Dk. Bana awajia juu CHADEMA/CUF kuhusu M4C & V4C

Dk. Bana awajia juu CHADEMA/CUF kuhusu M4C & V4C

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Na Datus Boniface

Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana amevijia juu vyama vya siasa na kukosoa kauli mbiu zao ikiwemo ya Movement for Change (M4C), inayotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo na V4C ambayo inatumiwa na chama cha Wananchi CUF, kuwa siyo wakati wake kwa sasa.

Hivyo,waiache serikali iliyoko madarakani chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza ahadi na ilani zake kwa Wananchi.

Dk. Bana alisema hayo jijini Dar es Salaam leo katika semina ya siku moja yenye kujadili masuala ya Sheria kwa vyama vya siasa iliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

"M4C siyo wa halali siyo wakati wake kwa sasa, kama kila chama kitakuja na Kauli Mbiu yake itaipeleka nchi pabaya, Wananchi wana matatizo mengi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa sasa badala ya mikutano inayofanywa na vyama vya siasa" alisema.

Kwa mujibu wa kauli yake, Kauli Mbiu hizo zina wakati wake ikiwemo kipindi cha kampeni za uchaguzi.

Alienda mbali zaidi na kuwataka viongozi wa vyama hivyo kuiacha serikali itekeleze ahadi zake kwa uhuru na amani.

​
 
Huyu mzee kila siku anazidi kujishushia hadhi
 

Kauli MBIU ??? Mimi naona ni MOJA ya UHAMASISHO wa kutaka MAENDELEO na kukifanya CHAMA TAWALA kwa MIAKA 32 na zaidi

KUAMSHWA na kuwatumikia Wananchi...
 
Sasa matatizo ya Wananchi yanatakiwa kutatuliwa na Vyama vya siasa au Serikali??? Suala hapo ni serikali itatue matatizo ya wananchi kwa kiasi cha kuridhisha, Funga Mafisadi wote jela, na komesha kabisa Ufisadi then hakutakua na need ya M4C wala nini....
 
Huyu Bana si arudi shule asome angalau aelimike? Nadhani baada ya kugundua kuwa kuna kustaafu, ameanza kujiuza kama kachangu ili lau CCM wamkumbuke na siyo kumtilia kichumvi atakapoomba kazi upya.
 
Bangi za kiziba kalii!.. Zinatesa watu mpaka uzeen!
 
Duh! huyu jamaa bomu sana naona anatafuta ULAJI kwa nguvu 2015....Juzi kaulizwa kwanini uchumi wa Tanzania unaanguka? Jibu lake likawa hajui ni kwanini uchumi unaanguka!!! kaficha ukweli ili kutoisema vibaya magamba!!! Na huyu inasemekana ni mchumi.
 
hivi kuna watu wanajivunia kufundishwa na huyu mpumbavu au ndiyo ukiwa ccm prof hana tofauti na wa la saba..kikwete alisema chadema ni chama cha msimu leo bana anatulazimisha tukae kimya ilitukamilishe usimi wa dr dr dr dr kikwete Bana akae kimya angalie siasa ninavyotendewa haki..
 
Nawapa pole waliopita kwenye mikono ya huyu zezeta! Mhadhiri anazidiwa na wanafunzi wake?! AIBUUUUU! Tumweke kwenye mzani na Deus K. tuone kama huyu Dr mwenye kichwa cha kufugia nywele hajapigwa gap!!
 
Na Kilimo kwanza sio Kauai Mbiu? Mbonahusemi ifutwe .......Huyu chizi kasomeni Majibu ya tafiti za Redet kuwa Vyama vya upinzani haviendi vijijini Ndio maana viko dhaifu, Leo anakuja na hoja kua visiende vijijini. Ili viendelee kuwa dhaifu? CDM mjibuni Huyu mwehu.........
 
Msomi asiye na elimu, dr Bana yule ni zuzu tu! Hajui maana ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Na kazi rasmi ya vyama vya siasa.
 
Vyama vya siasa lazima vitoe somo la uraia kwa wananchi yeye alitaka vinyamaze ili mwisho wa siku aseme vimeshinda kufanya kazi ya siasa.
 
anatapatapa kama kuku aliyekatwa kichwa nusu....Naona anapamba ateuliwe before 2015
 
Mwenye picha yake aitundike humu tafadhali.

images


Ndiye huyu hapa, picha yake haitofautiani sana na maneno yake!
​
 
CCM na serikali yake imekabwa koo, sasa inatumia vibaraka wake kuomba huruma. Aseme tu kama kuna sheria imevunjwa, vinginevyo akae kimya.

Ila CUF nao wamezidi kuiga kuliko hata mume wao CCM, walianza wote kuiga matumizi ya Helkopta, sasa leo wanaiga kuchangisha pesa(harambe), sasa mpaka V4C .
 
Back
Top Bottom