Dhana ya uongo kuhusu Spika Ndugai

Dhana ya uongo kuhusu Spika Ndugai

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Yaliyosemwa kuhusu Spika Ndugai yamenifanya nikubaliane na wahenga waliosema, uongo hupanda lifti na ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa.

Spika Ndugai wa leo sio yule ambaye watu waliaminishwa uongo kupitia mitandao ya kijamii.

Katika suala ambalo nchi yetu inapiga hatua kwa haraka ni maendeleo katika fani ya uongo na udaku.

Udaku umewafanya hata wenye elimu ya chuo kikuu wakawa hawana tofauti kifikra/kimtazamo na mtu ambaye hakubahatika kuingia na kusoma kwenye darasa la kwanza.

Wakati inafahamika kuwa mhitimu wa chuo kikuu ni critical thinker, wahitimu wengi wa Tanzania ni passive thinker. Hawa ni wale wanakubali tu kila linaloibuka kwenye jamii au mitandao bila kujiuliza kwa undani zaidi.

Haishangazi kuona habari kama za Diamond Platnumz, Zari na Wema zinajadiliwa zaidi in face value kuliko hata habari za kiuchumi.

Mtu anaanzisha habari ya uongo kuwa Spika Ndugai kwa sasa hana hata vidole kwenye mikono halafu watu wanaanza kumsifia na kumpongeza eti kwa kupata habari hiyo mapema kabla hata ofisi ya Spika haijatoa ukweli.

Spika tuliyeambiwa kwa sasa hana hata vidole vya mikono amehojiwa na Azam TV na kuonyesha kuwa uwongo hutumia lifti. Inashangaza zaidi kuona kuna watu bado wanaamini kuwa vidole vya Spika havina tatizo.

Ikumbukwe pia sio siku nyingi tuliaminishwa kuwa Mbunge Mtulia kwa sasa yuko kwa waganga wa kienyeji na hajiwezi hata kuongea! Juzi tumemuona bungeni akila kiapo.

Kwa fikra hizi zinazochagizwa na udaku sishangai kuona Wakenya, Waganda na Wanyarwanda wanajazana nchini ili kuchangamkia fursa ambazo zinaonekana kwa watu ambao ni critica thinker na sio passive thinker.

Mtu mwenye passive thinking hana tofauti na nyumbu(herd mentality).

 
Nyumbu Mange akisema wanaweka akili nyuma wanaamini tu. Kwao Mange ni Kama maandiko toka juu Hana shaka ndani yake

Walisema Mtulia yu hoi kitandani, Jana Mtulia kaapishwa akiwa mwenye siha njema na bashasha

Walidai Rais ni mhutu, hawakujiuliza alikuaje mbunge, waziri Hadi Rais bila kathibitisha uraia wake huko kote ila leo Nondo kuhojiwa uraia wake wanajiuliza kwanini leo, kwani kasomaje huko nyuma Hadi chuo kwa pesa za serikali kama sio raia.

Kosa kubwa sana la kiufundi wanafanya kushikiwa akili na Mange
 
Ni kweli kabisa mpaka kufikia kumualika huyo Diamond kwenye sherehe za ufunguzi/makaribisho ya bombadia mpya......na kupewa nafasi ya mbele kabisa

Wewe nawe! Unasadifu hoja yangu kuhusu passive thinker.

Kwani nafasi ya mbele alikuwa Diamond.

Unasikia tu kwenye mitandao bila kutafuta ukweli halafu unabeba na kufanya hoja.
 
Mkuu

Hawa kina Yomboo na Swiss me wangekuwa na uwezo wangekunyamazisha!

Kwa sasa wanaku provoke ili upate ban lakini adhabu unayowapa ni kudharau wanachokiandika.

Ninajua wanafanya hivyo ili upate ban kutokana na kipigo cha hoja unachowapa bavicha mara kwa mara.

They are so dumb.

Dumb beyond belief!
 
Mtu anaanzisha habari ya uwongo kuwa Spika Ndugai kwa sasa hana hata vidole kwenye mikono halafu watu wanaanza kumsifia na kumpongeza eti kwa kupata habari hiyo mapema kabla hata ofisi ya Spika haijatoa ukweli.

Spika tuliyeambiwa kwa sasa hana hata vidole vya mikono amehojiwa na Azam TV na kuonyesha kuwa uwongo hutumia lifti. Inashangaza zaidi kuona kuna watu bado wanaamini kuwa vidole vya Spika havina tatizo.

Unaona unavodhihirisha ujinga wako. Aliyeandika kwamba spika amekatwa vidole aliandika kwamba ni vidole vya mikono? Alizungumza ishu ya kuchongewa viatu, nowadays viatu huvaliwa mikononi? Akili za wapi hizi?
 
Nyumbuza Mange akisema wanaweka akili nyuma wanaamini tu. Kwao Mange ni Kama maandiko toka juu Hana shaka ndani yake

Walisema Mtulia yu hoi kitandani, Jana Mtulia kaapishwa akiwa mwenye siha njema na bashasha

Walidai Rais ni mhutu, hawakujiuliza alikuaje mbunge, waziri Hadi Rais bila kathibitisha uraia wake huko kote ila leo Nondo kuhojiwa uraia wake wanajiuliza kwanini leo, kwani kasomaje huko nyuma Hadi chuo kwa pesa za serikali kama sio raia.

Kosa kubwa sana la kiufundi wanafanya kushikiwa akili na Mange

Mimi nadhani huwa hata hawakumbuki walichokisema jana!

Haiwezekani mtu mwenye akili timamu aambiwe kuwa Mtulia hawezi hata kuongea halafu kesho yake Mtulia anajitokeza na kuongea lakini bado akaendelea kuamini kuwa Mtulia hawezi kuongea.
 
Achana na wafia vyama, hivi bunge lilituambia nini kuhusu kipenzi chetu spika? Nakumbuka walisema haumwi bali alikwenda kucheki afya yake. Juzi nawasikia wanasema alikuwa kwenye matibabu huko India. Swali je bunge lilitudanganya?
 
Back
Top Bottom