Dhana ya uongo kuhusu Spika Ndugai

Dhana ya uongo kuhusu Spika Ndugai

Nionyeshe kwani Mimi ndo spika?

Vidole awe navyo ama lah inaathiri vp utendaji wake?

Awenavyo au asiwenavyo wewe inakusaidia nini?

Huko Shuleni ulienda kusomea ujinga!

Kwa akili hizi za kushikiwa na Mange upinzani utakufa kabisa TZ.
Mjinga ni wewe unayepingana na ukweli na kutetea uongo na huwezi thibitisha. Achana na hayo jibu hoja hizi. TUMEAMUA KUTUKUZA UONGO NA KUUTUPA UKWELI.

(Soma barua ya serikali kwanza - Kurasa mbili).

Wakati hali ya uchumi ni mbaya sana, serikali inatumia nguvu kubwa kulazimisha watu waamini mambo ni safi. Mazoezi ya kupandisha watumishi wa umma vyeo na kuwaongeza mishahara yamekwama kwa GIA ya uhakiki wa watumishi wa umma ulioanza mwaka 2016 mwanzoni na hadi leo uhakiki huo haufiki mwisho.

Mara kadhaa tumekuwa tukionya kwamba mipango mikubwa ya serikali haiwezi kuwa na tija kama haina muunganiko au haigusi maisha ya watumishi wa umma na au wananchi wa kawaida.

Yako maamuzi ya hovyo sana yamefanywa na serikali ya awamu ya tano kwenye baadhi ya maeneo ambayo ni moyo wa nchi. Kwa sababu nchi inaongozwa na wasiotaka kuambiwa ukweli, KILA KITU kinafichwa. Ndo maana juzi mmeona Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akijikuta akikanusha ripoti yake yeye mwenyewe juu ya deni la taifa.

Siku kadhaa zilizopita tuliona televisheni ya ITV ikilazimishwa kuiomba radhi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kosa la kuonesha "LIVE" ukweli kuhusu wizi wa masanduku ya kura kwenye uchaguzi mdogo wa marudio jimbo la Kinondoni.

Sote tunafahamu kuwa hali ya wetu uchumi ni mbaya sana, hali ya mzunguko wa fedha ni mbaya mno, thamani ya pesa yetu inazidi kuporomoka na serikali inajiendesha kwa kukopa fedha nyingi sana na zenye riba kubwa ili kuendesha miradi ya maendeleo - hata hivyo serikali na hasa Rais amekuwa akisisitiza kuwa kila anachokifanya anatumia fedha za ndani.

Unaweza kujiuliza kama tungelikuwa na hizo fedha za ndani kwa nini deni la taifa linapaa kama roketi kila siku na ni kwa nini tumeshindwa kuwapa watumishi wa umma stahili zao na kuwapadisha madaraja kwa uhakika? Kwa nini kila siku tunawapiga dana dana?

Nchi za wenzetu zinazojiendesha kwa uwazi, serikali ikiishiwa pesa za jambo fulani, inasema waziwazi na watu wote wanaelewa, maana masuala ya uchumi wa nchi ni ya kila mmoja wetu, na serikali ni wakala wetu tu.

Hapa kwetu tumeamua kuongozwa kwa UONGO na PROPAGANDA. Mtu anapigwa risasi na polisi hadharani tunaishia kusema risasi ilitokea juu au bunduki inasakwa. Uchumi wa nchi unaporomoka tunasema "we are in the right direction"... probably a direction to HELL!

.
 
Yaliyosemwa kuhusu Spika Ndugai yamenifanya nikubaliane na wahenga waliosema, uongo hupanda lifti na ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa.

Spika Ndugai wa leo sio yule ambaye watu waliaminishwa uongo kupitia mitandao ya kijamii.

Katika suala ambalo nchi yetu inapiga hatua kwa haraka ni maendeleo katika fani ya uongo na udaku.

Udaku umewafanya hata wenye elimu ya chuo kikuu wakawa hawana tofauti kifikra/kimtazamo na mtu ambaye hakubahatika kuingia na kusoma kwenye darasa la kwanza.

Wakati inafahamika kuwa mhitimu wa chuo kikuu ni critical thinker, wahitimu wengi wa Tanzania ni passive thinker. Hawa ni wale wanakubali tu kila linaloibuka kwenye jamii au mitandao bila kujiuliza kwa undani zaidi.

Haishangazi kuona habari kama za Diamond Platnumz, Zari na Wema zinajadiliwa zaidi in face value kuliko hata habari za kiuchumi.

Mtu anaanzisha habari ya uongo kuwa Spika Ndugai kwa sasa hana hata vidole kwenye mikono halafu watu wanaanza kumsifia na kumpongeza eti kwa kupata habari hiyo mapema kabla hata ofisi ya Spika haijatoa ukweli.

Spika tuliyeambiwa kwa sasa hana hata vidole vya mikono amehojiwa na Azam TV na kuonyesha kuwa uwongo hutumia lifti. Inashangaza zaidi kuona kuna watu bado wanaamini kuwa vidole vya Spika havina tatizo.

Ikumbukwe pia sio siku nyingi tuliaminishwa kuwa Mbunge Mtulia kwa sasa yuko kwa waganga wa kienyeji na hajiwezi hata kuongea! Juzi tumemuona bungeni akila kiapo.

Kwa fikra hizi zinazochagizwa na udaku sishangai kuona Wakenya, Waganda na Wanyarwanda wanajazana nchini ili kuchangamkia fursa ambazo zinaonekana kwa watu ambao ni critica thinker na sio passive thinker.

Mtu mwenye passive thinking hana tofauti na nyumbu(herd mentality).

Mbona wewe ndiye kama umeleta udaku humu MsemajiUkweli ?

Nimeingalia hii vidéo mwanzo mwisho akihojiwa na Charles Hilal. Sijaona wala kusikia swali la:

"Mh. Spika, inasemekana umekatwa vidole vya mikono yako na miguu, ni kweli ? "

Naye akajibu "Hapana. Hivyo ni viwanda vya udaku tu ndugu mtangazaji. Mimi nina vidole vyangu vyote 20 . Kumi vya, kwenye viganja vyangu na kumi kwenye makanyagio yangu....!"

After all hata mtangazaji angemuuliza swali hili mbele ya kamera, binafsi ningemshangaa kwelikweli....

Sasa na wewe tukuulize umeyatoa wapi haya ? Umesikia tu, au ?

Kwa mtazamo wangu, wewe ama nyie hukohuko watetezi wake ndiyo hasa mnataka kulikuza jambo hili bila hata sbb za msingi kwa sbb hata kama ni kusema, watu watasema tu huwezi kuzuia midomo ya watu kusema. Kazi ni kwa msomaji ama msikilizaji kuchuja na kupokea kisemwacho...

Na kuhusu hili, hata kama amekatwa vidole vyake iwe vya mikono ama miguu binafsi sioni tatizo lolote iwapo tu hiyo ndiyo ilikuwa sehemu ya tiba ya tatizo lililokuwa linamsumbua....

Watu hukatwa mikono, maziwa, hata miguu. Sasa tunashangaa nini huyu kukatwa tuvidole tu ?? Kwa sbb ni Spika wa bunge ?

Alaa !!. Kwani yeye hawezi kufa ? Wote tutakufa siku moja. Sembuse kupunguziwa baadhi ya viungo vya miili yetu ??

Siasa wakati mwingine ni taabu kwelikweli !!
 
Na bado herd mentality wataumbuka sana siku zijazo.
 
Umegawa dozi mkuu! Safiii
 
Uwongo na ushabiki usio na maana vyote sawa tu. Hebu mwangalie vizuri mzima au mgonjwa kisha rudi uandike upya post yako.
Ulijiuliza kwanini wakati anaenda India kutibiwa ilikuwa siri kubwa mpaka huyohuyo unaemwita mwongo aliponyetisha lakini wakati wa kurudi inekuwa sherehe ya mapokezi!!
 
vidole vilivyosemwa ni vya mguuni, mbona mguu haujaonyeshwa? au ndo kusema mkoni wake ndio mguu???? acheni propoganda na hivyo.
 
Kwani mgonjwa wa Ukoma kuna ajabu gani kukosa vidole mkuu?
 
Yaliyosemwa kuhusu Spika Ndugai yamenifanya nikubaliane na wahenga waliosema, uongo hupanda lifti na ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa.

Spika Ndugai wa leo sio yule ambaye watu waliaminishwa uongo kupitia mitandao ya kijamii.

Katika suala ambalo nchi yetu inapiga hatua kwa haraka ni maendeleo katika fani ya uongo na udaku.

Udaku umewafanya hata wenye elimu ya chuo kikuu wakawa hawana tofauti kifikra/kimtazamo na mtu ambaye hakubahatika kuingia na kusoma kwenye darasa la kwanza.

Wakati inafahamika kuwa mhitimu wa chuo kikuu ni critical thinker, wahitimu wengi wa Tanzania ni passive thinker. Hawa ni wale wanakubali tu kila linaloibuka kwenye jamii au mitandao bila kujiuliza kwa undani zaidi.

Haishangazi kuona habari kama za Diamond Platnumz, Zari na Wema zinajadiliwa zaidi in face value kuliko hata habari za kiuchumi.

Mtu anaanzisha habari ya uongo kuwa Spika Ndugai kwa sasa hana hata vidole kwenye mikono halafu watu wanaanza kumsifia na kumpongeza eti kwa kupata habari hiyo mapema kabla hata ofisi ya Spika haijatoa ukweli.

Spika tuliyeambiwa kwa sasa hana hata vidole vya mikono amehojiwa na Azam TV na kuonyesha kuwa uwongo hutumia lifti. Inashangaza zaidi kuona kuna watu bado wanaamini kuwa vidole vya Spika havina tatizo.

Ikumbukwe pia sio siku nyingi tuliaminishwa kuwa Mbunge Mtulia kwa sasa yuko kwa waganga wa kienyeji na hajiwezi hata kuongea! Juzi tumemuona bungeni akila kiapo.

Kwa fikra hizi zinazochagizwa na udaku sishangai kuona Wakenya, Waganda na Wanyarwanda wanajazana nchini ili kuchangamkia fursa ambazo zinaonekana kwa watu ambao ni critica thinker na sio passive thinker.

Mtu mwenye passive thinking hana tofauti na nyumbu(herd mentality).

Shida kubwa ni hii mipassive thinker kutoka lile lichama la kikabilia likishirikiana na yule changudoa wa marekani wanazusha uongo kwenye mitandao ya kijamii. Hili lichama linatafuta taarifa ya uongo halafu wanamrushia yule malaya kule wanamwambia asambaze na lile malaya bila kuwa na ushahidi kisa kitu kimetoka kwa lichagadema linarusha tu. Hayawazi haya majamaa aiseeeee, ona sasa yanavyoaibika. Baada ya Magufuli kufanya kila kitu unafikiri watatumia sera gani zaidi ya kuzua oooh tumemuapia Mtulia na kweli anaumwa, sijui Ndungai hana vidole. Yani hii ndio miganya ya kienyei na mganga mwenzao anaipotosha kweli. Tuisaidi iamke aisee lasivyo tutaipoteza kabisa kwenye ulingo wa siasa na critical thinker.
 
Haloo. Habari zenu waungwana. Mimi binafsi ninadhani kuwa taarifa za afya ya mh. Spika imetokana na mambo mawili kama c matat.
1. Usiri wa taarifa yenyewe kutoka kwenye of is I ya Bunge. tunajua sote kuwa swala LA afya ya MTU ni siri. Lkn taarifa za jumla ni budi zikatolewa mapema na weledi mkubwa ili kuzuia taarifa zisizo rasmi kutamalaki.
2. Issue ya Tundu Antipas Lissu kutopewa japo sent moja ya matibabu hadi sasa kumeendelea kujenga chuki kati ya wapinzani na watawala. Hali imechangia kwa mh. Spika kuombewa mabaya. hivyo taarifa hizo zilizotolewa ni ishara ya chuki na dua mbaya kwake
3. Propaganda. Ahsante
 
Hebu tuwekee picha ya mguu yake tuhesabu vidole vyake.
 
Kwahiyo last week hakuwa na vidole Leo vimeota?

Huko Shuleni ulienda kusomea ujinga!
Sisi tunachosema Hana vidole vya mguuni, Sasa wewe unajaa nyembe kwani wewe ndie mkewe?
 
Kama umetumia habari za Diamond [na Zari?] kuimarisha hoja yako in negative way, kwanini unabeza reaction ya hoja inayojengwa kumtumia Diamond huyo huyo kupewa nafasi ya kusikilizwa na mkuu wa nchi katika event kama hiyo? Unafikri ni kwanini picha ya Diamond akiteta na Rais ilipewa nafasi kubwa na media? Kufikiri katika "passive thinking" sio tu ni suala linalohusu kuelimika kwa kwa mtu, vinginevyo wewe mwenyewe usingeleta hoja hii hapa, kwani kwa kufanya hivyo umethibitisha kuwa na wewe ni "passive thinker" tu! Utabebaje mambo ya kipuuzi ya mitaani utuletee hapa?
Sikujui lakini kupitia maandishi yako inaonekana kichwani zipo vizuri haswaa! Umemjibu vizuri sana
 
Mbona wewe ndiye kama umeleta udaku humu MsemajiUkweli ?

Nimeingalia hii vidéo mwanzo mwisho akihojiwa na Charles Hilal. Sijaona wala kusikia swali la:

"Mh. Spika, inasemekana umekatwa vidole vya mikono yako na miguu, ni kweli ? "

Naye akajibu "Hapana. Hivyo ni viwanda vya udaku tu ndugu mtangazaji. Mimi nina vidole vyangu vyote 20 . Kumi vya, kwenye viganja vyangu na kumi kwenye makanyagio yangu....!"

After all hata mtangazaji angemuuliza swali hili mbele ya kamera, binafsi ningemshangaa kwelikweli....

Sasa na wewe tukuulize umeyatoa wapi haya ? Umesikia tu, au ?

Kwa mtazamo wangu, wewe ama nyie hukohuko watetezi wake ndiyo hasa mnataka kulikuza jambo hili bila hata sbb za msingi kwa sbb hata kama ni kusema, watu watasema tu huwezi kuzuia midomo ya watu kusema. Kazi ni kwa msomaji ama msikilizaji kuchuja na kupokea kisemwacho...

Na kuhusu hili, hata kama amekatwa vidole vyake iwe vya mikono ama miguu binafsi sioni tatizo lolote iwapo tu hiyo ndiyo ilikuwa sehemu ya tiba ya tatizo lililokuwa linamsumbua....

Watu hukatwa mikono, maziwa, hata miguu. Sasa tunashangaa nini huyu kukatwa tuvidole tu ?? Kwa sbb ni Spika wa bunge ?

Alaa !!. Kwani yeye hawezi kufa ? Wote tutakufa siku moja. Sembuse kupunguziwa baadhi ya viungo vya miili yetu ??

Siasa wakati mwingine ni taabu kwelikweli !!
Mkuu una akili nyingi sana
 
Shida kubwa ni hii mipassive thinker kutoka lile lichama la kikabilia likishirikiana na yule changudoa wa marekani wanazusha uongo kwenye mitandao ya kijamii. Hili lichama linatafuta taarifa ya uongo halafu wanamrushia yule malaya kule wanamwambia asambaze na lile malaya bila kuwa na ushahidi kisa kitu kimetoka kwa lichagadema linarusha tu. Hayawazi haya majamaa aiseeeee, ona sasa yanavyoaibika. Baada ya Magufuli kufanya kila kitu unafikiri watatumia sera gani zaidi ya kuzua oooh tumemuapia Mtulia na kweli anaumwa, sijui Ndungai hana vidole. Yani hii ndio miganya ya kienyei na mganga mwenzao anaipotosha kweli. Tuisaidi iamke aisee lasivyo tutaipoteza kabisa kwenye ulingo wa siasa na critical thinker.
Mkuu inaonekana una hasira nyingi. Hebu tuliza mshono kwanza.

Je, kavua viatu?
 
Mliambiwa vidole vya miguu nyie mnazungumzia vya mikono,basi akanushe kwa kutuonyesha miguu yake
 
aisee, ameonyesha na vya miguuni? [emoji2]
 
Back
Top Bottom