Dizasta Vina anaweza akawa ndio best rapper Tanzania

Hahaha,,

Mapangala samba/
Brazili samba/
Mbishi anatamba
na sultan tamba/

Bomoabomoa X/
Picha za ngono X/
Hata mpenzi wa zamani X/
Fransis cheka/

Bibi wa temeke cheka/

mayweather boksa/

Nguo ya ndani boksa/
 
Dah nimesikiliza kanisa na lost one,dah jamaa anajua nadhani watu wanaoku challenge kuhusu Fid watakua hawajamsikia
 
Sitaki gemu-Dizasta vina.

Hii Mboga imekosa chumvi,nikiweka ooh aliyeweka amebugi.
 
Huyu dogo toka nimemsikia kwenye kile kipindi cha dakika 5 bomba sijui 10 za eatv planet bongo nikatambua uwepo wake katika vijana wanayoiweza hihhop. Mbaya zaidi baada ya kugundua anatokea lunduno basi sikuwa na shaka na uwezo wake basi!
 
Vip Chindoman mkuu..naona sometimes anakaza sometimes analegeza
Anachofanya Chindo "Umbwa mzee, nyang'au" ni kutuumiza wapenzi wa hip hop tuliodhani hatabadilika! Ili poa, inabidi sasa muziki uanze kumlipa na maisha yaendelee. Kwakuwa Watengwa ndio kundi pekee Afrika lenye marapa zaidi ya kumi, naamini wengine wata-takeover!!
 
Siwafichi mpaka sasa Dizasta vina anaweza kuwa best real rapper Tanzania....take time umsikilize...Huyu jamaa kanifanya nifute nyimbo zote za wasanii kama kina Fid Q kwenye playlist yangu.
Siku mbaya,kanisa moja kat ya ngoma nnazo zisikiliza sana.Disasta yuko vzur ila si kwa kumfananisha na Ngosha.
 
Mimi si nawasikiliza tu.

Sisi ndio foundation wao walitusikiliza sisi kabla hawajawa hapa.

I was there when it all started, with Kwanza Unit, Hard Blasters, GWM,O Juice etc.

Back in the early nineties.
Hebu tupe history ya bongo hip hop

Kumbe ndo maana uko na uwezo Wa kupambanua mambo due to old skull hip hop +vitabu(literacy)
 
Wakati huo tunarekodi ama Mawingu Mwenge, ama Don Bosco Upanga ama Temeke Soundcrafters.

Halafu hapo ITV na Radio One ndiyo zinaanzishwa, tunaongea nao wanarekodi music video.

Videos kama za "Oya Msela" Mawingu Band/ O Juice, "Usiige Mambo ya Mjini" wa Hard Blasterz, "Pilika Pilika" wa Sossy B na "Cheza Mbali na Kasheshe" wa GWM zilikubalika sana.

Halafu tulifanya sana parties, mara nyingi za Beach, hususan Oysterbay. Beach ilikuwa inafunga watoto wa pande zote za Dar tunakutana, tunachanganyika, one love.

Baada ya hapo yakawa mashindano kama ya Kim Mgomelo "Yo Rap Bonanza" na ya Don Bosco Youth Festival. Vikundi vilikuwa vinajiandaa mwaka mzima kwa mashindano haya.

I was there when Mr 2 came to Dar from Mbeya, and Dar Young Mob took him in.

I was there with him at Don Bosco Studios, when he was recording one of his early albums.

Concerts za Korean Cultural Centre, Empire Cinema, ma beach parties zilifana sana. Lakini watu wengi walichukulia muziki kama sehemu ya kufurahia maisha tu, ulikuwa haujawa biashara bado.

Mtu aliyekuja kuanza kufanya kweli kwenye biashara alikuwa Mr. 2. Alideal na wahindi wa Dar, wakamtengenezea kaseti na kuziuza nchi nzima, baada ya yeye kupewa chajuu. Lakini alidhulumiwa sana kwa sababu alikuwa hana control baada ya kuwapa masters zake wahindi.

Mr. 2 alianza kupata mafanikio ya kibiashara, ingawa alikuwa si mtoto wa Dar, na alivyokuja alikuwa anafanya kazi kwenye petrol station kabla hajawa maarufu.

Kuna watoto wa Dar waliokuwa wameanza kufanya Hip Hop (enzi hiyo jina Bongofleva halikuwepo) kabla ya Mr. 2 wakina Kwanza Unit, Hard Blasterz, Dar Young Mob (ambao Mr. 2 alijiunga nao) na hata kabla zaidi, Saleh Jabri alijirekodi kwenye instrumental ya Vanilla Ice "Ice Ice Baby".

Kitu kingine kikubwa kilikuwa kupeleka Chrome tapes Radio One, zipigwe redioni. Taji Liundi alikuwa Radio DJ aliyepokea tapes za wasanii wengi sana na kupiga nyimbo zao redioni.

Siku hizo Taji akikuchagua na kupiga nyimbo zako katika kipindi cbake cha DJ Show, unakuwa maarufu sana, kwa sababu kipindi kinasikilizwa na watu wengi sana.

Baadaye kipindi hiki kikaja kuendeshwa na Mike Muhagama, ambaye nafikiri ndiye aliyeanza kutumia neno "Bongo Fleva"
 
Wakati huo tunarekodi ama Mawingu Mwenge, ama Don Bosco Upanga ama Temeke Soundcrafters.

Halafu hapo ITV na Radio One ndiyo zinaanzishwa, tunaongea nao wanarekidi music video.

Duuh

Najenga Picha jinsi mlivyo enjoy back then

Sasa wewe ulikua nani

Rapper,producer ,DJ or?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom