Diamond Platnumz: 2025 tunaenda nawewe Rais Samia

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Msanii Naseeb Abdul almaarufu Diamond Platinumz, amemtakia heri ya siku ya mfanano wa kuzaliwa Rais Samia Suluhu, na pia amemuahidi kuwa 2025 yeye na wanaom-support watampigia kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais.

Ameandika Diamond Platnumz kwenye ukurasa wake wa Instagram,

"Kupata Rais ni Jambo Moja ila Kupata Rais Mwenye Busara, anaethamini Utu, na kujua kuwa anaowaongoza ni Binadam Wenzie hivyo kuna Muda inafaa awavumilie hilo ni jambo lingine… Rais ambae licha ya Mamlaka makubwa alionayo lakini anaamua Kutanguliza Hekima na Ubinadamu Mbele ni jambo la Kumshukuru Mwenyez Mungu…. Ni Mengi Umeyafanya na unaendelea kuyafanya Kuanzia Kwenye Nchi kama Nchi, Taasisi, Makampuni, Vyama pinzani, kusaidia hadi Vikundi na kwa mtu mmojammoja, ila kwa Hekima yako wewe sio mtu wa Kujikweza ama kudharirisha watu kuwa fulani nimemfanyia hili na lile, Amini kwamba Tunakushukuru sana….Tanzania ni nchi ambayo Mpaka Kiongozi anapomaliza Muda wake ndio Anasifiwa, hivyo usije kukatishwa tamaa na Maneno ya Watu wachache ambao pengine wanaogopa kukusifia sasaivi labda wataonekana Wanajipendekeza au Pengine itawafanya wapoteze riziki zao kwa kuonekana sio Wapinzani tena.. Nikuahidi kwamba 2025 Tunaenda na wewe na si Mwingine! Nikutakie Heri ya Siku ya Zuliwa na InshaAllah Mwenyez Mungu aendelee Kukulinda, kukupa Maisha Marefu, Yenye Afya na Amani na kika lenye Kheri🙏🏼 Samia Suluhu Hassan"

Nini maoni yako?

Written by Mjanja M1
 
Back
Top Bottom