DJ Mark namba moja

DJ Mark namba moja

Mi ni msela ndo maana sina makuzi ya kichoko, nakupa somo bila hela kwasababu we ni mtoto mnoko.../

We ni dj unaye play ngoma za taarabu, na ndo maana hazisikiki kwenye hivi vilabu.../
msela gani wewe upo kigoigoi,huna future huna taste kama kiepe kilichokosa yai,ila unajitahid kukesha kama mimi,saa tisa hii au upo karantini?
 
ila siskii muvi zake saiv,mm naona kwa bongo Anayejua english vzur ni Ommy dj yan movie zake ni kali utamsikia"piga bao sasa weweeee"
MZEE WA ACHECHE, CHUKUA NAMBA MOJA

Na, Robert Heriel

Kila mtu duniani hupenda kazi yake ifurahiwe na watu wengine. Hakuna asiyetaka kazi yake isipendwe. Ndoto ya watu wengi duniani ni kuona kazi wazifanyazo zinapendwa na kufurahiwa na watu. Lakini kufurahiwa peke yake haitoshi bali kufurahiwa pamoja na kuijenga jamii. Sio kufurahiwa lakini hapo hapo inabomoa jamii.

Hata hivyo sio kila mtu anafanikiwa katika hili. Wengi hujikuta wakifanya kazi lakini hazifurahiwi wala kupendwa na watu wengine.

Moja ya vijana waliofanikiwa katika kazi zao ni pamoja na Hamad Abdulrahman Abdallah alimaarufu kama DJ MARK ambaye Taikon napenda kumuita Mzee wa Acheche kutokana na kupenda kutumia neno hilo mara kwa mara.

DJ Mark ananifurahisha sana, ni kijana mwenye kipaji cha kipekee ambacho bila shaka Watanzania wengi wanajivunia kuwa na mtu kama yeye.

DJ MARK ni msanii anayefanya kazi ya kutafsiri filamu zenye lugha ya kigeni kwenda Kiswahili.

Pengine mtu fulani anaweza kuniuliza kwa nini Taikon nampa DJ MARK namba moja katika kutafsiri Filamu hapa Tanzania. Sababu zifuatazo nitazitaja:

1. DJ MARK ANAUTAMBULISHO/ Identity
Katika utambulisho kuna utambulisho wa aina mbili kwenye kazi za utafsiri wa filamu;

i/ Utambulisho wa Sauti
Kazi ya kutafsiri Filamu inatumia sauti. Msanii yeyote katika fani hii ili awe mkubwa lazima ajitofautishe na wasanii wengine na kuwa na sauti yake. Dj Mark amefanikiwa kuwa na Utambulisho.

Akiitafsiri filamu hata ukiwa mbali unajua kabisa huyo ni Dj Mark. Katika hili Dj Mark ameweza kuigwa na baadhi ya vijana chipukizi katika fani hiyo ya utafsiri wa filamu. Kitendo cha kuigwa ni moja ya mafanikio ya wazi kwa DJ Mark.

Wengine waliofanikiwa kwenye Utambulisho wa Sauti ni pamoja na DJ AFRO wa Kenya, Juma khan(Huyu anapenda za wahindi) na DJ Murphy

ii/ Utambulisho wa Maneno/ Msamiati
Katika utafsiri wa filamu mbali na sauti pia kuna Msamiati wanayotumia watafsiri.

Msamiati unaweza kuwa utambulisho wa DJ katika kazi yake ya utafsiri. DJ Mark amefanikiwa katika hili kwa hapa Tanzania. Hakuna Mtafsiri mwingine hapa Tanzania mwenye Identity katika msamiati zaidi ya DJ Mark.

Neno "Acheche" ni utambulisho ambao DJ MARK anatambulika nalo. Popote utakaposikia neno hilo akili yako itakuja kwanza kwa DJ Mark ndio umfikirie anayelitaja.

Mbali na Acheche, Dj mark anamaneno fulani ambayo ni kama punchline, mfano "Mbaruku Toli" "Kudadadadeki" "Dubwana" kisha anamalizia na mlunzi. Hii inaleta ladha kwenye kazi ya usanii ya kutafsiri.

Marehemu Lufufu pia katika hili la msamiati alifanikiwa mno maneno kama "Mdebwedo" yalimbeba.
Huko Kenya DJ AFRO Kalidhibiti vyema soko lake kutokana na Identity yake ya msamiati. Mfano hupenda kutumia msamiati "olololoyae" "Ashalala" "Ooooraiti" "Chunga chana"

Utambulisho ndio kiini cha kwanza cha msanii yeyote katika sanaa. Mtu asiye na utambulisho hawezi kwenda mbali katika kazi yake.

2) Uchaguzi wa Filamu
DJ MARK anajua kupoint filamu za kuzitafsiri lengo ni kuhakikisha sisi Watazamaji wake na wasikilizaji hatujuti kuzitizama filamu anazotafsiri. DJ MARK anajua soko lake kubwa kwa sehemu kubwa ni vijana, na watu wa kipato cha chini na kati. Ambapo kimsingi watu hao hupenda Action Movies na sio zile filamu za kuongea mwanzo mwisho.

Filamu zenye mapigano makali ya kila mara, zenye stori kali ndizo anazipointi jambo ambalo linamfanya mtazamaji na msikilizaji kutaka zaidi na zaidi filamu alizozitafsiri.

Filamu za kutisha kama za mazombie, vampire, Horror movies ndizo anazipenda, na vijana wengi wa tabaka la kati na chini huzipenda.

3) Anajua kushirikisha Hadhira
DJ MARK kama Msanii atahakikisha Mtazamaji au msikilizaji wake ambaye ndiye hadhira kuwa anakuwa makini kufuatilia filamu. Anajua wapi aongee na wapi akuachie utazame mwenyewe. Anajua kukuamsha hisia na mchecheto wakati wa hatari inapotokea kwenye filamu. Hili pia DJ AFRO analimudu kwa sehemu kubwa.

Wasanii wengine wa utafsiri wa filamu hushindwa hapa. Wengine hupoa sana na kuifanya filamu usiipe umakini sana.

Nampongeza kwa kuweza kukitumia kipaji chake vizuri. Hii ni sehemu ya ajira lakini pia ni sehemu ya lugha kwani kazi yake kwa asilimia 50 inategemea lugha mbali na vifaa vya teknolojia.

Je, unafikiri ni Mtafsiri gani anashika nafasi ya pili baada ya DJ MARK? Dondoka hapo chini

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
0711345431

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ROBERT HERIEL,

Upo vizuri jamaa ila kwa sasa naona kama ameadimika..
Ila mtafsiri filamu mwingine ninayemkubali anajiita OMMY DJ jamaa naona ni wa Arusha yupo vizuri sana kwenye movies za kimarekani hasa za kivita na kijasusi. Jamaa naye anajua yupo serious na pia hata kwenye lugha. Hawa ma dj uchwara wanatafsiri sana uongo.

MÊmENtO HoMO
tuwekeee picha mkuu ya ommy dj

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je analipa kodi? na anafwata masharti ya hati miliki?
 
ROBERT HERIEL,

Upo vizuri jamaa ila kwa sasa naona kama ameadimika..
Ila mtafsiri filamu mwingine ninayemkubali anajiita OMMY DJ jamaa naona ni wa Arusha yupo vizuri sana kwenye movies za kimarekani hasa za kivita na kijasusi. Jamaa naye anajua yupo serious na pia hata kwenye lugha. Hawa ma dj uchwara wanatafsiri sana uongo.

MÊmENtO HoMO
Naiangalia movie yake moja hapa ya "The Game Of Thrones" Ommy D yupo vyema sana sauti ya simba jamaa anaunguruma kweli kweli lugha nayo《English》 kaisimamia vilivyo.
 
Kuna dj mmoja huwa ananifurahisha anavyotamka Kung Fu hustle,utasikia"muvi hii ya kong fu hustule"yaan ni shida anatamka kama ilivyoandikwa.english bado ni tatizo kwa wengi
 
ila siskii muvi zake saiv,mm naona kwa bongo Anayejua english vzur ni Ommy dj yan movie zake ni kali utamsikia"piga bao sasa weweeee"

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha!! vigwagizo vingine ni kama "ndani ya nyumba huyu ni Ommy D hapana shaka tunapiga bao, Waooooh, dooh, hutaki au, Wewe tu, Twende sawa, hakika ni kizaazaa, we cheki mambo hayo, mimi sina msaada nae/nao hakika nakwambia. Jamaa haboi namkubali sana hasa kwenye... The Knight Rider, Game Of Thrones, Lord Of The Rings, The Outpost n.k
 
Naiangalia movie yake moja hapa ya "The Game Of Thrones" Ommy D yupo vyema sana sauti ya simba jamaa anaunguruma kweli kweli lugha nayo《English》 kaisimamia vilivyo.
Kiufupi jamaa anajua sana .. yaani anakwambiq Marekani anaijua kuliko hata mama yake..... Ukute labda anatafsiri filamu ya kimarekani akianza kutaja mitaa na maeneo..na ukifuatilia kwa ku Google unakuta ni kweli .jamaa yupo vyema sana

MÊmENtO HoMO
 
Kuna mmoja anaitwa BABUU huyo wanamjua wengi wa Arusha. Nakuhakikishia ukibahatika kupata kazi zake hata moja hutajuta. Kuna movie moja iko youtube inaitwa CKANK 1. Ukibahatika kuangalia hata nusu saa,utatoa majibu kwa uwezo wa jamaa kutafsiri vema.. Muvi anaso deal nazo nyingi niza Action(kizungu) alafu Ommy yeye za kivita sana sana
 
zombies wanakuuuuuuujaaaa woouhuuu wakuchechemea hatarii ukipigwa na mruzziii wote mnarudi ndani.
afro majina wa watu tu nichekesho😅😅.
wakina kabdaa.odhobee.wololooo bila kusaaau wapishi wakuuu wakina maaenjaaaa
 
Kiufupi jamaa anajua sana .. yaani anakwambiq Marekani anaijua kuliko hata mama yake..... Ukute labda anatafsiri filamu ya kimarekani akianza kutaja mitaa na maeneo..na ukifuatilia kwa ku Google unakuta ni kweli .jamaa yupo vyema sana

MÊmENtO HoMO
hapana shaka
 
Back
Top Bottom