Yaliyosemwa kuhusu Spika Ndugai yamenifanya nikubaliane na wahenga waliosema, uongo hupanda lifti na ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa.
Spika Ndugai wa leo sio yule ambaye watu waliaminishwa uongo kupitia mitandao ya kijamii.
Katika suala ambalo nchi yetu inapiga hatua kwa haraka ni maendeleo katika fani ya uongo na udaku.
Udaku umewafanya hata wenye elimu ya chuo kikuu wakawa hawana tofauti kifikra/kimtazamo na mtu ambaye hakubahatika kuingia na kusoma kwenye darasa la kwanza.
Wakati inafahamika kuwa mhitimu wa chuo kikuu ni critical thinker, wahitimu wengi wa Tanzania ni passive thinker. Hawa ni wale wanakubali tu kila linaloibuka kwenye jamii au mitandao bila kujiuliza kwa undani zaidi.
Haishangazi kuona habari kama za Diamond Platnumz, Zari na Wema zinajadiliwa zaidi in face value kuliko hata habari za kiuchumi.
Mtu anaanzisha habari ya uongo kuwa Spika Ndugai kwa sasa hana hata vidole kwenye mikono halafu watu wanaanza kumsifia na kumpongeza eti kwa kupata habari hiyo mapema kabla hata ofisi ya Spika haijatoa ukweli.
Spika tuliyeambiwa kwa sasa hana hata vidole vya mikono amehojiwa na Azam TV na kuonyesha kuwa uwongo hutumia lifti. Inashangaza zaidi kuona kuna watu bado wanaamini kuwa vidole vya Spika havina tatizo.
Ikumbukwe pia sio siku nyingi tuliaminishwa kuwa Mbunge Mtulia kwa sasa yuko kwa waganga wa kienyeji na hajiwezi hata kuongea! Juzi tumemuona bungeni akila kiapo.
Kwa fikra hizi zinazochagizwa na udaku sishangai kuona Wakenya, Waganda na Wanyarwanda wanajazana nchini ili kuchangamkia fursa ambazo zinaonekana kwa watu ambao ni critica thinker na sio passive thinker.
Mtu mwenye passive thinking hana tofauti na nyumbu(herd mentality).