hannibali
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 468
- 428
Habarini za muda huu waungwana.
Majuzi kati kuna msiba ulitokea kuna jamaa mmoja alifariki lakini yeye alikuwa anaishi nchi za Scandinavia, umauti ulimkuta hukohuko lakini mwili wake ulisafirishwa kuja kuzikiwa huku, kitu kilichonishangaza ni kuona kuna baadhi ya watu walikuwa wanaonesha kufurahia kwa msiba huo kutokana na baadhi ya watu nilivyokuwa nikiwasikia wakizungumza.
Nanukuu mmoja nilimsikia akisema: "Unaona sasa hata ukijifanya kukimbia ulikotoka mwisho wa siku utafukiwa tu hukuhuku, kiko wapi sasa si huyu karudi"
Kwakweli nilistaajabu sana. Kuna mwingine pia alikuwa anasema: "Wanaenda huko mwisho wa siku hamna lolote wakifa kazi kuchangiwa nauli, si bora wabaki makwao tu"
Ama kweli ni maneno ambayo yalionesha waziwazi si mazuri hasa ukizingatia kwa mtu ambaye amekwishakata roho, ilipaswa aombewe anakokwenda apokelewe vizuri na muumba.
Sijajua tatizo ni nini kwa watu wa jamii ya huku (Bongo) ni kwamba hawawapendi diaspora au hawataki vijana watoke nje kuangalia fursa za maisha..ni nini kibaya kafanya yule kijana mpaka wamuongelee maneno ya namna ile.