semina ya siku moja yenye kujadili masuala ya Sheria kwa vyama vya siasa iliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

“M4C siyo wa halali siyo wakati wake kwa sasa, kama kila chama kitakuja na Kauli Mbiu yake itaipeleka nchi pabaya, Wananchi wana matatizo mengi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa sasa badala ya mikutano inayofanywa na vyama vya siasa” alisema.

Kwa mujibu wa kauli yake, Kauli Mbiu hizo zina wakati wake ikiwemo kipindi cha kampeni za uchaguzi.

Alienda mbali zaidi na kuwataka viongozi wa vyama hivyo kuiacha serikali itekeleze ahadi zake kwa uhuru na amani.

Huyu kada bado ana matumaini ya kupewa ukuu wa wilaya maana ana kera mno
 
Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu 2010 ni takribani miaka 2 lakini serikali ya ccm haijatekeleza japo asilimia 10% ya ahadi zake. M4C ya Chadema na hiyo V4C ya cuf hazijaizuia ccm kutekeleza ahadi zake. Vyama vya siasa vitafanya kazi zao sambamba na serikali ikitekeleza mipango yake. Kama wameshindwa majukumu yao wasitafute kisingizio cha M4C ama V4C.
Kama vipi ccm na serikali yake waanzishe Manifesto 4 Completion.
na kutotekeleza hizo ahadi kwa kasi inayostahili kunakipa CDM kazi ya kuwafafanulia wananchi hayo na hiyo ndio siasa, na ndio maana CCM hawataki hilo kwa kuwa udhaifu wao unazidi kuwekwa hadharani!
 
Huyo nae ni wa kumouuza tu, tunapo hangaika nae anajiona na ni mtu wa maana sana kaytika siasa za tanzania,
 
du, sasa nimeamini kuwa nastahili kuwa na digree moja tu, kuwa dr halafu unaishia kubaki kutokufahamu unafanya nini ni kitu cha ovyo kabisa, walisema wenyewe vyama vya upinzani ni vyama vya msimu, wakasema tena vyama upinzani havipo vijijini, CHaDEMa wameamua kufanya kazi tafiti za hao wanaojiita madocta wakabadilika na kuwa cha hai kinachofanya siasa muda wote na kufungua ofisi kila kijiji mfano lindi na mtwara du kufika moro jamaa wameananza kuua watu, nalia namkumbuka Prof, Chachage ........daah namkumbuka pro. wa ukweli. kwake yeye chepe lilikuwa chepe tuu.R.I.P SEITH.KWELI UMETUACHIA MAKUADI WA SOKO HURIA. Viaondoka vichwa yanaachwa makombamwiko puuuuuh

the best swahili novel,
pia usimsahau prof Haroub Othman,kuna siku SHIVJ ALISOMA SHAIRI PALE UDSM AKASEMA KWANINI WANAKUFA WATU WAZURI AMBAO BADO WANAHITAJIKA???
 
Orijino komedi was session yao inaitwa LE PROFESSERI huyu mzee naona anasadifu mazingira hayo.
 
the best swahili novel,
pia usimsahau prof Haroub Othman,kuna siku SHIVJ ALISOMA SHAIRI PALE UDSM AKASEMA KWANINI WANAKUFA WATU WAZURI AMBAO BADO WANAHITAJIKA???
hakika kazi wameifanya kutuelimisha
kupumzika ni muhimu katika haya maisha
mwache Bana aharibu maana mapema atasahaulika
daima tutawaenzi walimu waliotukuka
walikuwa na madhaifu lakini bana unapitiliza
RIP chachange na othman daima tutawakumbuka!
 
“M4C siyo wa halali siyo wakati wake kwa sasa, kama kila chama kitakuja na Kauli Mbiu yake itaipeleka nchi pabaya, Wananchi wana matatizo mengi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa sasa badala ya mikutano inayofanywa na vyama vya siasa” alisema.

Yaani Tendwa ndio alitaka CHADEMA wakae chini kumsikiliza huyo Benson Bana? Huyu Benson Bana anakiri hajui ni kwanini uchumi wa Tanzania ni mbovu, wakati huo huo anasema wananchi wana matatizo mengi. Yote tisa, kumi, Benson Bana amenukuliwa akisema hajui CHADEMA wanataka nini?

Ah hebu nipate supu yangu maana vituko vya Benson Bana ni vingi mno. Hivi REDET yake imefikia wapi, I know wafadhlili walijitoa baada ya kuona ujuha wake.
 
Watu wa CCM wana tabu sana, wakati wa kampeni wanaviita vyama vya msimu i.e siasa zao wakati wa kampeni tu, leo wanawasha moto kila siku, wanalalamika sio wakati wake... Damned if you do, damned if you don't.
 
Kwani harakati za wapinzani zinawazuia nini Magamba kutekeleza ilani za Chama chao?? huyu naye mwehu....Alitaka hatakati ziwe wakati wa Kampeni?? Kilaza msomi - The Proffesori
 
Hii inadhihirisha wazi jinsi tunaowaita kuwa wasomi wa nchi hii wasivyokuwa na umuhimu katika mabadiriko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. CCM ndio wanaongoza dola, ndiyo yenye bajeti ya kufanya maendeleo kwa wananchi. Vyama vya upinzani kazi yake ni kuangalia makosa ya chama tawala na kuyatumia kuwaeleza wananchi ili chama tawala kichukiwe hivyo kutoa fursa kwa vyama vingine kushika dora kama wananchi wataona inafaa kufanya hivyo. Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugezi mbona wanafanya kazi za ukada wa CCM, mbona huyo Banana hajasema chochote? Cuf na Chadema kujiimarisha kwa kuwaambia wananchi ukweli na madudu yanayofanywa na ccm kunakosa gani? Kujiimarisha kwa kufungua matawi na kutafuta wanachama kuna kosa gani? Hilo linawazuia nini ccm kutekeleza sera au kuwatumikia wananchi? Huwezi kuamini kama ni msomi ndio katoa hoja yenye kupwaya kama hii.
 
mh!!!!!!!!!!,ukitaka upoteze hadhi kwenye mijadala km hii ijadili cdm vibaya!,sasa uko c kulazimishana kufikiri sawa!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom