Disemba 9 kila mwaka: Tunasherehekea uhuru wa nchi ipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Disemba 9 kila mwaka: Tunasherehekea uhuru wa nchi ipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BABA JUICE, Nov 20, 2010.

 1. BABA JUICE

  BABA JUICE JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tanzaniza ni muungano wa nchi mbili,kuna Zanzibar na Tanganyika na wote tulipata uhuru nyakati tofauti.Inanichanganya nikisikia watu wanasema miaka 49 ya uhuru wa Tanzania.

  Msaada wenu unahitajika sana,nipe elimu mimi sijui faida za muungano lakini nitalinda na kuheshimu mawazo ya wazee wangu na kutetea muungano kwani wote ni wamoja kihistoria mkoloni ndio alileta utofauti.

  Usinipotoshe niambie ni Tanganyika au Tanzania
  .
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Tatizo tanganyika yetu imemezwa bila sababu ya msingi.zanzibar ipo na mambo yake ya msingi tanganyika hakuna kitu!siasa tuu za tanzania huku ZAN hana nia ya dhati ya muungano
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Nov 20, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ni tanzania bara!
   
 4. sbilingi

  sbilingi Senior Member

  #4
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani umelazimishwa, hata mke akimchoke mwezi wake anamba kutengana!!!!!!!!!!!
   
 5. BABA JUICE

  BABA JUICE JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni tanzania bara! bado sijaelewa
   
 6. Z

  Zahor Salim Member

  #6
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Uhuru wa tanganyika kabla ya 1964 kulikuwa hakuna tanzania. Tanzania ilizaliwa 26/4/1964.
  Kabla ya hapo kuliwa hakuna nchi ikitwa tanzania wala tanzania bara. Sasa semeni tunasherehekea uhuru wa tanganyika
  uliopatikana dec 1961
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Nov 21, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tunasherehekea uhuru wa sehemu mojawapo ya Tanzania, yaani, Tanzania Bara ambayo zamani ilikuwa inajulikana kama Tanganyika.

  Kwa Kiingereza sentensi hiyo inasomeka hivi:

  We are celebrating the independence one of the parts that constitutes Tanzania, that is, Tanzania Mainland, formely known as Tanganyika.
   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikisikia na kusoma ya kwamba mwaka huu Tanzania inasheherekea miaka hamsini ya uhuru wa iliyokuwa Tanganyika. Kulingana na kumbukumbu zangu, maana nilikuwa tayari ni mtu mzima, uhuru wa Tanganyika ulipatikana katika awamu tatu; kwanza yalipatikana madaraka ya ndani mwaka 1960; baadaye ukapatikana uhuru tarehe 9/12/1961; na hatimaye ikapatikana jamhuri tarehe 9/12/1962.

  Tatizo langu ni kwamba wakati uhuru ulipopatikana mwaka 1961, Malikia aliendelea kuwa mkuu wa nchi; na hivyo Gavana aliendelea kubaki hapa nchini akimwakilisha huyo malikia. Mambo yalibadirika mwaka 1962 baada ya Tanganyika kuwa jamhuri; hapo ndipo rais wetu alianza kushika nyadhifa zote mbili za mkuu wa nchi na mkuu wa serikali.

  Kwangu mimi huo ndiyo mwaka ambao Tanganyika ilipata uhuru kamili. Kwa mantiki hiyo mwaka huu tutasherekea miaka 50 ya uhuru na mwaka ujao tutasherekea miaka 50 ya uhuru kamili. Hapa ninachozungumza bila shaka ni uhuru wa bendera, maana uhuru wenyewe bado unatupiga chenga.
   
 9. LUKAZA

  LUKAZA Senior Member

  #9
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 136
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Wzanzibar munao ishi UK kweli Tunashindwa kui-advertisement Zanzibar indipendence?

  Kufanya jambo hili ni moja ktk mikakati ya kuwafumba mdomo hawa Wtanganyika wenye kuishukuwa historia ya uhuru wao na kuingiza ktk historia ya Muungano fake wa Tanganyika na Zanzibar.

  Ili wajuwe December 1961 ni uhuru wa Tanganyika sio Tanzania? Sasa na nyiyi mukishapicha matangazo yetu hapo Uk ya uhuru wa Zanzibar 1964 mutawaziba mdomo hawa matapeli?.[​IMG][​IMG]

  Ukweli haufischiki kaka hii ndo hali wazanzibar imefika wakati wa kuamka wakati ndo huu hawa tukiwalegezea watazowe CHADEMA KAZENI KASI ya kuiokoa Serikali ya Tanganyika hawa CUF washashiba Umakamo wa kwanza wa Rais hawasikii chochote sasa du inauma sana kwa wazanzibar.
   
 10. M

  Makemba Member

  #10
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni muhimu kuzidisha kilio cha kudai Tanganyika na tujivunie nayo kama wao wanavyopenda kujinadi na Uzanzibar wao!
   
 11. n

  ngoko JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Songa mbele kuchapisha vipeperushi UK ; siku ikifika viteremshe Zenji watu washerehekee uhuru wao; Kama Kawaida tutakuja kufanya gwaride maana ninyi ni wenzetu/ndugu zetu
   
 12. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Mwaka 2011 ni miaka hamsini tangu uhuru wa Tanganyika ulipopatikana. Naomba niulize: Tutasheherekea kivipi? Uhuru wa Tanganyika au wa nji hii ya Tanzania ambayo inatimiza miaka 47?
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Rungu, Tungo tata hilo!!!!!!
   
 14. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Si uongo. Swala hili limenikwaza mazee!
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Machozi kurudi tumboni kwa miaka 50!!!!!!!!!!!!!!!
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Look at it this way: tunasherehekea uhuru wa miaka 50 ya Tanganyika ambayo miaka mitatu baadaye ilibatizwa na kuwa Tanzania. How does that sound?
   
 17. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #17
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Nadhani hata kwa serikali swala hili lina utata ndio maana hakuna msisimko wa kuusheherekea huu mwaka, kama vile nchi nyingine za kiafrica zilivyofanya.
   
 18. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #18
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Personally I would rather that we celebrate 50 years of Tanzania's independence, although that does not sound right historically.
   
 19. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #19
  Jan 1, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mmechelewa. the wright person wakumuuliza hili swali ni the late nyerere au labda amani kwa mbaaaali. Pole.
   
 20. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #20
  Jan 1, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Asante!
   
Loading...