Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

Kwa hiyo kama jirani yako shoga/msagaji basi na wewe unataka kuwa hivyo kwa vile jirani ni wa hivyo? Bana eee idadi ya watu wanaotenda kosa, haiwezi kuhalalisha kosa..

uchumi wa dunia ya tatu unategemea sana dunia ya kwanza.
 
Kwa staili tanzania inavyoenda ni hatari, ufisadi angalia kagoda, deep green,richmond, rada,maliasili zinaporwa, elimu inashuka, epa, tanesco wanaagiza nguzo nje wakati zipo mafinga, mgao wa kupanga, usalama wa taifa umeoza, jeshi la polisi lilikosa weledi hivi kutumia mamilioni kumkamata munge kisha kesho yake anapewa dhamana utafikiri ni jambazi ni uthibitsho wa jeshi letu kukosa weledi, raisi muoga hawezi kushughulika changamoto hizi tunataka raisi mwenye maamuuzi magumu ingawa wengine watakuona dikteta ila utaikomboa inchi hii vinginevyot ???????????????

Kweli mimi mwenyewe na suport kwa hali iliyopo,hali ni ngumu ya maisha watz wenyewe wanahitaji hilo, hata hofu ya mungu watu hawana, Utu wenyewe hakuna,Tumwombe mungu asaidie taifa letu!
 
Kweli mimi mwenyewe na suport kwa hali iliyopo,hali ni ngumu ya maisha watz wenyewe wanahitaji hilo, hata hofu ya mungu watu hawana, Utu wenyewe hakuna,Tumwombe mungu asaidie taifa letu!
sawa mkuu tuko pamoja mpk magmba yatoke
 
Plato alikuwa ni moja Kati ya ma ' DICTATOR WAZALENDO 'Nyerere alikuwa ni mfuasi wa Plato, pia Nyerere, alikuwa Dictator Mzalendo. Nimeongezea neno 'MZALENDO' ili kuondoa maana mbaya ya neno 'DICTATOR' Kama ilivyozoeleka kwa watu wengi, Kwa kifupi namaanisha, Tanzania tulipofikia kwa sasa tunahitaji kiongozi ambaye ni 'DICTATOR' ili tusonge mbele Kama Taifa. Hii Democrasia tunayoipigia kelele na kuitaka kila kukicha ndiyo imetuweka ktk basi ambalo Ma dereva wake hawajui wapi tunaelekea hivyo hata wakitumwaga mtoni kwao ni sawa tu.


''Plato, Myunani wa kale, alipendekeza kuwa mafilosofa ndio wanaofaa kuwa watawala wa nchi, maana wana sifa mbili muhimu: Kwanza wana uwezo wa kutawala, na pili hawapendi kutawala. kwa hiyo jamhuri ya plato itakuwa na sheria ya kuwalazimisha mafilosofa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikiisha, atafurahi sana kurudia shughuli zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazozipenda. lakini nchi zetu hazitawaliwi na mafilosofa wa plato; Watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala, hata kama hawana uwezo wa kutawala; na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa watawala, na wakisha kuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. Si busara kuwaachia wao wenyewe ndio wawe waamuzi wa lini waache kutawala''.

- Julius Kambarage Nyerere, Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Ukurasa wa 8.


Defenders wa Democrasia karibuni tujadili kwa kina kuanzia hapa kwa Plato na Nyerere Kama ma dictator wazalendo.....Kama una swali lolote la kuhusu wana filosofia wa siasa toka Enzi za wayunani, wajerumani , waingereza, wa denish, wafaransa N.K

Karibuni

'' Kama SOCRATE ni Mwana falfasa basi hata MWANAMALUNDI ni Mwanaafalsafa''- Andrew NKumbi
 
udikteta wa nyerere ulitufikisha wapi kimaisha? napata tabu na uwezo wako wa kufikiria. tanzania tunachotaka ni viongozi wenye vision, basi.
 
udikteta wa nyerere ulitufikisha wapi kimaisha? napata tabu na uwezo wako wa kufikiria. tanzania tunachotaka ni viongozi wenye vision, basi.

''Wanapenda sana kutawala, hata kama hawana uwezo wa kutawala; na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe''
- Julius Kambarage Nyerere,

Kupata shida juu ya uwezo wa mtu kifikiri ni kawaida sana mbona, inategemea ni jinsi gani umefikiria kufikiri uwezo wa kufikiri wa mtu na Kama ukifikiri vibaya ni ngumu kupata kujua nini hasa nilikuwa nafikiri na hata kufikiri na kuamua kuweka nukuu ya Mwalimu.

Ukijitahidi na ukitaka kunielewa utanielewa, ( fanya hivyo)

NB: Hata dictator Ana VISION ndio maana anaamua kuwa Kama anayotaka kuwa, na hata viongozi wa sasa pia wana VISION na bado Taifa Lina didimia, sasa hiyo VISION ni bora ukaieleza zaidi ikapata kueleweka.

Bila Mwalimu Unayoyaona Leo huenda yangekuwa yalishafanyika miaka kumi ilitopita, Ina maana kwa sasa hivi tungekuwa ktk hatua mbaya zaidi ambayo huenda tukawa nayo miaka kumi ijayo Kama hari haitabadilika.

Nyerere sio lazima awawekee watu pesa mifukoni ndipo tu amini kuwa alitusaidia
 
''Wanapenda sana
kutawala, hata kama hawana uwezo wa kutawala; na ambao wako tayari hata
kuhonga ili wachaguliwe''
- Julius Kambarage Nyerere,

Kupata shida juu ya uwezo wa mtu kifikiri ni kawaida sana mbona,
inategemea ni jinsi gani umefikiria kufikiri uwezo wa kufikiri wa mtu na
Kama ukifikiri vibaya ni ngumu kupata kujua nini hasa nilikuwa nafikiri
na hata kufikiri na kuamua kuweka nukuu ya Mwalimu.

Ukijitahidi na ukitaka kunielewa utanielewa, ( fanya hivyo)

NB: Hata dictator Ana VISION ndio maana anaamua kuwa Kama anayotaka
kuwa, na hata viongozi wa sasa pia wana VISION na bado Taifa Lina
didimia, sasa hiyo VISION ni bora ukaieleza zaidi ikapata kueleweka.

Bila Mwalimu Unayoyaona Leo huenda yangekuwa yalishafanyika miaka kumi
ilitopita, Ina maana kwa sasa hivi tungekuwa ktk hatua mbaya zaidi
ambayo huenda tukawa nayo miaka kumi ijayo Kama hari haitabadilika.

Nyerere sio lazima awawekee watu pesa mifukoni ndipo tu amini kuwa
alitusaidia

Ongera, uu mtaalamu wa kucheza na maneno.

Tanzania tunasafari ndefu na mbele ni kiza kitupu. Back Tanganyika huwenda tukafika.

wacha nilale kwanza kukipambazuka nitarudi kuchangia. g9t
 
Ongera, uu mtaalamu wa kucheza na maneno.

Tanzania tunasafari ndefu na mbele ni kiza kitupu. Back Tanganyika huwenda tukafika.

wacha nilale kwanza kukipambazuka nitarudi kuchangia. g9t

Ahsante sana kiongozi, Edward Sambai. Ni kweli safari yetu ni ndefu sana hii iko wazi nadhani kwa kila Mtanzania zaidi Mioyo ya matumaini ndiyo inafanya angalau tujadili hata haya hapa jukwaani.

Bila matumaini ya unafuu mbele yetu, humu mbona wengi tungepakimbia . Hivyo acha tuendelee kuwa na matumaini ya Taifa zuri mbele yetu, Japo ni mbali natumai tutafika, tuko pamoja kiongozi
 
....wala hatuitaji filosofia za kina Plato kujua kuwa tunahitaji mzalendo wa kweli kuiongza hii nchi...hakika kwa tulipofikia kama nchi....mkwamo huu unahitaji mtu mwenye uthubutu wa kufanya yale ambayo hata marafiki na wapambe wake hawatayapenda....mtu atakayekuwa tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya taifa hili....mtu atakayewaadhibu wale wote walioriharibu taifa hili.....maana nchi hii imepoteza kabisa mwelekeo...hatuna misingi yoyote ya maana tunayofuata kama taifa....hata yale mazuri yote yaliyoachwa na waasisi wa taifa hili yameharibiwa......nchi hii inahitaji ukombozi wa kweli katika fikra za watawala.....hatuwezi kusonga mbele kama taifa kwa hali hii....inaumiza sana..

....inasikitisha pia kuona bado kun watu...tena wasomi wanaotegemewa kulikomboa taifa hili...bado wanafikiri kuanzisha vyama vipya vya siasa ndio dawa ya kutibu virusi vya kimaadili vya taifa hili.....hii si kweli.....ukombozi wa taifa hili utaanza na mtu mmoja kwenye nafasi ya urais wa taifa hili.....maana mkwamo tulionao kama taifa umechangiwa kwa asilimia kubwa na watawala wa miaka hii katika taifa hili.....

...Tiba halisi ya mkwamo huu itaanza na uwepo wa rais mzalendo wa kweli atakayekuwa tayari kusimamia misingi ya katiba, sheria na haki ...mu atakayeweza kuwaadhibu hata jamaa na ndugu zake pale watakapovunja sheria za nchi.....mtu atakayechukia rushwa....tukianza na kiongozi wa namna hii....basi tutakuwa tumeipata tiba ya mkwamo huu kama taifa....sijui tutampata lini kiongozi wa namna hii....tuliwahi kuwa na Sokoine....hadi sasa hatujawa na kiongozi kama huyu.....watu hawa ni nadra sana kuwa nao ....na bahati mbaya sana watawala huwa hawawavumilii...........


....Namwona Mh.Lissu kuwa mtu ambaye taifa hili angeweza kulikomboa....lakini kwa siasa chafu tulizonazo...mtu huyu anapigwa vita na watawala vibaya sana...maana wanajua huyu ni wale wachache ambao kama atapata nafasi ya uongozi wa taifa hili anaweza kuja kuwaadhibu watawala woote waliopita kwa matendo yao wakati wa utawala wao.....maana Lissu ni mpenda haki...na anasimamia sheria....kama anaweza kudai haki za waasisi waliokufa.....na hata kuhoji matendo ya waasisi...basi hatashindwa (kama akiwa kiongozi) kuja kuwawajibisha watawala wa sasa na waliopita kwa matendo yao....mfano; mauaji ya wazenj enzi ya Mkapa....msamaha wezi wa EPA ....wizi richmond...dowans...mauaji na mateso ya raia(kina Ulimboka...Kibanda..Mwangosi na wengine)...mauaji operaton tokomeza n.k. n.k.....Madhila haya yote yamefanywa na serikali za watawala(wa sasa na waliopita)na lazima watu makini wakiingia madarakani wawajibishe.....Ndio maana watu kama kina Lissu wanapingwa na watawala kwa nguvu zote....wanajua hawatapona watu hawa wakikamata dola..... Its just a matter of time....
 
Naungane nawe kumtafuta dictator mzalendo na nimekuwa nikisema kuwa nchi hii inamhitaji mtu mwenye msimamo thabiti na maamuzi yasiyopindishwa na mwenye uchungu na nchi hii ivyo anatamani aone nchi yenye mabadiliko hata kama ni miaka 10 ijayo.

Watu wanadhani kuwa dictator ni kuwa hovyo hovyo tu na kufanya mambo bila justification, si kweli ila zaidi ni kuwa na timu ya waandamizi yenye akili akili na msimamo sahihi lkn bado ww ukabakia kuwa na maamuzi sahihi na dhabiti zaidi juu ya yale mnayotamani kuifanyia nchi yako. Hivyo bado udictator una vision ambazo kwazo huzisimamia kikamilifu
 
Nkumbi tatizo la Tanzania sio demokrasia kwani nchi ngapi zenye demokrasia zina maendeleo? Tatizo la Tanzania kubwa sana ni tabia na utamaduni wa kutokuwa watekelezaji na tuna tabia ya kuangaliana zaidi kuliko kuangalia taifa.
 
Tunaitaji viongozi wenye kufikiria tofauti na ambao ni watekelezaji zaidi. Wengine tulishatoa mawazo lakini utekelezaji wake ni mgumu kwasababu watanzania wanapenda ushabiki zaidi ya vitendo

Mfano mdogo jinsi ya kuongeza kipato na kupunguza matumizi

Ajiri kampuni ya utawala ya kitaifa kama Price coopers au arnest young wafanya uchunguzi kuhusu vitu viwili vikubwa (1) Kodi je ni kodi gani zikirekebishwa zitaongoza maendeleo ya uchumi mfano kiwango cha kuingiza magari kiko juu au chini, kina sadia uchumi au kupunguza magari (2) uchunguzi wa idara zote za serikali na kujaribu kuongeza ufanisi na kupunguza matumizi. Kwa sasa maamuzi mengi ni kwa wanasiasa ambao hawana ujuzi au utafiti wa kuangalia vitu. Mfano mwingine je ni kwanini watu wanatumia mamilioni kufungua biashara wengine wanatoa hata rushwa kufungua kampuni wakati pato la taifa linategemea kodi ya kampuni ni kwa nini serikali inaweka ugumu wakati haina cha kukosa.
 
Kiongozi , Kamundu, Utakubaliana na Mimi kuwa ili Taifa lipige hatua hasa kiuchumi, Democrasia ni lazima iwe ya herufi ndogo. Na hii Democrasia ya herufi ndogo ndiyo hii niliyomaanisha inahitaji' Dictator Mzalendo'

Kama ulivyochangia hapo juu kuwa Watanzania wanapenda Ushabiki ni kweli na kwa maana hii, Kiongozi atakayetaka kutekeleza Democrasia kwa asilimia 100 hawezi kulifikisha Taifa Hili na Taifa jingine lolote duniani popote pale. Na ndio maana Mimi lugha ya Dictator Mzalendo ni kumaanisha kiongozi wa kuweza kuwa na maono chanya ya kimaendeleo na kuwa tayari kwa maamuzi mengine ya lazima kwa manufaa ya Taifa pasipo kufuata huo unaoisema Ushabiki na kiongozi akiwa wa aina hii kwangu Mimi ndiye ' dictator mzalendo'

Na utakubaliana na Mimi tu kuwa ktk dunia hii ya Leo hakuna Taifa lenye Democrasia kwa asilimia 100 limeweza kupiga hatua, Democrasia kwa sasa ni Kama neno linaloabudiwa na kila Taifa, Na halitekelezwi Kama linavyotakiwa.

'' dictator mzalendo huweka kando urafiki na kazi hasa kazi ya kuiongoza jamii Yake ''- Andrew Nkumbi
 
Ili mataifa yetu (Tanganyika, Zanzibar na Tanzania) yaendelee ni sharti CCM wang'oke kwa stahili yoyote ile!
 
Nkumbi tatizo la Tanzania sio demokrasia kwani nchi ngapi zenye demokrasia zina maendeleo? Tatizo la Tanzania kubwa sana ni tabia na utamaduni wa kutokuwa watekelezaji na tuna tabia ya kuangaliana zaidi kuliko kuangalia taifa.

Mkuu Kamundu, moja ya mambo yanayokweza tamaduni hizo chafu ni Demokrasia! Kwa taifa ambalo asilimia kubwa ya watu wake huongozwa na mahaba, ushabiki na hisia zao katika kufanya maamuzi, Demokrasia ni mzigo kwao, kwani hutoa nafasi kwao kutumia upuuzi wao kufanya maamuzi. Rejea HAKI ZA BINADAMU kama msingi wa Demokrasia! Almost all African countries ziko hivyo.

Na kwa raisi yeyote yule katika nchi zetu udikteta wake ni jambo nyeti katika kutambua Uzalendo wake kwa nchi yake. Kama unaipenda nchi yako haswaa, basi hakuna namna ya kutotumia dictatorship kama raia wako walio wengi wanatumia zaidi hisia zao(mahaba/ushabiki) badala ya critical thoughts katika kufanya maamuzi!

Tz hata kwenye uyanga na usimba unashinikiza maamuzi yetu kuamua masuala nyeti ya Taifa. Hapo bado kuna udini, ukabila, ukanda, uchama, u-handsome, sauti, cha mfukoni kwanza, n.k. Ni upuuzi kiasi gani eti kudai unalinda demokrasia na ukawaacha hao kufanyia maamuzi mustakabali wa TaIfa?
Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Kuna siku nchi hii itaongozwa na mashoga kwa utaratibu huu wa demokrasia maana kizazi hiki kinaongozwa na watu wasiofikiri vizuri waimba taarab bungeni na wasiopenda ukweli.Hawa watawala wanatumia vyombo vya habari kama mawingu efem kuwapumbaza vijana na kuwafanya kama wanawake wanaosubiri kuolewa.Huku wakisaidiwa na wasanii nyota wa bongofleva walioanza kuvaa sketi na mavazi ya kike(huku wao wakiwa wanaume)ili kuwafanya vijana wetu wawe na akili ya kikekike tu.Sasa asipotawala dictator mzalendo hii nina hofu hii nchi itakufa!Hili neno demokrasia haliwafai wapumbavu katu!na wengi wa watanzania wako hivyo hivyo tu bila kujali elimu yao

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom