Dick Sound: Milionea aliyeanza kuuza maji, kufunga muziki Magomeni

Nimevutiwa na utajiri mkubwa huyu kijana mwenye miaka 31.

Amekuwa akiuza maji kabla ya kujiajiri kwa kazi be ya kufunga mziki magari na kuyapimpu.Kazi hii kafanya kwa miaka zaidi ya ishirini.

Ana miliki nyumba yenye thamani ya zaidi ya milioni 350 TSH, pamoja na magari ya kifahari ya thamani ya zaidi milioni 850.

Hakika kijana huyu ni kielelezo cha vijana wenye mafanikio makubwa kwa kujiajiri wenyewe bila ya kutegemea ajira ya serikalini, mafanikio ya kijana huyu ni zaidi ya wasomi walioajiriwa wakisubiri mshahara kiduchu kwa mwezi.

Hongera yake.
Amefanya hiyo kazi Kwa miaka zaidi ya 20 na yeye ana miaka 31🤔
 
Wapo walioanza kabla yake mbona hawajatoboa
Na hawatokaa watobowe ng'oo, hapa mjini si kila ofisi unayoiona ndio source of income ya muhusika.

Hizo ofisi ni cover tu, watu wana mambo yao mengine.

Hii dunia ina siri kubwa, utashangaa siku ukimkuta mchungaji yupo kwa mganga wa kienyeji kunyoosha mambo yake, kesho kanisani anakemea wachawi na mapepo hii ndio dunia ilivyo.
 
Watu hawataki kukubali jamaa ashatusua "
Mleta mada hii ndio hali halisi ya watanzania,,, ukiwa nacho unapondwa usipokuwa nacho pia unapondwa ....
Ana miaka 31, kafanya Kazi zaidi ya miaka 20.
Hebu Elezea hili tafadhali ....

#YNWA
 
Usisahau pia Magomeni ndio makao makuu ya wauzaji na wasafirishaji wa dawa za kulevya Tanzania.

Nia ya muanzisha uzi ilikuwa useme kama ulivyoandika !!! Haamini kuwa bila Kuwa punda huwezi kutoboa!
 
Huyo sasa ndy mwamba alikuwa anafunga miziki

Hawa wa sahv wote mbwembwe tu

Nikas yupo sema ka lay low anapiga mishe zingine mdg mdg

Ova
Alinifungia muziki mwaka 2008 kile kinu husikii nje kabisa Ila nikifungua mlango au mtu akiingia ndani ya gari ndio alikuwa anaelewa Watts zilizomo mle ndani.

Jamaa bonge la sound technician Yuko Safi sana, naona ameona hiyo biashara wamevamia madogo na bidhaa za kichina haimlipi.

Zamani Kama hauna kuanzia milioni na nusu hupati kinu Cha ukweli, .sasa imagine 1.5 ya 2008 kwa sasa ni bei gani maana by that time hata Dola moja ilikuwa 980.
 
Alinifungia muziki mwaka 2008 kile mini husikii nje kabisa Ila nikifungua mlango au mtu akiingia ndani ya gari ndio alikuwa anaelewa Watts zilizomo mle ndani.

Jamaa bonge la sound technician Yuko Safi sana, naona ameona hiyo biashara wamevamia madogo na bidhaa za kichina haimlipi.

Zamani Kama hauna kuanzia milioni na nusu hupati kinu Cha ukweli, .sasa imagine 1.5 ya 2008 kwa sasa ni bei gani maana by that time hata Dola moja ilikuwa 980.
Nikas alikuwa anajuwa

Ova
 
Back
Top Bottom