Dirisha la Maombi ya Samia Scholarship lafunguliwa

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,316
8,227
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefungua dirisha la maombi ya SAMIA SCHOLARSHIP kwa wanafunzi 640 waliopata ufaulu wa juu kwenye masomo ya sayansi katika mitihani ya Kidato cha Sita 2022. Majina ya wanafunzi hao yanapatikana kuanzia leo katika tovuti ya wizara www.moe.go.tz na ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu www.heslb.go.tz.

Aidha wanafunzi hao wataanza kuomba ufadhili huo kuanzia kesho Septemba 28, 2022 kupitia tovuti ya Bodi ya Mikopo ya Mikopo https://olas.heslb.go.tz kwa siku 14.

Akitoa tangazo hilo leo Septemba 27, 2022 jijini Dodoma Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema wanafunzi hao watafadhiliwa kwa asilimia mia moja kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mitano kulingana na programu husika walizodahiliwa.

Amefafanunua kwamba wanafunzi hao ni wa Tahasusi za sayansi ambazo PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN.

"SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa asilimia mia moja masomo ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba katika cyuo vikuu vya hapa nchini vinavyotambulika na Serikali ," amesema Prof.

Mkenda Ameendelea kusema kuwa, ufadhili huo utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kugharamia ada ya mafunzo, posho ya chakula na malazi, vitabu na viandikwa, mahitaji maalum ya vitivo, mafunzo kwa vitendo, utafiti, vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na bima ya Afya.

Prof. Mkenda ametaja masharti saba ya ufadhili huo ikiwemo kiwango cha ufaulu wa mnufaika kisiwe chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo na chini ya hapo ufadhili utasitishwa. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgullam Hussein amepongeza hatua ya Serikali kutoa ufadhili huo ambapo kwa upande wa Zanzibar ufadhili wa aina hiyo pia umetolewa kwa wanafunzi 30 hivyo kuongeza fursa kwa watoto wa Kitanzania kupata elimu ya juu.

1664277399524.jpeg

Source: Chief Government Spokesperson / Msemaji Mkuu wa Serikali on LinkedIn: Dirisha la Maombi ya Samia Scholarship Lafunguliwa Na Mwandishi…
 
View attachment 2369695
Source: Chief Government Spokesperson / Msemaji Mkuu wa Serikali on LinkedIn: Dirisha la Maombi ya Samia Scholarship Lafunguliwa Na Mwandishi…
Hongera sana mama kwa kuendelea kuzalisha wasomi wengi nchini maana kupitia scholarship hii itawapa wanafunzi chachu ya kusoma zaidi
 
Bora tu uombe zako mkopo wa HESLB usome kwa kurelax,ukipiga first class ni poa tu.
Unaweza omba hio hela ya Samia,bahati mbaya ukapiga 3.5,jamaa wakaanza kukuambia eti,huruhusiwi kuomba tena
 
Hata atoe nini 2025 lazima ajambe cheche! Hakuwekwa pale magogoni kuwa li picha tu la kuongozwa kwa remote! Hoves kabisa!!
 
Hawa jamaa bwana ukisoma viandishi vyao utasema wana vyama imara kumbe hamna lolote.hebu imarisheni kwanza demokrasia ktk vyama vyenu ambavyo viongozi wenu ni kama marehemu Eliza wa UK.
Hata mpango hauna uhusiano wote na 2025 SSH ni kiongozi mkuu wa nchi na kila kiongozi ana maono yake.
Wengine maono yao ni kubadili katiba za vyama vyao ili wawe viongozi wa Kisumu.
Kupanga ni kuchagua
 
Back
Top Bottom