Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

Upo udikteta wenye matokeo hasi na chanya kijamii,kiuchumi,kisiasa...
Yapo mataifa yamesonga mbele na yanasonga mbele sababu ya udikteta chanya Mfano Marekani,China,Malyasia,Singapole,Russia..nk.Lakini yapo pia yanayorindima kwenya dimbwi la umaskini.

Tanzania ili isonge mbele haina budi kuongozwa kwa mfumo wa Demokrasia ya kidikteta la sivyo ni ngumu mno na hasa ukiwa na ufahamu halisi wa nini kimekuwa kikiendelea katika mifumo mbalimbali ndani ya nchi.

Kuna mambo yanakera mpaka waweza tamani ufe kuliko kushuhudia yanayofanyika na baadhi ya wenye mamlaka wenye uroho wa ufisadi,kansa ya rushwa na utapiamulo wa ubinadamu.Vilio vingi havina budi kuwepo sasa sababu ya udhati wa kupambana na uovu,dhambi,uchafu,uzandiki,ufisadi...safisha safisha inayoendelea ina neema kubwa kwa vizazi vijavyo...

Kuna wakati demokrasia ya kuwapendezesha wafadhiri/wafaidi rasilimali kwa mgongo wa misaada/mikopo/ruzuku kupitia taasisi zisizo za kiserikali na propaganda za kisiasa imepelekea umaskini endelevu katika jamii nyingi kifikra,kimtazamo,kimaamuzi...
 
naonga mkuno hoja , 100% . hadi mahakama zetu watu wanazihongo na hakimu anapata anatoa hukum ambayo ukimuuliza vifungu vya kisheria alivyotumia kutoa hukum hiyo hawezi kukujibu mpaka kiama
 
Wananchi wa nchi hii bana.... Wakati wa Kikwete utawasikia "Nchi hii bana inahitaji kuongozwa na Rais Dictator" Mwenyez Mungu ametujaalia Rais mwenye vimelea vya udictator wameanza.... " Oohhh Rais huyu anatuendesha kuductator" Pigeni kimya mmetaka Dictator mmepata Dictator..... Mzee Magu kanyaga Mwendo twende.. Hakuna kusikiliza mtu. Btw wew Kama Rais huwezi mridhisha kila Mtanzania.... Binafsi nakubali kazi zako baba[emoji603][emoji100]
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Dk Antony Diallo, amesema anatamani rais wa awamu tano awe dikteta, lakini anayepatikana kwa njia ya kura ili awatie adabu Watanzania.

Dk Diallo aliyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa ngazi za juu wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, katika kikao alichokiitisha kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya namna ya kuboresha shughuli za jiji la Mwanza.

Mwenyekiti huyo wa CCM, alisema kuwa hivi sasa taifa linakabiliwa na tatizo la wananchi, hasa wanasiasa la kutotii sheria na kujiamulia mambo kiholela na hivyo kuleta hofu kwa wananchi.

"Ninatamani sana rais ajaye wa awamu ya tano awe dikiteta, lakini ambaye atakuwa amechaguliwa kwa kura na wananchi, ili aje atutie adabu, kwani taifa liko katika hali mbaya, kila mmoja ni mjuaji na yote haya yamekuwa yakisababisha uvunjifu wa amani," alisema Dk Diallo.

"Watanzania ni waoga sana, wakisikia mlio wa bunduki wengi watakimbilia uvunguni mwa kitanda, tunataka Rais ajaye awe dikteta ili ainyooshe nchi hii, kwani imefikia katika hali mbaya, kuna watu wanaichezea amani yetu na ni mabingwa wa kuhamasisha vurugu na wanazungumza mambo wasiyoyajua," alisema Dk. Diallo, ambaye pia amewahi kuwa Naibu Waziri na Wizara katika serikali za awamu ya tatu na nne.

Mwenyekiti huyo pia alisema kuwa sheria za nchi pia zinapaswa zitazamwe upya katika kuilinda nchi hii kuepuka kupata viongozi wasiofaa na kuitaka Idara ya Usalama wa Taifa kuhakikisha inaisaidia serikali katika kupata viongozi bora na wasio na kasoro.

Alisema kuna baadhi ya maeneo baadhi ya watu wamejipenyeza kugombea uongozi na kushinda, huku wakiwa si watu safi, hali ambayo inaiyumbisha nchi.

"Kuna baadhi ya wabunge na madiwani ni X Criminals, ni wahalifu sugu wamefanikiwa kushika nafasi hizo, hapa unatarajia nini na kuna kiongozi mmoja hivi sasa ni kiongozi wa chama cha siasa katika ngazi ya wilaya huyu siyo Mtanzania, tatizo hapa katika siku za karibuni vyombo vyetu vimelegalega," alisema Dk Diallo.

Chanzo: Mtanzania

Tujikumbushe jinsi baadhi yetu walivyotamani Rais awe dikteta ingawa wengi tulisema hii si jambo jena

Sasa tunasema tunataka Rais anayecheka nasi na kutumia lugha nzuri na kumsingizia Rais Magufuli eti dikteta wakati kaamua tu kutumia nguvu aliyo nayo kikatiba na kufanya maamuzi magumu

Bindamu haturidhiki!
 
Kiukweli magu yuko poa je wakulima tungepanga wapi uongozi kama sio watoto wa wakubwa nimeamini hatujipendi mzee heshima imerudi
 
Rais Magufuli ana utashi wa kisiasa na siyo dikteta. Anakamilisha falsafa ya Baba wa Taifa kuwa ili nchi ipate maendeleo inahitaji vitu vinne: watu, ardhi, siasa safi na uongizi bora (Rais Magufuli na utashi wa kisiasa)
 
Bado valid!! point 2014

"
Udikiteta na uzalendo hauendani kabisa. Hakuna mtu hata mmoja dunia hii anaye juu kuliko systems. Nchi haziendeshwi kwa ubabe pekee nchi zinzendeshwa kwa utaratibu mzuri na jamii zenye nia ya kujikimu kiuchumi. Mimi ni mpenzi wa system ya kibepari na ninaamini vitu vikubwa viwili (1) Ili kufanikiwa ni lazima uwe na haki ya kutokufanikiwa (Fail) (2) Watu wakifanya kazi kwa uoaga kwa sababu ya dikteta watachoshwa Ngoja ni fafanue vizuri
ya (1) Utaratibu wa ujamaa hauruhusu serikali au biashara kufeli na ndiyo maana kuna kampuni nyingi zinazoenda kwa hasara. Kwa sababu hii vilevile ujamaa una chukia washindani kwasababu kama biashara au shirika la serikali halifanyi vizuri wanasingizia ni kwasabu ya ushindani hivyo ujamaa ni system isiyo na ubunifu na ndiyo maana miaka ya nyuma vitu vingi sana viligunduliwa kwenye nchi zenye system za kibepari (2) System ya kidikteta ni kama ya jeshi ni ya misheni na kwa misingi hivyo haiwezi kuwa ya muda mrefu watu watachoka. Binadamu unaweza kuwaongoza kwa muda kwa kulazimisha lakini kila binadamu ni tofauti hivyo baada ya muda hii system inashidwa mfano Musevi watu walikuwa wanampenda lakini sasa wamemchoka. Vilevile kama tunaongozwa kwa kutegemea mtu mmoja je akifa tutapata mtu anayefikiria vilevile?
Lakini kikubwa zaidi ya yote mwandishi ameonyesha upungufu wa utamaduni wetu tunafikiri tatizo ni mtu raisi pekee narudi kwenye utamaduni wa kuangaliana watu!! tatizo ni system na culture yetu imeingiwa na hii system ambayo haijui vinginevyo. Na hata kama tukiwa na mawazo watu watakuangalia wewe binafsi na si mawazo yako"
 
Hahahahaahahah...huu uzi umenikumbusha mbali sana. Aisee hii mitandao kwa kutunza kumbukumbu ni balaa!!!!
 
Back
Top Bottom