Discordant Couple

laussane

JF-Expert Member
Oct 8, 2009
255
0
Habari zenu wapendwa,

Naomba msaada, mimi na mme wangu ni discordant couple, tuligundua miaka 2 ya nyuma wakati mimi mjamzito na tulipoenda kupima ndio tukapata majibu hayo, tuna mtoto 1 na sasa hivi tumefikiria kupata mtoto wa 2, tangia tumegundua hilo tunatumia condom tu mpaka leo hii.

Tumeenda kwa daktari wa kina mama ametuambia tunaweza kupata mtoto wa pili kwa njia ya kujamiina ya kawaida lakini mimi amenipa dawa ambazo zitasaidiwa kupevusha mayai mengi kwa wakati mmoja ili uwezekano wa kupata ujauzito uwe mkubwa.

Jamani naombeni mawazo yenu kuna yeyote aliwahi kufanya hivo akafanikiwa na hakupata maambukizi? Na kitaalam hii ni njia sahihi? Au kuna yeyote anafaham njia nyingine tofauti na hii?

Doctors wa JF naomba mnipe maoni yenu
 
usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
500
Duh! Hizi vitu zinakuwaga ngumu hata kutoa ushauri. Huyo mwenye tatizo anatumia dawa? Manake kama hamkuambukizana kabla ya kutumia dawa kuna chance kubwa ya kutoambukizana. Fateni ushauri wa daktari kwani predictability ya kutokea mchubuko ni ngumu. Gud luck and God bless you. I can assume how hard it is.
 
laussane

JF-Expert Member
Oct 8, 2009
255
0
Kweli it is very hard, hatumii dawa na ana CD4 za kutosha tu, na kwa muonekano yuko safi tu
 
usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
500
Kweli it is very hard, hatumii dawa na ana CD4 za kutosha tu, na kwa muonekano yuko safi tu

in that case its hard kwa kweli. Maana mtu anayetumia arv anakuwa na low viral load chini sana hivyo kupunguza chance ya maambukizi. Do a thorough consultation to your doctor kwa case hiyo.
 
HoneyBee

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
912
1,000
Pole sana!

Kwahiyo mme wako ni HIV+? Mtoto wenu ni + pia? Itabidi ufuate ushauri wa madaktari, nisingekushauri kutafuta ushauri humu ndani kwa mambo kama haya. Jaribu kuonana na wataalamu kwenye hospitali mbalimbali ili ujue options zako . Best of luck!
 
Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,367
1,250
kwa heshima naomba Invisible hii thread uihamishie jukwaa la mmu maana huyu mdau kwa kweli anaitaji ushauri wa hali ya juu
humu wadau wengi hawaji
natanguliza shukrani
 
Last edited by a moderator:

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,367
1,250
Dr Riwa where are u?
Dr Riwa MUDA WOTE YUPO MMU ANAMENDEA TU MADEMU MLE,ndo maana nimemuomba Invisible hii post aipeleke tu kule maana huku watu wengi hawaji na unavoona mdau hapa anaitaji ushauri makini..afya ya mtu bwana ni jambo la msingi sana!
 
Last edited by a moderator:

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,367
1,250
There are currently 22 users browsing this thread. (4 members and 18 guests)

back to topic mi nashauri abaki tu na huyo mtoto alieko nae maana katika kutafuta huko anaweza kukutana na mengine mazito!
by the way tuwe honest! hivi walipopima majibu yangekuwa mwanaume negative na mwanammke ndo yupo positive hii ndoa ingekuwepo kweli?
 
Riwa

JF-Expert Member
Oct 11, 2007
2,597
2,000
Kweli it is very hard, hatumii dawa na ana CD4 za kutosha tu, na kwa muonekano yuko safi tu

in that case its hard kwa kweli. Maana mtu anayetumia arv anakuwa na low viral load chini sana hivyo kupunguza chance ya maambukizi. Do a thorough consultation to your doctor kwa case hiyo.

Dr Riwa MUDA WOTE YUPO MMU ANAMENDEA TU MADEMU MLE,ndo maana nimemuomba Invisible hii post aipeleke tu kule maana huku watu wengi hawaji na unavoona mdau hapa anaitaji ushauri makini..afya ya mtu bwana ni jambo la msingi sana!

Samahanini kwa kuchelewa kuitikia wito..Smile, Dr Riwa is single and searching, usiwe na wasi kuwepo kwangu kule nikisalandia dogo dogo!

Tuache utani, am serious now....kwanza pole da Laussane na hongera kwa ujasiri wako na mapenzi ya kweli kwa mumeo, si wanawake/wanaume wengi hubaki na wenzi wao pale mwenza anapokuwa ameambiukizwa VVU. Hongera sana. Nilishawahi kuongelea discordant couples humu, nimetafuta ule uzi wala sikukumbuki tena, sijauona. Ila naomba niwe specific kwa scenario hii yako.

Ni kweli discordant couple wanaweza pata mtoto hasiye na maambukizi ya VVU na pia bila mama kuambukizwa (kama Baba ndiye muathirika kama kwenye scenario hii). Tatizo ni kuwa, mwanamke kutokana na maumbile yake, ana risk kubwa zaidi ya kuambukizwa akikutana na mwanaume mwenye VVU, kiliko ambavyo mwanaume anaweza kuambukizwa akikutana na mwanamke mwenye VVU. Na hii ni sababu...uke una ngozi laini kulinganisha na na ngozi ya uume, hivyo ni rahisi kuchubuka. Pia Kutokana na maumbile, manii (shahawa) humwagwa ukeni, na VVU huwa kwenye majimaji ya shahawa, kama kuna mchubuko wa ngozi ya uke (ambayo ni delicate), then shahawa zina muda wa kutosha wa kupenya na kuinfect mwanamke. Condom huzuia shahawa kumwagwa ukeni na hivyo kumkinga kukukinga.

Utakapoacha kutumia Condom ili mzae, hiyo effect niliyoelezea hapo juu bado inahold. Kupewa dawa za kupevusha mayai ready for fertilization, inaongeza uwezekano wa wewe kushika mimba at first attempt, na hivyo kutapunguza ninyi kujaribu jaribu mara nyingi ili kupata ujauzito kwani kufanya hivyo kunakuongezea risk ya kuambukizwa....but still, dawa hizo hazikuzuii kuambukizwa katika hiyo first attempt. Bado kuna risk ya kuambukizwa iwapo utapata mchubuko na shahawa zikamwagwa ukeni na kubaki huko.

Nia salama kabisa ya kuzaa kwa discordant couples ambazo mwanaume ndio muathirika..ni kufanya in-vitro fertilization (IVF)...ambapo mwanaume atatoa shahawa kwa kujicua kwanye chombo maalum, na yai la mwanamke litakuwa harvested, kisha fertilization inafanyika nje...na fertilized egg inakuwa planted kwa mwanamke. Hii huwezi kabisa kupata maambukizi kwa kuwa...VVU wapo kwenye maji maji ya maniii/shahawa, na sio kwenye mbegu (sperm cell), na kwenye IVF wanavuna sperm cell, hivyo huwezi ambukizwa. Problem ni kuwa...IVF ni expensive (sijui economic status yenu, sio expensive sana kwamba its not affordable), lakini ndio salama kabisa...na hizo njia nyingine zilizobaki zinapunguza uwezekano wa kuambukizwa..but still the risk is there.

Karibu kwa maswali zaidi, au hata PM iwapo kuna amabayo hutapenda share jamvini.
 
nashukuru sna dr wetu . nimeona hupatikani kabisa ila post ilivoletwa humu mmu fasta nimekuona online ...ahaaa
ila najisikia amani sasa kwa majibu yako kwa huyu mdau
hii ndo jf kisiwa cha busara
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,347
2,000
Njia salama kabisa ya kuzaa kwa discordant couples ambazo mwanaume ndio muathirika..ni kufanya in-vitro fertilization (IVF)...ambapo mwanaume atatoa shahawa kwa kujicua kwanye chombo maalum, na yai la mwanamke litakuwa harvested, kisha fertilization inafanyika nje...na fertilized egg inakuwa planted kwa mwanamke. Hii huwezi kabisa kupata maambukizi kwa kuwa...VVU wapo kwenye maji maji ya maniii/shahawa, na sio kwenye mbegu (sperm cell), na kwenye IVF wanavuna sperm cell, hivyo huwezi ambukizwa. Problem ni kuwa...IVF ni expensive (sijui economic status yenu, sio expensive sana kwamba its not affordable), lakini ndio salama kabisa...na hizo njia nyingine zilizobaki zinapunguza uwezekano wa kuambukizwa..but still the risk is there.

Karibu kwa maswali zaidi, au hata PM iwapo kuna amabayo hutapenda share jamvini.

I didn't know that aisee...!!!!

ok..maan mi nlikua nafikiria ni kitu simpo sana..wapige game kwa mpira akikaribia kufunga anavua gloves!!! kumbe ingekua balaaa.....
thnx dr. Riwa.

Naona dr. MziziMkavu yuko bize na hepi besidei!!!! au yy sio 'mtaaalamu wa magonjwa ya kina mama na watoto?:becky:'
 
Last edited by a moderator:

Neylu

JF-Expert Member
May 28, 2012
2,943
2,000
Nimependa sana maelezo ya Dr. Riwa..!!

Natumaini yatamsaidia huyu dada..!!
 
Riwa

JF-Expert Member
Oct 11, 2007
2,597
2,000
There are currently 22 users browsing this thread. (4 members and 18 guests)

back to topic mi nashauri abaki tu na huyo mtoto alieko nae maana katika kutafuta huko anaweza kukutana na mengine mazito!
by the way tuwe honest! hivi walipopima majibu yangekuwa mwanaume negative na mwanammke ndo yupo positive hii ndoa ingekuwepo kweli?

Smile ulivyon'shupalia leo...nakoma!

Tusiende huko kwenye red tafadhali...katika uDaktari wangu nimeona discordant couples nyingi, lakini hizi experience mbili zilinitoa chozi:

- Couple ya kwanza walikuwa walokole wawili, walikuwa wanataka kuoana, hivyo wakaja pima afya zao. Nikawapa ushuria nasaha na wakawa tayari kupokea majibu...mdada akawa positive, na kaka negative. But kaka akasema atamuoa huyo dada, na watasali ataponywa au atalindwa hasipate maambukizi. Nikwaelekeza jinsi ya kujilinda but kaka akasema no need, sala zitawalinda. Nikasikitika. Nikawa nawafuatilia, wakaoana, wakawa wanakutana kimwili bila kinga, na baada ya miezi ^ kaka akawa positive. Alilia sana lakini ndio hivyo, sasa wako wanatumia dawa, wana mtoto mmoja hasiye na maambuki kwani dada alipopata ujauzito alifuata mpango wa kuzuia maambukizi kwa mtoto!

- Couple ya pili walikuwa wanandoa, mdada alijifungua, lakini akaumwa sana baada ya kujifungua, nilipowaona alikuwa na dalili za HIV, nikawapa ushauri nasaha wakakubali kupima, na majibu ni kuwa dada ni positive, na kaka ni negative, dada aliendelea kuugua kwa muda lakini alifariki baadaye...lakini yule kaka wakati wote wa alimuuguza mkewe kwa mapenzi makubwa..nilikuwa nikimuona wodini nilikuwa natamani kama ndoa zote zingekuwa na upendo vile, bahati mbaya mtoto ameambukizwa (kwa kuwa hawakujua na hawakufuata mpango wa kuzuia maambukizi kwa mtoto)...baba yupo, bado negative anamlea na kumuuguza mwanae. Mtoto ana miaka 8 sasa, anasoma.
 
Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,845
2,000
I didn't know that aisee...!!!!

ok..maan mi nlikua nafikiria ni kitu simpo sana..wapige game kwa mpira akikaribia kufunga anavua gloves!!! kumbe ingekua balaaa.....
thnx dr. Riwa.

Naona dr. MziziMkavu yuko bize na hepi besidei!!!! au yy sio 'mtaaalamu wa magonjwa ya kina mama na watoto?:becky:'
Mkuu Mentor Mimi bado ninasheherekea Happy Birthday yangu huku nimemuachia mkuu Dr.@Riwa afanye vitu vyake ..............
 
Last edited by a moderator:

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,367
1,250
Smile ulivyon'shupalia leo...nakoma!

Tusiende huko kwenye red tafadhali...katika uDaktari wangu nimeona discordant couples nyingi, lakini hizi experience mbili zilinitoa chozi:

- Couple ya kwanza walikuwa walokole wawili, walikuwa wanataka kuoana, hivyo wakaja pima afya zao. Nikawapa ushuria nasaha na wakawa tayari kupokea majibu...mdada akawa positive, na kaka negative. But kaka akasema atamuoa huyo dada, na watasali ataponywa au atalindwa hasipate maambukizi. Nikwaelekeza jinsi ya kujilinda but kaka akasema no need, sala zitawalinda. Nikasikitika. Nikawa nawafuatilia, wakaoana, wakawa wanakutana kimwili bila kinga, na baada ya miezi ^ kaka akawa positive. Alilia sana lakini ndio hivyo, sasa wako wanatumia dawa, wana mtoto mmoja hasiye na maambuki kwani dada alipopata ujauzito alifuata mpango wa kuzuia maambukizi kwa mtoto!

- Couple ya pili walikuwa wanandoa, mdada alijifungua, lakini akaumwa sana baada ya kujifungua, nilipowaona alikuwa na dalili za HIV, nikawapa ushauri nasaha wakakubali kupima, na majibu ni kuwa dada ni positive, na kaka ni negative, dada aliendelea kuugua kwa muda lakini alifariki baadaye...lakini yule kaka wakati wote wa alimuuguza mkewe kwa mapenzi makubwa..nilikuwa nikimuona wodini nilikuwa natamani kama ndoa zote zingekuwa na upendo vile, bahati mbaya mtoto ameambukizwa (kwa kuwa hawakujua na hawakufuata mpango wa kuzuia maambukizi kwa mtoto)...baba yupo, bado negative anamlea na kumuuguza mwanae. Mtoto ana miaka 8 sasa, anasoma.
kuhusu red shahidi ni Invisible hii thread imekaa jukwaa la jf dokta siku mbili hakuna cha ushauri wala nini na case yenyewe ni sensitive kama unavoiona hadi imeamishiwa huku mmu ndo umeonekana jamani maajabu!
back to topic siwezi kuongea sana ila nadhani ushauri nasaha unaitajika kwa hizi case kwa kweli
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom