Diallo amlipua Lowassa

Diallo amlipua Lowassa

Si kimkakati tu, hata kimwili pia.

hahahahahaha mkuu, ni kweli aisee watamzika kimwili, manake mpaka inafikia Membe na jopo lake kufatilia ripoti ya afya ya jamaa ni wazi wanaweza kufanya kitu ambacho ni worse than that...
 
Membe kweli hachoki kuratibu Uchonganishi na Uzushi baada ya kufeli kumchonganisha , mwandosya,January , familia ya Jk , wasira sasa kaanza Uchonganishi Kati ya Dialo na Lowasa ! Membe nenda kabuni mbinu zingine hii ya Uchonganishi umefeli tayari, hata uchonganishe Lowasa na mawaziri wote Hakuna atakayekupa ridhaa ya kuingia ikulu, wewe endelea kukesha, Kuwa busy na kutengeneza Uzushi juu ya Lowasa mpaka siku ambayo utajitambua Maana sasa fikra zako zipo gizani.
 
Dialo anaoneka mpuuzi tu, mbaya zaidi mtu unayemshambulia hana muda na wewe, Dialo wewe pambana kurudisha ubunge wako mipasho haitakusaidia.

Kaka nafkiri umenena vyema mkuu........kama hakuna ambaye hatakuelewa basi atakuwa na matatizo ya akili........big upu umemaliza kila kitu
 
Membe kweli hachoki kuratibu Uchonganishi na Uzushi baada ya kufeli kumchonganisha , mwandosya,January , familia ya Jk , wasira sasa kaanza Uchonganishi Kati ya Dialo na Lowasa ! Membe nenda kabuni mbinu zingine hii ya Uchonganishi umefeli tayari, hata uchonganishe Lowasa na mawaziri wote Hakuna atakayekupa ridhaa ya kuingia ikulu, wewe endelea kukesha, Kuwa busy na kutengeneza Uzushi juu ya Lowasa mpaka siku ambayo utajitambua Maana sasa fikra zako zipo gizani.

Kazi yake kubwa usalama ni Disinformation. kuna kitabu kinakuja kuelezea kazi ya huyu jamaa hapo makumbusho......

Disinformation is false or inaccurate information that is spread deliberately with intentions of turning genuine information useless. For this reason, it is synonymous with and sometimes called black propaganda. It is an act of deception and false statements to convince someone of untruth.
 
Heko Diallo!! Mafisadi yanararuana!!

Unakumbuka kilichomfukuzusha Dialo Uwaziri? Uliza uambiwe huyo boss wako ni full fisadi vioja alivyofanya wakati Akiwa Waziri havifai hata kuhadithiwa ,? Nenda kawaulize wafanyakazi wake kwenye miladi yake utaambiwa udhaifu wake Nina imani utazimia ukiamka unawalaani wote waliopata kumteua Kuwa Waziri kwani hakuwa na vigezo.!
 
Lowassa hawezi kumwaga lolote kwani kwa uchafu wake akienda kwa kuchafuana ni yeye atakayeumia zaidi.

Sijui kama kuna uchafu zaidi ya kuuza unga (madawa ya kulevywa), au pembe za ndovu......je ni Lowassa au kambi yake waliokamatwa China na madawa ya kulevya? nakuachia ujibu mwenyewe

Pili yule mzungu aliyekufa juzi MayFair Plaza kabla ajafa tarehe 18/9/2014, saa kumi na moja jioni alionekana na nani maeneo ya Sea Cliff ? jibu mwenyewe....KUMBUKA ALIKUFA NA MADAWA YA KULEVYA AKIWA ANAOGA......DETAILS ZIKO WAZI na soon mtaona washirika wake wa sembe humu humu, just stay tuned
 
..........Namsema EL kwa sababu ni mchafu, na sasa sitayasema yaliyo mazito au machafu zaidi dhidi yake, hadi nitakapoona kweli kachukua fomu kugombea Urais!..........kumbe hii ni rasharasha, masika bado!
 
......eti EL akizunguka uwanja wa taifa mara moja tu, lazima ajikute ICU!........siongezi neno mimi...!

Speed yake ni 10km/hr. vijana wa mama salma watakufa safari hii mkuu, jamaa yao Membe HAUZIKI kabisa
 
DIALO KAJIBU HIVI;


"Tuhuma za Kundi la Makuwadi wa EL dhidi yangu hayana msingi wowote na kama ni kweli Edward amewapa waziseme kwangu na kuhusisha Mheshimiwa Rais ni mwendelezo wa EL kumdharau Rais ambaye alimpa madaraka makubwa na kosa likiwa kukubali ajiudhuru baada ya kufanya madudu aliyoyafanya. Huu ni mwendelezo wa kumsumbus Rais ambao ulianza tangu 2008 baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu. Anayoyasema haya sipendi kuyajibu ila kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa, imebidi niyajibu lakini nikizingatia kuwa sitaweza kuyajibu yale ninayoyajua chini ya kiapo:

1: Sijamtuma Mzee yeyote kwenda kwa Lowasa kwa sababu sio waziri mkuu tena na hata kama angekuwa bado waziri mkuu nisingeweza kumwambia mtu akaniombee vyeo kwa Lowassa. Hao wazee aliowataja wapo Mwanza na mnaweza kupata namba zao za simu na kuwauliza kama nilishawahi kufanya hivyo. Pili, mwaka 2003/4 haukuwa mwaka wa uchaguzi, ilikuwaje niende kuomba cheo wakati niliingia baraza la Mhe. Rais Mkapa 2001? Wakati huo Lowassa hakuwa waziri mkuu! Tatu, mwaka 2004 sijaonana na JK na Karamagi hajanishawishi kumuunga mkono JK mwaka 2005. Mimi ndiye niliyetumwa kumwambia Lowassa asigombee 2005 kwavile dhambi na tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Mwalimu zilikuwa kwenye mioyo ya watanzania na asingeweza kupata kura za ushindi isipokuwa angempunguzia JK kura zake na wote kukosa. Karamagi tumekutana naye bungeni baada ya kuchaguliwa ubunge baada ya kifo cha Mhe. Kinyondo. Mimi nimezaliwa na kukua kwa kuzingatia nidhamu ya Kisukuma, sijalelewa kihuni kufika kumsema mtu kama JK. Namsema EL kwa sababu ni mchafu, na sasa sitayasema yaliyo mazito au machafu zaidi dhidi yake, hadi nitakapoona kweli kachukua fomu kugombea Urais! Mimi sijasema Lowassa alidhulumu CCM kupata hisa Vodacom, nilichosema CCM ilikuwa iwe mbia wa MTN, kampuni iliyonyimwa leseni wakijua fika kuwa ilikuwa ikisaidie chama, badala yake wakafanya njama kuvunja tume ya mawasiliano kihuni, na hapohapo wakaipatia vodacom leseni lowasa kwa kutumia watoto wake, alipata walikipata. Ushahidi kuhusu hili ni kampuni yake kupewa U-Super Dealer wa Vodacom ambayo uliwafanya wanufaike kwa kuuza simu nchi nzima.

Kama wanasema Lowassa ni mzima, naomba akakimbie uwanja wa Taifa azunguke hata mara moja kama hataishia ICU. Na kama ni mzima, anatumia fedha za nchi kwenda kutibiwa nini ujerumani kila wakati au Ujerumani nako siku hizi kuna waganga wa kienyeji? Pili kwanini alikwenda kuombewa kwa Emmanuel Ministries huko Nigeria? Kampeni za Urais zinahitaji afya nzuri, sio mzaha kuweka mgonjwa akatufia kwenye jukwaa! Kuhusu tuhuma ya rushwa toka kwa Kimaro, nina hakika Kimaro bado yupo hai, na kama ni mkweli aseme ukweli. Kimaro ni rafiki yangu na nilimshawishi akawekeza hoteli ya Nyumbani sasa ni JB Belmonte, Mwanza. Sijachukua fedha ili nimpatie kitalu kwavile yeye sio mwindaji na sijasikia kuwa ana hiyo biashara. Ninachofahamu ana mahoteli na ndiyo biashara yake. Rais yupo kama alishaniita kunieleza hilo anaweza akasema, ni mkweli. Tuhuma za mimi kuhongwa na Kimaro alizianzisha Lowassa baada ya mimi kutaka kumuondoa Mkurugenzi wanyama pori wizara ya Maliasili. Mkurugenzi huyo alikuwa na mahusiano naye na baadae walikuja kuoza watoto wao. Hilo kila mtanzania analifahamu, na alimtetea sana abaki wizarani wakati huo. Lowassa yupo kwenye mtandao wa yote yanayosemwa kuhusu wanyama pori. Pia tuhuma za kumtapeli aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Mhe Karume ndio nazisikia leo. Karume sijafika nyumbani kwake Zanzibar na wala hata alipokuwa Ikulu Zanzibar. Yupo na anaweza kuulizwa, ni mkweli atasema yaliyo kweli.

Huyo msichana anayesemekana nilimpa mimba, mhudumu wa Dodoma hotel, ndiyo namsikia leo, na kama yupo aniletee mtoto huyo kwani ndio nasikia kwenye watu wa Lowassa baada ya kuweweseka na machache tu tuliyoyaweka hadharani. Mwisho la kupewa fedha na mtuhumiwa wa IPTL nalo jipya simfahamu, labda Lowassa anamfahamu! Tatizo la huyu Lowassa, ni kupata URAIS, asipoupata sijui kama atabaki na afya ya kuridhisha. Anatuhumu watu tusiounga mkono jitihada zake tu, je wanaogombea watakuwa na hali gani mbele yake? Ushauri wa bure kwa wapambe wa Lowassa: Kuleni fedha yake maana ni halali yenu, fedha za kukwapua kwa njia zisizo halali ni haki ya kila mtu kuzitafuna, ila Urais hatopata.Kidumu Ccm."
 
Rais zitto kabwe tu hawa wengine msiba tu..sasa yeye diallo kama aliyajua haya kwa nini asiyaseme kitambo na kuyaripot sehemu husika?

lowa-hasa kamwaga mboga watu wanamalizia na ugali kabisa.
 
Asante ya nini?afukunyue nini ? Wananchi wapi? ni wewe pekee na wajinga wachache sana wanaweza kukaa na kumsikiliza Dialo, usifikiri kwa kisogo jitambue.

nchi hii haiwezi kuongozwa na fisadi naikiwa hivyo mimi narudi kwetu Ukerewe.
 
Back
Top Bottom