Diamond Platnamz arushiwa "mayai viza" stejini, KISA?

Diamond Platnamz arushiwa "mayai viza" stejini, KISA?

matumbo

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
7,224
Reaction score
3,960
[h=3]SHOW YA DIAMOND YAGEUZWA UWANJA WA NGUMI NA MATUSI.....[/h]

​


​

Diamond platinum amefungua mwaka vibaya baada ya show yake ya jana pale Maisha Club kumwendea ndivyo sivyo. Usiku wa Wasafi haukwenda kama ulivyokua umepangwa baada ya kutokea fujo kubwa.


Show hiyo ilianza saa saba na nusu na baada ya dakika chache za Diamond kwenye stage fujo zilianza baada ya kundi kubwa la vijana wasiojulikana kuanza kutukana watu, kurusha chupa na viti, kupigana na kupora vitu vya thamani kutoka kwa mashabiki wa Diamond.

Chupa zilipoanza kurushwa kwenye stage ,moja ilimpata Diamond mkononi na nyingine ilimjeruhi mpiga picha wake Bestizo Mkononi. Kuona hivyo Diamond alishuka kwenye stage na kwenda kwenye chumba cha mapumziko mpaka fujo zilipotulizwa.




​
Vitu vya thamani kama cheni,pete na camera ya Bestizo ya ThisisDiamond iliporwa kwenye fujo hizo. Inasemekana Diamond na uongozi wa maisha ulipata taarifa kuhusu uwezekano wa fujo hizi kutokea na hatua zilifanyika kuweka usalama zaidi ila vijana hawa walikuwa wengi na ndio sababu ya show ya Diamond kuharibika.
 
[h=3]DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU FUJO ZILIZOTOKEA WAKATI WA SHOW YAKE PAMOJA NA HASARA ILIYOPATIKANA[/h]

​
​


Usiku wa january 1 2013 Maisha Club ulikua usiku maalum kwa show ya WASAFI ambao wanaongozwa na Diamond Platnums, usiku huu umeingia kwenye Headlines baada ya fujo kubwa kutokea za kurushwa chupa, viti na mayai viza.

Noma ilianza dakika 15 baada ya Diamond kuanza kuingia kwenye stage ambapo anakiri kwamba alijua kulikua kuna watu wamepanga kuja kumfanyia fujo na aliuambia uongozi wa Maisha Club mapema kwa tahadhari na wakamwambia aendelee manake wameshaongea na wahusika lakini kumbe maongezi hayakubadilisha chochote.

Anavyosema Diamond ni kwamba waliofanya fujo ni washkaji zake wa siku nyingi ambao alikua nae Kariakoo, hao washkaji walikua wamegombana hivyo kugawanyika katika makundi mawili ambapo kundi moja lilikua linataka Diamond awe nalo alafu jingine alitenge, anasema yeye alikataa hilo wazo kwa sababu wote ni washkaji zake.

Huo msimamo ulifanya hilo kundi lililomshawishi kukasirika na kuamua kulipiza kisasi kwa kufanya fujo Maisha Club, taarifa alizipata mapema kwamba wangekuja kumzomea ambapo kweli hao jamaa walipofika Maisha wakati wa show walianza kuzomea lakini Diamond akatangaza kwa mashabiki ambao walimsupport Diamond na kupiga kelele zilizowashinda hao wazomeaji ambao baada ya kuona hivyo walianza kufanya fujo.

Mmoja wa hao wazomeaji ambae aliongea na millardayousiku huo huo kwenye eneo la tukio alisema wao hawahusiki na fujo zilizotokea, waliofanya fujo ni mashabiki tu ambao pengine walichoshwa na show ya Diamond, wao walichokuja kufanya ilikua ni kuzomea tu kwa sababu Diamond alikiuka makubaliano yao.

Makubaliano yenyewe ni kwamba kwa sababu Diamond ni mshkaji wao toka kitambo kabla hajajulikana kisanii, walishakubaliana toka wakati huo kwamba akifanikiwa kimuziki inabidi asaidie na washkaji wengine wa kundi hilo ambao ni wasanii wachanga kitu ambacho jamaa wanadai Diamond hajakifanya kabisa, siku ya tukio alitakiwa kuperform na msanii mmoja wapo aitwae Papaa Masai lakini Diamond alikataa na hicho ndicho kilichowapa hasira.

Baada ya mambo kuharibika hili kundi pia limedai kwamba kuna wakati Diamond alikua anawatuma kwenda kumzomea Bob Juniour kwenye show zake na pia alikua anawatumia kwenye show zake kwenda kumshangilia.

Diamond amesema wote waliomfanyia fujo anawajua mpaka kwa majina na tayari ameshawashitaki polisi na atahakikisha wakienda kukamatwa wanakamatwa kukiwa kuna kamera inawarekodi ili waonekane.

Kitu kingine alichokisema ni kwamba kati ya hao waliokwenda kumfanyia fujo ni pamoja na mdogo wa msanii ambae aliwahi kuwa na ugomvi nae wakapatana (huyo msanii) lakini bado huyo msanii amekua na chuki dhidi yake.

Yani Diamond aliwahi kuwa na beef na huyo msanii wakayamaliza lakini bado jamaa ana chuki, hawezi kumtaja kwa sasa na anachofanya ni kuacha uchunguzi wa polisi ufanyike kwanza, ikigundulika ni kweli atamtaja hadharani.

Kuhusu huyo msanii namkariri zaidi Diamond akisema "Uhusiano wangu na huyu msanii hauko vizuri, tulishahitilafiana kama mwaka umepita tukapatana lakini bado ana chuki dhidi yangu, tatizo niliona liliisha lakini nikaona mwenzangu kama bado ananionyesha chuki hata nikikutana nae najifanya kama hakuna tatizo lakini moyoni najua mwenzangu kuna vitu ana viendeleza vya chinichini ambavyo sivielewi"

Diamond amesema hasara ya vitu vyake kwenye hizo fujo ina thamani ya milioni zaidi ya 13 kutokana na kuibiwa simu yake ya iPhone5, cheni pamoja na camera ya video ya thamani kubwa ambayo aliinunua kwa ajili ya website yake.

 
Milioni 13??? Anataka aponee hapo hapo
 
aaaaaaaah ana2ma wa2 wakamzomee mwnzie na kushangliwa yy k sasa yamemrud kwake
 
juzi kati hapa Ndugu zangu Matola na Kiranga walisakamwa sana hapa na wafuasi wa Diamond...
ikafika hatua Diamond akafananishwa na Mbaraka Mwinshehe.

Kiko wapi sasa?
 
:becky::madgrin: mayai viza hilo neneo sijalikia miaka dah aisee uswazi kutamu sana hahahaa watu wana akili za kizamani mno karne hii
 
Poleh yake ila siamini kwamba iPhone 5 na camera na cheni inafika 13M au ni kujipaisha?
 
juzi kati hapa Ndugu zangu Matola na Kiranga walisakamwa sana hapa na wafuasi wa Diamond...
ikafika hatua Diamond akafananishwa na Mbaraka Mwinshehe.

Kiko wapi sasa?

Huyu Diamond ndio nani? ni mbunge or?!
 
juzi kati hapa Ndugu zangu Matola na Kiranga walisakamwa sana hapa na wafuasi wa Diamond...
ikafika hatua Diamond akafananishwa na Mbaraka Mwinshehe.

Kiko wapi sasa?

Hehe, usikute na wewe ulikuwepo kuzomea?
 
wagombanao ndio wapatanao si awapoze kidogo tu washkaji sbb hasara yake ni kubwa zaidi
 
hahahahha!umjui diamond platnamz...wabongo bwana ndio maana tunamaendeleo sana.

matumbo, Hebu nielimishe mi simfahamu ki ukweli,nilidhani ni yule wa Kenya ambaye tulisoma nae Engineering kule Nairobi miaka mingi ilopita ila nimefatilia yeye sasa yupo Nigeria ktk Visima vya mafuta,nauliza seriously,"Huyu Dimond ni nani?" au ni yule Engineer karudi?
 
Last edited by a moderator:
matumbo, Hebu nielimishe mi simfahamu ki ukweli,nilidhani ni yule wa Kenya ambaye tulisoma nae Engineering kule Nairobi miaka mingi ilopita ila nimefatilia yeye sasa yupo Nigeria ktk Visima vya mafuta,nauliza seriously,"Huyu Dimond ni nani?" au ni yule Engineer karudi?

kamuulize demu wako anamjua..au kasikilize ringtone kwa simu ya sista ako utamtambua vizuri..maana ata uki-act haumjui bado haisaidii kitu.
 
Last edited by a moderator:
kamuulize demu wako
anamjua..au kasikilize ringtone kwa simu ya sista ako utamtambua
vizuri..maana ata uki-act haumjui bado haisaidii kitu.

matumbo,mkuu mbona umetumia lugha kali sana? hivi kweli wewe ni Great Thinker kweli? nina doubt kuhusu uwezo wako wa kifikira! pole nikiwa nimekukwaza,lakini mi "SIMJUI DIAMOND"
 
Last edited by a moderator:
matumbo,mkuu mbona umetumia lugha kali sana? hivi kweli wewe ni Great Thinker kweli? nina doubt kuhusu uwezo wako wa kifikira! pole nikiwa nimekukwaza,lakini mi "SIMJUI DIAMOND"

hahahaha!unatamani ungekuwa umjui kweli,lakini ndio ivo tena..msubirie siku akishuka ufanye tafrija mkuu,maana mafanikio yake kwako yamekuwa kero unajuta ata kwa nini unamjua.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom