Diaspora amekufa wengine wanachekelea, kwanini?

Diaspora amekufa wengine wanachekelea, kwanini?

Acha wasemwe.... ni nani asiyesemwa ....watu wanamsema Mwenyezi Mungu sembuse maiti?


Ila tukiacha utani tu na kujua jua kwingi.

Ni aibu.... umeishi nje kila mwaka unasafiri unakuja nyumbani na mbwembwe kibao unafikia Lodge halafu msiba unachangiwa na marafiki na wanarudisha kabegi tu na Iphone 11.

Tuache mengine hata watoto utawaachia aibu [emoji23][emoji23][emoji23]


Kikwetu....kuna msemo tunasema hizi ndizo zile aibu walizokuwa wanajinyongea babu zetu. Watu wa zamani walikuwa na aibu bwana....
 
So wanajiweza wajiweke chama cha kufa na kuzikana kama wasambaa
 
Tunarudi pale pale, wenye pesa, elimu nzuri na maisha mazuri huwa wana handle stress tofauti na masikini. Unaweza kwenda mapumziko, kubadili muonekano wa nyumba nk.
Watu wa hali ya chini huku uswazi kwetu hua hawanaga stress. Stress ziko Masaki, Mbezi Beach na huko Ununio. Sisi huku tembele, vibua, dagaa tukitoka nje Ni mnanda, mchiriku na taarabu za mafumbo.
Wazaramo hatunaga presha Wala stress.
 
Acha wasemwe.... ni nani asiyesemwa ....watu wanamsema Mwenyezi Mungu sembuse maiti?


Ila tukiacha utani tu na kujua jua kwingi.

Ni aibu.... umeishi nje kila mwaka unasafiri unakuja nyumbani na mbwembwe kibao unafikia Lodge halafu msiba unachangiwa na marafiki na wanarudisha kabegi tu na Iphone 11.

Tuache mengine hata watoto utawaachia aibu [emoji23][emoji23][emoji23]


Kikwetu....kuna msemo tunasema hizi ndizo zile aibu walizokuwa wanajinyongea babu zetu. Watu wa zamani walikuwa na aibu bwana....
Maisha ni mapambano Kuna kupata na kukosa na pia huwezi kumlazimisha MTU ajenge TZ,acheni chuki za kishamba bongo hata mtu akiongea kingereza mnamwona anaringa
 
Maisha ni mapambano Kuna kupata na kukosa na pia huwezi kumlazimisha MTU ajenge TZ,acheni chuki za kishamba bongo hata mtu akiongea kingereza mnamwona anaringa
Mkuu hizi sio chuki ni sheria zisizo rasmi za maisha tu.

Sasa wewe rafiki yangu tumesoma wote. Ukabahatika ukaenda Bulaya.

Unajua fika kwetu umasaini ni kimasai na kiswahili cha kuibia...unakuja kunisalimia unaongea yes no yes no nyingi....huko si kujibrag mkuu?
 
Sio amekufa, mstahi basi kidogo... sema amefariki au roho imeacha mwili!
 
Mimi siwezi kucheka msiba lakini siwapendi maana kuna diaspora mmoja alikuja kutoka marekani na vingereza viingi hadi kanibebea sikudhani wangu
Kwa nini unawachukia wote wakati ni mmoja tu aliyekuhusu.
 
Watu wana uhuru wa kuzungumza maana baadhi ya diaspora wakienda majuu hawakumbuka kutengeneza maisha nyumbani.
 
Masikini hutamani watu wote wawe masikini kama wao

Huyo marehemu hata kama angezikwa huko alipofia pia wangesema,wangesema "Unaona amezikwa nchi za watu,amekosa hata hela yakuja kuzikiwa

Nyumbani" Binadamu hawakosi maneno hata ufanyaje huwezi kuwaridhisha,muhimu mtu ni kupambana kivyako tu na kuziba masikio kwa hawa masikini waliokwisha jikatia tamaa nakuamua kujiajiri kwenye wizara ya chuki na masimango.
 
Masikini hutamani watu wote wawe masikini kama wao,
Huyo marehemu hata kama angezikwa huko alipofia pia wangesema,wangesema "Unaona amezikwa nchi za watu,amekosa hata hela yakuja kuzikiwa Nyumbani" Binadamu hawakosi maneno hata ufanyaje huwezi kuwaridhisha,muhimu mtu ni kupambana kivyako tu na kuziba masikio kwa hawa masikini waliokwisha jikatia tamaa nakuamua kujiajiri kwenye wizara ya chuki na masimango.
Wapo wizarani[emoji38]
 
Habarini za muda huu waungwana

Majuzi kati kuna msiba ulitokea kuna jamaa mmoja alifariki lakini yeye alikuwa anaishi nchi za Scandinavia, umauti ulimkuta hukohuko lakini mwili wake ulisafirishwa kuja kuzikiwa huku, kitu kilichonishangaza ni kuona kuna baadhi ya watu walikuwa wanaonesha kufurahia kwa msiba huo kutokana na baadhi ya watu nilivyokuwa nikiwasikia wakizungumza.

Nanukuu mmoja nilimsikia akisema "" unaona sasa hata ukijifanya kukimbia ulikotoka mwisho wa siku utafukiwa tu hukuhuku, kiko wapi sasa si huyu karudi"" kwakweli nilistaajabu sana. Kuna mwingine pia alikuwa anasema "" wanaenda huko mwisho wa siku hamna lolote wakifa kazi kuchangiwa nauli si bora wabaki makwao tu""

Ama kweli ni maneno ambayo yalionesha waziwazi si mazuri hasa ukizingatia kwa mtu ambaye amekwishakata roho, ilipaswa aombewe anakokwenda apokelewe vizuri na muumba.

Sijajua tatizo ni nini kwa watu wa jamii ya huku ( bongo) ni kwamba hawawapendi diaspora au hawataki vijana watoke nje kuangalia fursa za maisha..ni nini kibaya kafanya yule kijana mpaka wamuongelee maneno ya namna ile.
Wala shida siyo kuwa Diaspora.

Wabongo ndivyo tulivyo.

Sijui unashangaa labda huko kwenu ni tofauti.

Huku kwetu ni kawaida kufurahia matatizo ya watu.

Mtu akipata majanga kazini tunafurahiiii.

Akifukuzwa ni Sherehe kuubwa.

Hata sisi "Wazarendo" wa Magufuli tunafurahia sana mtu akitumbuliwaaaa.

Hata vijiweni kwetu tunafurahia stori ni za watu waliotumbuliwa. Utasikia yule jamaa enzi za Jakaya alikuwa vizuri, kwasasa kafukuzwa kazi ana hali mbayaaaaaaa, hahahaha huhuhuhu hahahaha 🤣🤣

Mibongo ndivyo tulivyo
 
Diaspora nao wana nyondo sana na wanasahau sisi walio tuacha huku manyovu kigoma ndo wachimba makaburi wao
Aliyewasahau nyie ni Zitto Kabwe, alikuwa anawavuruga akili tu huku akiwapa ahadi nyingi tu za kijinga.
 
Inategemea na nini
MTU, SABABU, MAJIRA

Namaanisha inategemea na

1. Aina ya mtu aliyekufa (mwizi, mlevi, shekhe, paroko, changudoa, jambazi

2. Sababu ya kifo chake (sumu, kipigo, ajali, mshtuko nk)

3. Majira/kipindi kifo kilipotokea (hali ngumu, msimu wa hela, taharuki, ukata, mlipuko wa maradhi fulani
 
Sio kila diaspora ana good life unless labda awe ana professional career huko abroad. Otherwise unakuta tu mtu ameamua kubadili mazingira ya ku hustle huko anafanya kazi za kawaida zenye kipato chakuweza kujikimu yeye na familia yake kama waliopo hapa bongo tu.

Tatizo tumekariri kuwa ukisikia mtu anaishi mamtoni basi ni milionea fulani au ana good life sana labda anaringa na presumption nyingine kibao.

Kikubwa tuache wivu na kupenda kuchukia maendeleo ya wengine. Kisa mtu katoka kaishi nje ya nchi watu wanakuwa na wivu kiasi cha kufurahia kifo cha mwenzao?
Niliishi Mkoa wa Mbeya kama miaka mitano hivi, Wilaya ya Rungwe. Kwa kweli issue kama hii kule ni kama ugonjwa hivi. Wastaafu wanaoamua kurudi kwao wanasemwa sana mpaka wanazeeka kabla ya wakati wao. Inasikitisha kwa kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom