Je, Intergovernmental agreement (IGA) kati ya EMirate of Dubai, au The United Arab of Emirate, DP worl na JMT ni MoU?

HANGAYA THE CHIEF

JF-Expert Member
Sep 10, 2021
329
947
Utangulizi:

Naheshimu sana mawazo ya watu, ila kama taifa tuna shida mahali, nadhani ni sababu ya rushwa ikitamalaki inapofusha macho (sitaki kuhukumu sina uhakika ila kwa jicho la tatu DPW kuna harufu ya rushwa kubwa sana, maana sio kwa udalali unaofanyika sasa katika ngazi zote, kwenye media usiseme, viongozi wetu wamewekwa mifukoni .......................... nadhani wanaitamani hii investment kuliko sisi tunavyotamani huduma yao.........) au ghalama walizotumia kufanya lobying ni kubwa kuliko matarajio yao.

Tuendelee kujenga taifa letu; si wakati wote kila mtu anaweza kuongea chochote hata kama sio eneo lake la ufahamu, kwa mfano maswala ya afya tuwaachie madaktari watueleze, maswala ya uchumi tuwaachie wachumi watueleze, maswala ya sheria tuwaachie wanasheria watueleze, na kadhali na kadhalika, kuna maswala ya ujumla tunaweza kuwa na mawazo tofauti kulinga na utashi na uwelewa na experience tunazopitia.

Mkataba wowote ni sheria, una muunganiko wa mambo mengi sana mpaka uwe na nguvu ya kisheria (enforcement). Kama taifa tumeingia kwenye sintofahamu nadhani shida inaanzia pale serikali inaponyima watu uhuru wa kuongea; watu hawako wenyewe, (free). hivyo imejipa ifinyu wa maeneo na haiwezi kutumia wataalamu wake walio ndani serikali au wazalendo wenye lengo la kusaidia. hivyo ukiwa tofauti unaoneka wewe ni mpinzani, mdini, mkabila, mdau bandarini.

Mnataka kusema TZ hatuna wataalamu wa international trade, hatuna wachumi?, hatuna wanasheria katika mawanda ya uwekezaji na sheria za kimataifa? Dah ni aibu sana, siasa chafu zinaharibu taifa letu sana, kweli ili tushawishi watanzania kuwa mkataba wa DPW na JMT ni mzuri inabidi tulipie machawa waende kuhoji makuli Dubai, kuwa hatuwezi kuona uzuri wa mkata kwenye mkataba. Kwa kweli ni aibu ya karne, tumepoteza sifa ya kuwa Taifa.

Nirudi kwenye mada yangu,

MAANA YA INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT (IGA),

“inter” imetumika kama prefix (neno tangulizi likiwa na maana ya between, amidst, among), “governmental” serikali “agreement” makubaliano, wengine hutumia “understanding” (consus ad idem)

Kwa hiyo ukienda kwenye tafsiri sisisi (moja kwa moja) IGA ni “ makubaliano kati ya serikali mbili zenye mamlaka kamili ” mathalani inaweza kuwa kati ya Tanzania na Kenya, au Msumbiji na Tanzania, lakini kwa muktadha wetu wa bandari ni JM ya Tanzania na Serikali ya Dubai (kadili ya mkataba dubai ni nchi, kama kuna nchi inaitwa Dubai).

Swali hapa Je, kila makubaliano (agreement) ni mkataba?

Hapana
, si kila makubaliano ni mkataba, ila makubaliano yenye guvu ya kisheria ni mkataba. (hapa inategemea sheria husika kama makubaliano hayo yanakidhi viwango vya sheria).

Je, “IGA” kati ya JMT na Dubai Emirates ni mkataba au si mkwataba.

Makubaliano yeyote kati ya nchi na nchi yenye nguvu ya kisheria yanaitwa “treaty” na ili mkataba wa nchi hizo uwe na adhi hiyo lazima uoane na (conform with), Vienna Convention on the law of treaties, (VCLT)1969. Kwa mfano ibara 6 (VCLT), 1969 inasemea nchi hizo lazima ziwe na uwezo (capacity), kiufupi lazima iwe states, soma pia, characteristics of states, kwa mujibu wa Montevideo Convention on the Rights and Obligation of states, 1933) (swali hapa, tumeingia mkataba na Emirate of Dubai au United Arab Emirates au DPW, japo hilo sio sehemu ya mjadala. Ukienda ibara ya 7 ya VCLT, 1969 inaeleza mwenye mamlaka ya kusaini ni Rais na kama hafanyi hivyo basi anampa mtu full power (power of attorney’s hili nimeliongelea sana kwenye andiko liko hapa). Kifupi kisheria aliyesaini ni Rais, sababu mbarawa alipewa instrument, ya kuonyesha ana ridhaa ya nchi kusaini mkataba huo.

Kwa kifupi, mkataba wa kuuza bandari za Tanganyika kati ya JMT na Emirates of Dubai, ni mkataba wa kisheria, (its enforceable in the eyes of laws), nchi yeyote kati ya Tanzania au Emirate of Dubai, au the United Arab Emmirates, (nota bene: power of attorneys yao imetumia hayo maneno yote), inaweza kupeleka shauri kwenye mahakama za kimataifa za uwekezaji, yaani International Centre for Settlement of Investment Dispute (ICSID) kwa kutumia sheria hii:

Kwa nini IGA kati ya JMT na Emirates of Dubai, the United Arab Emirates ni Sheria.

Kuna sheria za aina mbili, yaani Municipal Laws (domestics laws) and International laws. tukiachana na hiyo ya kwanza, international laws (sheria za kimataifa) ni sheria ambazo kama nchi zinaridhia, kwa kufuata utaratibu wa sheria za kimataifa za mikataba yaani VCLT, 1969.

Duniani kuna mifumo niwili ya nchi kujifungamanisha na mikataba ya kimataifa; yaani, Monism countries na “Dualism Countries” sisi Tanzania ni Dualism country ni mfumo ambao nchi inasaini kwanza mkataba halafu baadae ndio unapelekwa Bungeni, ndicho kilichofanyika ili kuweza kukidhi takwa la katiba kwa mujibu wa ibara ya 63 (3) ( e) ya Katiba ya JMT, 1977. Wenzetu wa Monism, kabla ya kuingia kwenye mikataba hiyo kwanza kabla ya kujifunga. Shida ya dualism ukipata kiongozi asiye mwadilifu anaweza kuingiza nchi katika mikataba na sheria za kipuuzi. Kwa kifupi, Mkataba kati DP world una hadhi ya sheria za nchi.

Kwa nini wawekezaji wanataka kuwe na IGA:

Hakuna sheria kabisa za kimataifa za uwekezaji za mataifa mbalimbali ambazo ni binding (no binding Multilateral Investment Treaties) iliyokubalika kuwalinda wawekezaji kwa ujumla, hivyo wawekezaji kutoka nchi za kigeni wamekuwa wakitegemea sana uingia wa mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties) kujihakikishia usalama, uhakika wa kazi zao, wa mitaji yao, kuondoa uncertainities , Kwa sababu uongozi unabadilika lakini sheria ikiwekwa itaendelea kuwalinda, hata uongozi ukibadilika wanajua tayari walishaweka sheria na kiongozi yeyote akija lazima aheshimu makubaliano hayo kwa sababu ni nchi iliingia si Rais kama Kiongozi. kwa hiyo hata utata wa ukomo wa muda kwenye Dp world sio wa bahati mbaya, ni technicalities za kisheria na kwa sababu, Hamza Johari haijui imeleta shida.​

Je, ni kweli IGA ni MoU?

Kumekuwa na dhana kuwa IGA ni MoU (memorandum of Understanding), makubaliano ya awali tu, itakuja specific contract (HGA), hizi ni adithi za uongo , na kulaghai wananchi, kwa kifupi MoU is a document which has no legal effect in law (haina madhara yeyote kisheria) kaama ile ni MoU, utatuzi wa migogoro una kazi gani kwenye Mou? Uchaguzi wa sheria (choice of law) unakazi gani kwenye MoU, uchaguzi wa sehemu ya migogoro (choice of forum) una kazi gani kwenye MoU.?​

Je, IGA ina kazi gani?
Kazi ya IGA ni kama katiba kwenye mikataba inayofuata kwenye uwekezaji, yaani Host Government Agreement, kwenye specific contracts, mikataba ya utekelezaji haitakiwi kuendakinyume na IGA, kwa sababu ndio sheria mama, yaani katiba. kwa hiyo kama mikataba hiyo ikienda kinyume na IGA mwekezaji ana option ya kushitaki kuwa mumekiuka makubaliano. kwa mfano watu wanalalamikia ardhi, kapewa bila kikomo, kwenye HGA ukisema ukomo, maana yake umevuja IGA hivyo mwekezaji anaweza kukushitaki kwa kufanya hivyo, mfano ukamwingilia kwa swala la usalama wa nchi, atakushtaki kwa sabau IGA mlishakubaliana umempa maeneo yote kwa muda usiojulika
Is there a solution? Kuna suluhisho?

Kimsingi Mheshimiwa Rais asitengeneze bomu wa vizazi vijavyo au mazingira magumu kwa viongozi wajao, au vizaji vijavyo vya wanatanganyika wenzetu, yeye kapata bahati ya kuwa Rais awatumikie wananchi kwa weredi mkubwa na kufuata ushauri wa kitaalam.
machafuko mengi duniani yaliletwa na viongozi wasio waadilifu katika mataifa yao.

Kwa hiyo basi pamoja na kwamba Mheshimiwa kashatunga sheria, Je itaanza kufanya kazi? Inategemea utayari wake na marafiki zake kama inaleta shida kwa wananchi wake, anaweza kuona namna nzuri ya kuongea nao,
ila sio Mou ni Mkataba na ni sheria za JMT kama zilivyo sheria nyingine unazozijua.​
 
Maudhui na mantiki ya andiko lako kwa kifupi ni nini haswa!
 
Unadhani kipo ambacho haswaa bunge linapaswa kujadili

Ni mkataba... au makubaliano kwa maana ya IGA?
 
Maudhui na mantiki ya andiko lako kwa kifupi ni nini haswa!
Mimi nimemwelewa na naungana naye kama nilivyoeleza kwenye bandiko lingine humu JF, pitia

huwezi kusoma, subiri kwenye majukwaa ya siasa wakusimulie
 
Kuna mjukuu wangu ambaye yupo Al Muntazir, ameniuliza kama ifuatavyo," hivi babu,kweli kuna hiyo mnaita IGA kati ya hawa DP World na nchi nyingine kama huu wetu?"
Naomba wadau mtusaidie.
 
Hapa kuna muujiza au vipi; kuwahusu hawa watoto. What a coincidence?

Wa kwangu, ambaye yupo 'KijiweTope', kaniuliza swali kama hilo hilo, nikashindwa kujibu!

Yeye kauliza kama kuna IGA kwenye mkataba wa Kampuni ya AGL ambayo imepewa ulaji kwa miaka mitano Bandari ya Malindi, Zanzibar.

Yeye kasisitiza kuwa pengine kuna IGA kati ya Zanzibar (isome kama nchi bandia ya Tanzania), na nchi inakotoka hiyo Kampuni ya AGL.

Wenye kujua haya maswala, tafadhali saidia hawa vijana nao wapate upeo kungali mapema.
 
Back
Top Bottom