Tanganyika ilizaliwa 9th Dec, 1961. Baadaye ikaungana na Zanzibar kufanya muungano wa Tanzania. Serikali ya Tanganyika iliunganisha kwenye serikali ya muungano, kwa hiyo hapo tunasherekea Uhuru wa Tanganyika ambayo ni Tanzania vilevile. Tar 26.04.2014 tutasherekea Muungano wa Tanzania na wala siyo Uhuru wa Tanzania. Kwa kifupi Tanganyika ilipata jina la Tanzania, lakini umri unabaki palepale. Kuna Uhuru wa Tanzania na Muungano wa Tanzania.
Ni nchi gani lilpata uhuru desemba mosi 1961????
Je Tanzania imetokana na nini?
Je Tanganyika ndo Tanzania siku hizi?
Nini asili ya jina Tanzania???
- Nchi iliyopata uhuru Decemba mosi 1961 ni TANGANYIKA
- Tanzania ni muungano wa majina mawili taani TANganyikaZANzibarIA
- Tanganyika ni sehemu ya Tanzania na herufi zake tatu za mwanzo zilichukuliwa kuunda jina la Tanzania.
- Asili ya jina la Tanzania ni muungano wa majina ya TANGANYIKA na ZANZIBAR.
Hii kazi kweli kweli, kwahiyo ikifika tareh 26.04.2014 ni miaka 50 ya muungano.

Hapo hapo,je bendera ya Tanganyika ndiyo hiyo inayotumika kama ya Tanzania?Wimbo wa Tanganyika ndiyo unaotumika kama wimbo wa Tanzania ya sasa?Katiba ya Tanganyika iliwahi kuwepo maana Zanzibar walianza na presidential decree,je katiba hiyo inafaa?

WANA JF nakumbuka wakati ninasoma UDSM niliwahi ongea na kujadiri kitu kuhusu Tanganyika lkn ndugu zangu wanafunzi wengi waliniita mimi msaliti na mkabila mpaka wakarefer kabila langu. Sasa LISSU msishangae anapoambiwa maneno kama hayo.

Kiufupi Tanganyika ilikufa na hakuna watu wa Tanganyika labda Watanzania Bara, je hii ni sahihi? IKUMBUKWE TULISHANGILIA SANA KUZALIWA SOUTHERN SUDAN, LINAPOKUJA KWETU BASI TUNAONA TABU, POLITICAL HYPOCRACY.
Una hoja ya msingi, lakini simpo mathematics ukihesabu miaka hamsini kufikia Desemba 9, 2011 unajua ni nchi gani inazungumzwa. Tusichokoze Muungano.