Discordant Couple

Kwa hapo sijiwezi kabisa si la kisasa ama orijino

Mmmh, kwa kweli kama ni upendo wao si wa kawaida
Off course kumwacha haiwezekani
Ila mambo ya kikubwa siwezi, nitakuwa celibate happily than doing it
kumbe ndio maana ulianzisha huu uzi https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/359581-celibacy.html

Huu ndio ushauri wangu kwa huyo mama(Scientifically proved)

1/Mumewe aanze kunywa ARV baada ya kushauriana na Daktari, aanze kunywa at list miezi miwili kabla ya kukutana kimwili na mkewe.
(Hatari yake ni kwamba, hatatakiwa tena kuacha kunywa hizo dawa maisha yake yote!!)

2/Mwanamke anywe Hizo dawa za kupevusha mayai kama alivyoshauriwa na Daktari.
(Hatari yake ni kwamba kuna uwezekano wa kupata mapacha au watoto walioungana!!)

3/Mwanamke aanze kunywa dawa kinga(ARV Prophylaxis) masaa 6 kabla ya kukutana na mumewe na aendelee nazo mwezi nzima baada ya kukutana na mumewe
(Hatari yake zinachosha sana kimwili na Afya!!)

4/Mumewe afundishwe jinsi ya kufanya tendo kwa umahsusi, yaani ajichue tu nje ya uke na ikifika wakati wa ku-ejaculate ndio aingize ndani ya uke wa mwanamke na kumwaga manii kisha achomoe.
(Hatari yake mimba inaweza isishike!!)

*Kama huyo mama atafuata ushauri wote huu, atapunguza uwezekana wa kupata maambukizi kwa asilimia kubwa sana, lakini hatari ndogo ya maambukizi itabaki pale pale.

*Kumbuka hata kutumia Condom hakuzuii asilimia 100 kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi, yaani unaweza kutumia Condom na bado ukapata maambukizi.
acha hadithi mkuu. hapo ni IVF tuu au kuja kulaumiana baadae mke akiathirika. condom zinazuia kama utaepuka manjonjo mengi kunako 6x6
 
Umeanza.
Mungu anakulinda unapojilinda

Unakumbumba yule mtume alitaka kutembea kwenye Maji kama Yesu? Alizama japo alikuwa mtume, seuse sie tulio na imani ndogo kulicho mbegu ya shayiri?

huu utakuwa unyanyapaa sasa. Kwa nini amuache? Wanapendana wakijikubali na Mungu atawalinda
 
Mmebahatika kupata mtoto mmoja mzima. Leeni huyo mtoto,
risk ya kuambukizwa wewe na mtoto mwingine bado ipo. Don't take the chance, enjoy what you were blessed with.

0
Habari zenu wapendwa,

Naomba msaada, mimi na mme wangu ni discordant couple, tuligundua miaka 2 ya nyuma wakati mimi mjamzito na tulipoenda kupima ndio tukapata majibu hayo, tuna mtoto 1 na sasa hivi tumefikiria kupata mtoto wa 2, tangia tumegundua hilo tunatumia condom tu mpaka leo hii.

Tumeenda kwa daktari wa kina mama ametuambia tunaweza kupata mtoto wa pili kwa njia ya kujamiina ya kawaida lakini mimi amenipa dawa ambazo zitasaidiwa kupevusha mayai mengi kwa wakati mmoja ili uwezekano wa kupata ujauzito uwe mkubwa.

Jamani naombeni mawazo yenu kuna yeyote aliwahi kufanya hivo akafanikiwa na hakupata maambukizi? Na kitaalam hii ni njia sahihi? Au kuna yeyote anafaham njia nyingine tofauti na hii?

Doctors wa JF naomba mnipe maoni yenu
 
Niseme tu kwa kifupi hii sredi imenisisimua na kunifundisha mengi.

Namshukuru Dr. Riwa kwa shule aliyonipa leo.

Naomba Mungu anipe moyo wa kwenda kupima, nikikuta sijaathirika ndo imetoka hivyo, labda kama ugali nao utakuwa unaambukiza.

Mimi na Ugali hakuna wa kututenganisha
 
Last edited by a moderator:
Smile ulivyon'shupalia leo...nakoma!

Tusiende huko kwenye red tafadhali...katika uDaktari wangu nimeona discordant couples nyingi, lakini hizi experience mbili zilinitoa chozi:

- Couple ya kwanza walikuwa walokole wawili, walikuwa wanataka kuoana, hivyo wakaja pima afya zao. Nikawapa ushuria nasaha na wakawa tayari kupokea majibu...mdada akawa positive, na kaka negative. But kaka akasema atamuoa huyo dada, na watasali ataponywa au atalindwa hasipate maambukizi. Nikwaelekeza jinsi ya kujilinda but kaka akasema no need, sala zitawalinda. Nikasikitika. Nikawa nawafuatilia, wakaoana, wakawa wanakutana kimwili bila kinga, na baada ya miezi ^ kaka akawa positive. Alilia sana lakini ndio hivyo, sasa wako wanatumia dawa, wana mtoto mmoja hasiye na maambuki kwani dada alipopata ujauzito alifuata mpango wa kuzuia maambukizi kwa mtoto!

- Couple ya pili walikuwa wanandoa, mdada alijifungua, lakini akaumwa sana baada ya kujifungua, nilipowaona alikuwa na dalili za HIV, nikawapa ushauri nasaha wakakubali kupima, na majibu ni kuwa dada ni positive, na kaka ni negative, dada aliendelea kuugua kwa muda lakini alifariki baadaye...lakini yule kaka wakati wote wa alimuuguza mkewe kwa mapenzi makubwa..nilikuwa nikimuona wodini nilikuwa natamani kama ndoa zote zingekuwa na upendo vile, bahati mbaya mtoto ameambukizwa (kwa kuwa hawakujua na hawakufuata mpango wa kuzuia maambukizi kwa mtoto)...baba yupo, bado negative anamlea na kumuuguza mwanae. Mtoto ana miaka 8 sasa, anasoma.

Dah couple ya pili imeniuma sana... nimeumia moyo!!!
 
Invisible ipo siku nitakutukana unipe life ban hakyamungu unanitafutia ban
 
Last edited by a moderator:
Invisible ipo siku nitakutukana unipe life ban hakyamungu unanitafutia ban
 
Last edited by a moderator:
Smile kauliza: Ingekuwa positive ni mwanamke, mwanaume angekuwa naye? Jibu ni HAPANA. Mifano ipo mingi ila kwa sie akinanamama huwa tunavumilia hata kuacha kabisa. Kuhusu dada yangu kuachana na mumewe sahau ndivyo tulivyo, tukipenda ni mapenzi hasa ila wanaume!!! utamalizia Lara 1
 
Mifano miwili aliyotoa Riwa walioathirika ni wanawake lakini wanaume zao hawakuwaacha.

Hebu na wewe tupe ushahidi ulio nao kutetea hoja yako.
 
Last edited by a moderator:
Babu hao watakua wanaume wa zamani hawa wa sasa walionyeshwa maji ya betri.

Mifano miwili aliyotoa Riwa walioathirika ni wanawake lakini wanaume zao hawakuwaacha.

Hebu na wewe tupe ushahidi ulio nao kutetea hoja yako.
 
Discordant couple ndiyo nini?

Nyani, hata mie sikujua maana ya hiyo kitu. LAKINI nikasoma thread yote niilewe kabla sijauliza. Na nikapata jibu. Either we mvivu wa kusoma thread au unachangamsha jamvi. Just saying..teheheetehee!
 
Habari zenu wapendwa,

Naomba msaada, mimi na mme wangu ni discordant couple, tuligundua miaka 2 ya nyuma wakati mimi mjamzito na tulipoenda kupima ndio tukapata majibu hayo, tuna mtoto 1 na sasa hivi tumefikiria kupata mtoto wa 2, tangia tumegundua hilo tunatumia condom tu mpaka leo hii.

Tumeenda kwa daktari wa kina mama ametuambia tunaweza kupata mtoto wa pili kwa njia ya kujamiina ya kawaida lakini mimi amenipa dawa ambazo zitasaidiwa kupevusha mayai mengi kwa wakati mmoja ili uwezekano wa kupata ujauzito uwe mkubwa.

Jamani naombeni mawazo yenu kuna yeyote aliwahi kufanya hivo akafanikiwa na hakupata maambukizi? Na kitaalam hii ni njia sahihi? Au kuna yeyote anafaham njia nyingine tofauti na hii?

Doctors wa JF naomba mnipe maoni yenu

hiko kithungu hapo kimenizuia nisielewe na kuchangia mada,maana yake ndo nini?pliz
 
Niseme tu kwa kifupi hii sredi imenisisimua na kunifundisha mengi.

Namshukuru Dr. Riwa kwa shule aliyonipa leo.

Naomba Mungu anipe moyo wa kwenda kupima, nikikuta sijaathirika ndo imetoka hivyo, labda kama ugali nao utakuwa unaambukiza.

Mimi na Ugali hakuna wa kututenganisha

karibu ugali
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom