Diamond Platnumz interview with Sports Arena (Exclusive)

Murano

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
2,059
2,000
Wakati jamaa anapata mashavu ya show kubwa kubwa duniani huku King K anagombana na maprodyuza kwa kutengeneza ngoma bure kisha anawakimbia Dunia hii jamani.
 
yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,129
2,000
haters ndo wanampaisha sana huyu jamaa na wakijua wakakaa kimya itamfanya abweteke
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,602
2,000
Msanii nguli wa kimataifa diamond platnumz a.k.a baba lao and CEO wa WASAFI MEDIA akihojiwa na sports arena baada ya kurudi kutoka misri kwenye tuzo za CAF mahojiano Kama ifuatavyo

Mtangazaji: kwanii una connection nyingi za kufanya show kubwa

Diamond:Africa Kuna wasanii wengi Sana na niwazuri lakini asilimia kubwa sio performer ndo maana nipata nafasi nyingi Kama hii hii inakuwa kwangu Mara yangu ya pili kufanya show kwenye tuzo za soka CAF.

Mtangazaji: baadhi ya watu wanasema unajiwakilisha wewe

Diamond: nikiwa na tambulishwa watanitaja jina langu lakini pia na jina la nchi yangu ukienda baadhi ya nchi za nje utaheshimika cos umetoka kwenye nchi yenye diamond.

Mtangazaji: unampango wowote wa kuwa na team yako ya mpira

Diamond: huo mpango nilikuwa ninao muda mrefu lakini focus yangu kwanza ni kujenga kituo Cha kukuza vipaji ambapo muda si mrefu tutaumaliza kwasababu process yake ni kubwa na ili wazo nilipewa na e'too.

Kuna wataalamu wa soka teyali tumeshawapa kwaajili ya kuendesha kituo hiko lakini pia lazima tuwe na facilities nzuri baada ya kumaliza hili ndo nitaamua kununua team ambayo teyali ipo ligi kuu na tutabadilisha jina lake litaitwa WASAFI football club sitaki nianze from scratch kabisa.

Mtangazaji: sasa hiv wasafi fm inasikika maeneo machache una mpango gani kufikia mikoa mingi

Diamond: wakati nimeifungua Wasafi fm nilitaka isikike maeneo machache na tuahakikishe tumeteka kwelikweli ili tutapoanza kutambulisha mikoani tutuwe kwa kishindo sio kinyonge na sema kweli teyali wasafi imefanya vizuri Sana na tumefanikiwa lengo letu kuanzia j'3 ya wiki moja ijayo tutaanza kutambulisha mikoa itayoanza WASAFI FM kusikika na hatutaki iwe kiholela watu hawajanizoea hivyo so tutambulisha kwa namna tofauti na kwa ukubwa.

Tumeichagua siku hiyo ya j'3 cos ni siku ambayo nitakuwa free baada ya hapo nitakuwa busy cos nitakuwa ninashow Nigeria kwenye tuzo za SOUNDCITY baada ya happy nitakuwa na show ufaransa na visiwa vya Madagascar, Mayotte then ninashowa Los Angeles Marekani baada ya hapo Nina European tour ambayo nitafanya kwwnye miji mingi.
Wewe nae andika vizuri Kiswahili. "teyali" ndiyo nini? Halafu umezijaza hizo "teyali". Pambaf.
 
myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,623
2,000
Eti "WASAFI football club ''😁😁😁😁😁😁

Mungu amsaidie
Hapana aisee, sema tu anaweza asiwe serious sana kwa sababu kimsingi Mond sio mpenzi wa soka but trust me, kwa influence aliyo nayo jamaa, kama anakuwa na timu fasta tu inakuwa na rundo la mashabiki nyuma ya Yanga na Simba! Hata ukiangalia ile Wasafi Media, ime-takeoff haraka sana kwa sababu ya influence yako. Kwa sababu jamaa tumchukie au tumpende, ukweli kwamba ana loyay fans ni ukweli usiopingika! Halafu tena yule jamaa anaweza kuwa na mashabiki wengi wa kuishangilia Wasafi FC pengine kuliko hao Simba na Yanga! HOW?! Siku ya Wasafi FC vs Yanga, mashabiki wa Wasafi walio Simba wanakuwa upande wao, and vice versa! Siku ya Wasafi vs Azam (kwa mfano), Fans wa Wasafi walio Simba na Yanga wanahamia Wasafi!!

Ndo vile tu kuna watu jamaa hawataki kumkubali lakini mara nyingi huwa anawa-prove watu wrong!!! Bado sijasahau mjadala Mond kuanzisha Tv hapa hapa JF miaka 4-5 iliyopita! Wengi wakawa wanakejeli kwamba labda aanzishe online tv!!
 
devijoy

JF-Expert Member
Oct 25, 2018
802
1,000
Mashabiki wengi kuliko Yanga au Simba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom