Diamond Platnumz akiri kuwa anapenda sana nyoka

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245

Bosi wa WCB Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz amejipatia mnyama aina ya nyoka wa kuweka nyumbani.
Katika tangazo lake kwenye Instagram, mwanamuziki huyo alibainisha kuwa siku zote kumiliki nyoka kipenzi imekuwa ndoto yake.
Staa huyo wa Bongo mwenye umri wa miaka 32 alimtambulisha nyoka huyo wake kama rafiki yake mpya.

"Siku zote nimekuwa na shauku ya kuwa na nyoka wangu kama kipenzi ❤️🐍.. jameni tukutaneni na rafiki yangu mpya," alitangaza siku ya Ijumaa.

Aliambatanisha ujumbe huo na video yake akicheza na mnyama huyo anayeteleza huku kundi kubwa la watu wakiwa wamemzunguka.
Katika video hiyo, Diamond alisikika akikiri upendo wake mkubwa kwa nyoka na kueleza furaha yake kwa kumpata wa kufuga nyumbani

"Huyu mimi namfuga mnyama huyu nyumbani. Mimi napenda nyoka sana," alisika akisema.
Umati ulitazama kwa udadisi alipokuwa akichezea na nyoka huyo kwa usaidizi wa mwanamke aliyekuwa akimuonyesha jinsi ya kumshika. Hakuonesha uoga wowote na badala yake alionekana kufurahi sana kumshika.

Mwimbaji huyo anayetambuliwa kote duniani alifichua kwamba nyoka huyo wake atatambuliwa kwa jina Chichi.
Katika hali ya kawaida nyoka sio wanyama wa kupendwa miongoni mwa watu wengi. Wengi wa wanyama hao wana sumu ambayo inaweza kusababisha kifo au ugonjwa mbaya mara tu wanapomng'ata mtu.

Baadhi ya jamii za Kiafrika huhusisha mnyama huyo na uchawi na hivyo kamwe hawawataki karibu nao. Wale wanaofuga wanyama hao mara nyingi huchukuliwa kuwa wanashiriki katika uchawi.
 
Attachments

  • unnamed (1).jpg
    unnamed (1).jpg
    38.5 KB · Views: 21

Huyo ajakutana na nyoka bado hicho kisebengo mbona kitakata chenyewe.
 
Nyoka ni viumbe wasio zuru mtu bila sababu...ndio maana anweza kukaa kwako akiwa mdogo hadi akawa lijoka kabisa na asikudhuru. Ila mwanada akimuona yeye atataka amuue huyo nyoka! Tu waajabu ndio maana kwenye Ecosystem tunatajwa kwamba tu viumbe namba mona waharibifu wa mazingira na Ecosystem....Btw watu watamwambia ni mshirikina.
 
I love snakes
Ndoto yangu kuwa na sehemu ya kufuga wa kila aina isipokuwa mmoja tu
Huyu hata adui yangu siwezi kumuombea akutane nae ni Black Mamba aka koboko,
Huyu ni shetani na nusu
Ukimuona binadamu mchokozi na anatukana watu bila kosa halafu mgomvi basi huyo hana tofauti na Koboko

Napenda nyoka hasa wale wakubwa sana na wale wasio kuwa na sumu
Screenshot_20230122_165747_Google.jpg
a4083f29867b661d9b2399306b361361.jpg
snakes-are-beautiful-at-least-when-theyre-in-pictures.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_20230122_165747_Google.jpg
    Screenshot_20230122_165747_Google.jpg
    64.3 KB · Views: 17
Nyoka ni viumbe wasio zuru mtu bila sababu...ndio maana anweza kukaa kwako akiwa mdogo hadi akawa lijoka kabisa na asikudhuru. Ila mwanada akimuona yeye atataka amuue huyo nyoka! Tu waajabu ndio maana kwenye Ecosystem tunatajwa kwamba tu viumbe namba mona waharibifu wa mazingira na Ecosystem....Btw watu watamwambia ni mshirikina.
Bro hujakutana na koboko aka black mamba!
Ni nyoka mwenye visasi balaa
 
Back
Top Bottom