Fredrick Sanga
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 3,153
- 697
<br />
<br />
Haya tunayoyashuhudia leo ni matokeo ya udikteta wa Nyerere ambaye watu wameaminishwa kwamba ni baba wa taifa. Je ni taifa lipi? Kama ni taifa la Tanzania kwa nini Karume naye asiitwe hivyo? Muungano haukutokana na matakwa ya watu wa Tanganyika wala wa Zanzibar, hapakuwa na kura ya maoni bali ni makubaliano tu ya Nyerere na mwenzie Karume.
Kwa nyakati zile inawezekana kuwa wazo la muungano lilikuwa sahihi lakini kwa mwenye upeo hata wa wastani tu anajua kuwa leo muungano hauna tija. Ni ujinga wa kupindukia kwa wanasiasa wa hovyo wa Tanganyika kufanya jina hilo lionekane kama jinai kulitamka na badala yake watu wamezoezwa kusema Tanzania Bara wakati Zanzibar wanatumia jina lao lilelile.
Ni mawazo duni kuamini kuwa eti muungano ukivunjika hatutakuwa salama, nani ana ushahidi wa hilo? Wala hakuna haja ya serikali mbili wala moja wala tatu; Tanganyika turudi kuwa nchi yetu na Zanzibar waendelee na ya kwao, ubaki ushirikiano wa nchi jirani. Inashangaza ukienda Zanzibar unakuta wana mifumo na taasisi zao aidha tofauti na za kwetu au zinazolingana na za kwetu halafu watu wenye akili timamu bado wanazungumza kana kwamba hii ni nchi moja.
Lazima Watanganyika tudai jina letu, bendera yetu, wimbo wetu wa taifa na nembo ya jamhuri yetu. Muungano ni sinema tu ya mchana, hakuna kitu kama hicho ndiyo maana hata Vasco da Gama akienda kule visiwani ni kama kiongozi tu wa nchi jirani amepita kuwajulia hali, hana mamlaka yoyote.
Naamini itakuwa vyema zikipatikana bendera ndogo za Tanganyika tuzipepee siku ya uhuru.
Mod Naomba ustick hii suala, Usiogope, Litasaidia sana katika katiba mpya.
Hii ndio habari nzito sana. tunadanganywa kama vitoto vidogo. Haiwezekani kabisa serikali ya Zanzibar ikabakia hakafu ya Tanganyika ikauawa, halafu tusherkehe uhuru wa Tanganyika. Tanganyika has been recolonised by few people. No need of this celebration. Till we get our state back.