Dhana ya uongo kuhusu Spika Ndugai

Dhana ya uongo kuhusu Spika Ndugai

Yaliyosemwa kuhusu Spika Ndugai yamenifanya nikubaliane na wahenga waliosema, uongo hupanda lifti na ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa.

Spika Ndugai wa leo sio yule ambaye watu waliaminishwa uongo kupitia mitandao ya kijamii.

Katika suala ambalo nchi yetu inapiga hatua kwa haraka ni maendeleo katika fani ya uongo na udaku.

Udaku umewafanya hata wenye elimu ya chuo kikuu wakawa hawana tofauti kifikra/kimtazamo na mtu ambaye hakubahatika kuingia na kusoma kwenye darasa la kwanza.

Wakati inafahamika kuwa mhitimu wa chuo kikuu ni critical thinker, wahitimu wengi wa Tanzania ni passive thinker. Hawa ni wale wanakubali tu kila linaloibuka kwenye jamii au mitandao bila kujiuliza kwa undani zaidi.

Haishangazi kuona habari kama za Diamond Platnumz, Zari na Wema zinajadiliwa zaidi in face value kuliko hata habari za kiuchumi.

Mtu anaanzisha habari ya uongo kuwa Spika Ndugai kwa sasa hana hata vidole kwenye mikono halafu watu wanaanza kumsifia na kumpongeza eti kwa kupata habari hiyo mapema kabla hata ofisi ya Spika haijatoa ukweli.

Spika tuliyeambiwa kwa sasa hana hata vidole vya mikono amehojiwa na Azam TV na kuonyesha kuwa uwongo hutumia lifti. Inashangaza zaidi kuona kuna watu bado wanaamini kuwa vidole vya Spika havina tatizo.

Ikumbukwe pia sio siku nyingi tuliaminishwa kuwa Mbunge Mtulia kwa sasa yuko kwa waganga wa kienyeji na hajiwezi hata kuongea! Juzi tumemuona bungeni akila kiapo.

Kwa fikra hizi zinazochagizwa na udaku sishangai kuona Wakenya, Waganda na Wanyarwanda wanajazana nchini ili kuchangamkia fursa ambazo zinaonekana kwa watu ambao ni critica thinker na sio passive thinker.

Mtu mwenye passive thinking hana tofauti na nyumbu(herd mentality).

Sio vya mkono ni vya mguu
 
Unahamisha magori!

Siwezi kushangaa kama utaviona baadaye utarudi na kudai tako limekatwa huku ukijua kuwa ni vigumu sana kuona!
Usinilazimishe nikubaliane na usemacho!
Mimi sikusikia wala kusoma popote kuwa alikatwa vidole vya mkono! Hilo la kusema alikatwa vidole vya mkono ndio nilisikia kwako...
Angeonyesha vidole vya mguu basi ningeamini alizushiwa!
 
Yaliyosemwa kuhusu Spika Ndugai yamenifanya nikubaliane na wahenga waliosema, uongo hupanda lifti na ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa.

Spika Ndugai wa leo sio yule ambaye watu waliaminishwa uongo kupitia mitandao ya kijamii.

Katika suala ambalo nchi yetu inapiga hatua kwa haraka ni maendeleo katika fani ya uongo na udaku.

Udaku umewafanya hata wenye elimu ya chuo kikuu wakawa hawana tofauti kifikra/kimtazamo na mtu ambaye hakubahatika kuingia na kusoma kwenye darasa la kwanza.

Wakati inafahamika kuwa mhitimu wa chuo kikuu ni critical thinker, wahitimu wengi wa Tanzania ni passive thinker. Hawa ni wale wanakubali tu kila linaloibuka kwenye jamii au mitandao bila kujiuliza kwa undani zaidi.

Haishangazi kuona habari kama za Diamond Platnumz, Zari na Wema zinajadiliwa zaidi in face value kuliko hata habari za kiuchumi.

Mtu anaanzisha habari ya uongo kuwa Spika Ndugai kwa sasa hana hata vidole kwenye mikono halafu watu wanaanza kumsifia na kumpongeza eti kwa kupata habari hiyo mapema kabla hata ofisi ya Spika haijatoa ukweli.

Spika tuliyeambiwa kwa sasa hana hata vidole vya mikono amehojiwa na Azam TV na kuonyesha kuwa uwongo hutumia lifti. Inashangaza zaidi kuona kuna watu bado wanaamini kuwa vidole vya Spika havina tatizo.

Ikumbukwe pia sio siku nyingi tuliaminishwa kuwa Mbunge Mtulia kwa sasa yuko kwa waganga wa kienyeji na hajiwezi hata kuongea! Juzi tumemuona bungeni akila kiapo.

Kwa fikra hizi zinazochagizwa na udaku sishangai kuona Wakenya, Waganda na Wanyarwanda wanajazana nchini ili kuchangamkia fursa ambazo zinaonekana kwa watu ambao ni critica thinker na sio passive thinker.

Mtu mwenye passive thinking hana tofauti na nyumbu(herd mentality).

Alisema ni vidole vya miguu you f.ool, lini uliona kisukari wakate kidole cha mkononi j.inga wewe kabisa
 
Back
Top Bottom