Dhana ya vua gamba vaa gwanda: Je, tunayakubali yale tuloyakataa na kuyapinga?

ayhan2000

Member
May 3, 2012
26
3
Nafikiri nahitaji kuzungumza kiasi juu ya Dhana hizi mbili za Vua Gamba na Vaa Gwanda.... **Miezi kadhaa iliyopita CCM ilikuja na dhana ya VUA GAMBA falsafa hii ilipigwa vita na kupingwa na CHADEMA kwa hoja kuwa nainukuu.."HATA KAMA WATAJIVUA GAMBA BADO MWILI NI ULEULE NA SUMU NI ILEILE-Kama nyoka.."mwisho wa kunukuu LAKINI hivi sasa kuna dhana ya VAA GWANDA VUA GAMBA..nashindwa kuelewa Je!Mtu akivaa GWANDA mwili nao unabadilika??na Je!sumu nayo inapotea?? **Ninachoamini mimi kwa kutumia kauli na tafasiri ya CHADEMA juu ya dhana ya vua gamba ni wazi kuwa hata wale wanaovaa Gwanda bado wana miili ileile na sumu ileile...sasa basi Hatuoni kuwa Chadema inawapokea watu ambao iliwakataa mwanzo??hatuoni kuwa Chadema inapokea watu walewale...wenye miili ileile...na sumu ileile...ni ipi dhana halisi na udhati wa vaa Gwanda dhidi ya vua Gamba???....mmmh Politics!
 
CHADEMA wao kazi yao ni kurukia kila hoja ya CCM, hawana jipya.

Leo Zitto kashushuliwa kwa kurukia hoja za CCM, alifikiri akiziongea Washington, Tanzania hawatozisikia. Namsikitikia sana yule kijana kwa kuishiwa na ubunifu.
 
Hakuna cha kushangaa hapo watanzania hatutaki kudanganyika tena, tumeamka sasa na wanachokisema CHADEMA ni ukweli mtu hatuwataki tena mafisadi kama ni hoja zako binafsi za kuwakumbatia mafisadi kila la heri ila sisi tutahakikisha CHADEMA inashika dola. Nenda vijijini uone watu wanavyokufa kwa kukosa huduma muhimu.
 
hoja imebadilika baada ya ccm kushindwa kuvuana magamba ! Sasa imetafsiliwa kuwa mwana ccm ni kuwa gamba maana haieleweki nani mwizi nani msafi! Kama ccm wangeanzisha hiyo dhana na kuitekeleza chadema wasingewaambia watu wavue magamba.
Kwa sasa gamba lenyewe c m2 mwiz Bali ccm yenyewe ndoo gamba na gwanda ni CDM!
Big up chadema kwa ubunifu!!!!!
 
Back
Top Bottom