ushua kaujua ukubwani ndio shida, kuna watu wamekulia masaki oyster bay huko tangu watoto na wala hawaoni kama wanatofauti na watu wa manzese, yeye mpaka wema anamuita wa ushuani wakati kakulia sinza eti wema si type ya kajala kwa kigezo cha shule alosoma wema, mi naona hata hiyo 0.5 umempendelea, au labda ni point ya kuhudhuria chuo lakini si kuelimika.
Sasa huyo Wema kasoma shule gani ya kumshtua mtu?
Umeshaona hata anavyoandika?
Eniwei, kumuongelea Wema kuhusu elimu yake ni kumuonea maana sijawahi kuona popote pale akijigamba kuhusu usomi.
Tubaki na huyu juha. Soma tu anayoyaandika. Angalia misamiati yake, angalia uchaguzi wake wa maneno, matumizi yake ya vivumishi, vielezi, vitenzi, na kadhalika.
Angalia makosa yake ya kitahajia. Na hapo wala sijagusia kabisa ukosefu wa mantiki katika hizo 'hoja' zake.
Hivi kweli, kwa kumsoma tu kupitia maandiko yake, unaweza kupata picha kuwa naye ni msomi?
Kwamba anaweza kukaa meza moja na wasomi?
Sasa labda mimi natumia vigezo ambavyo sivyo kwa mtu ambaye siye.
Mbele ya akina Linda na Mbuta Nanga anaweza akawa msomi kweli.
Lakini tukimpitisha kwenye tanuru la wasomi hawezi kabisa kusalimika.
Na hivi hizo shahada zake kazichukulia kwenye vyuo gani?