Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Ndugu,
Neno huna akili ni relative term. Wewe unaweza ukadhani sina akili lakini kuna mwingine atadhani tofauti na mtizamo wako.

Wajumbe watakaomchagua Prof. Safari watakuwa na informed decision na siyo kama bendera fuata upepo!

Kama huwezi hata kusoma na kuelewa maandiko, basi unaweza kuangalia video ya mahojiano.
Wewe ni kada wa CCM lakini naona siku zote moyo wako upo CDM.
 
Huna akili kabisa kuleta uongo wa kipumbavu na kijinga hapa jamvini.

Una lengo ovu la kishetani ili wajumbe wasimchague Prof Safari.

Nakuapiahautofanikiwa!
Wewe molemo kumbe uzee wako haukusaidii unadhani matusi yanaondoa ukweli wa hoja iliyopo mbele yetu unaweza kutukana matusi yote na ukweli ukabaki pale pale chadema mmezidi kwa ubaguzi na ukabila msikatae.
 
Ndugu,
Hii akili ya watu wa CCM ndiyo iliyokufanya kutoa comment!.

Suala la kumuua Nyerere ni suala ambalo liko chini ya utaratibu wa makosa ya jinai, otherwise unaweza kuwa kuwasaidia polisi kuhusiana na ushahidi wako.

Suala la mimi kupotea wala lisikusumbue kwa sababu liko juu ya uwezo wako!

Jikite kwenye mada iliyoko mezani.
Mkuu mwana,
shida ya chadema ukiuliza ukweli au kutaka kujua jambo ambalo linatokea kwenye chama chao unatukanwa chama gani hiki kila kitu ni matusi na kejeli?
 
CCM acheni kupindisha ukweli udini,ukabila na ukanda ni ule unaopandikizwa na CCM.Safari alimanisha kuwa CHADEMA ni chama cha watu wenye dini zote,wasiyo na dini na ni chama cha makabila yote bila kujali ukanda,tofauti na longolongo za CCM ili kuthibitisha hayo ndiyo maana kagombea.
 
Chaguzi mbali mbali huwa ni kipimo cha uongozi katika jamii. Chaguzi za vyama vya siasa huwa ni kipimo cha uongozi kwa viongozi wanaomaliza muda wao au kwa wagombea wanaotegemewa kuleta maendeleo katika njia ya mabadiliko au mwendelezo wa misingi ya kile kilichokuwa kinafanywa na uongozi unaomaliza muda wake.

CHADEMA mpaka sasa imeaihirisha chaguzi zake za viongozi wakuu zaidi ya mara moja kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi!. Kwa sasa chaguzi tumeambiwa zitafanyika kuanzia tarehe 16/09/2014.

Nimeguswa na utayali, uwezo, uadilifu na kikubwa zaidi, sababu kuu za mgombea Makamu Mwenyekiti wa chama Taifa-Bara, Prof Abdallah Safari.

Prof. Safari ameainisha mambo makuu matano anayoenda kupambana nayo kama atachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa-Bara.
1) Ukanda
2) Udini.
3) Ubaguzi wa rangi na jinsia.
4) Kuondoa umasikini, ujinga na Maradhi.
5) Ubadhirifu
Usipoyachunguza maneno/sababu anazozitaja unaweza kusema ni maneno/sababu za kawaida kabisa, lakini ukichunguza katika mantiki ya hoja pana utapata maswali fikirishi ambayo ndiyo yatakuwa akisi la CHADEMA kama chama cha kisiasa nchini hasa ikichukuliwa kuwa, Prof. Safari mpaka sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Ieleweke kuwa, unaposema unaenda kupambana na jambo fulani ina maana umeliona lipo ndiyo maana ukatafuta silaha za kwenda kupambana nalo. Kama una akili timamu huwezi kwenda kupambana na adui ambaye hayupo!

Prof. Safari anaposema ameombwa kugombea ili kupambana na dhana/matatizo ya ukanda na udini ndani ya CHADEMA, kwa lugha nyingine anatuambia kuwa ndani ya CHADEMA kuna ukanda na udini!. Kama hakuna, kuna umuhimu gani wa kumchagua kiongozi anayetaka kupambana na matatizo ambayo hayapo!.

Kubwa zaidi, kiongozi makini katika chama au taifa lisilo na dini au ukanda hawezi kuchaguliwa kwa msingi wa dini au ukanda. Prof. Safari anapotaka achaguliwe kwa misingi ya dini au ukanda ina maana anaingia kwenye ulingo wa kisiasa ndani ya chama ambacho mchezo wake ni udini na ukanda. Hii inanipeleka kwenye msingi wa hoja yangu inayouliza, ni kweli ndani ya CHADEMA kuna udini na Ukanda?


[video=youtube_share;dqrIQV6x8eU]http://youtu.be/dqrIQV6x8eU[/video]

Unaweza kutokubaliana na Mwl. Nyerere lakini huwezi kukataa mantiki ya hoja yake aliposema, chama au nchi endelevu haiwezi kumchagua mtu kwa msingi wa dini yake, au sehemu anayotoka nchini. Chama au nchi inayofanya hivyo inakuwa imefirisika kifikra na kimtazamo.

Ni kweli CHADEMA imefirisika kifikra na kimtazamo? If CHADEMA is about fair and equal opportunities for all, why Prof. Safari is playing religion and zone card?


[video=youtube_share;pKscF5wA5jM]http://youtu.be/pKscF5wA5jM[/video]

Tutasikia na kuona mengi kabla ya uchaguzi wa viongozi wakuu ndani ya CHADEMA!.

Mgombea yoyote hunadi Sera na husema au kuahidi atafanya nini atakapo chaguliwa na kukubali kwa prof safari kuwa atapambana na udini,ukanda na ukabila hii inadjihirisha n kweli hayo mambo ndani ya chadema
 
Huna akili kabisa kuleta uongo wa kipumbavu na kijinga hapa jamvini.

Una lengo ovu la kishetani ili wajumbe wasimchague Prof Safari.

Nakuapiahautofanikiwa!

Kwani lazima achaguliwe Prof safari? Mmewaagiza wanachama wamchague?
 
Ndugu,
Neno huna akili ni relative term. Wewe unaweza ukadhani sina akili lakini kuna mwingine atadhani tofauti na mtizamo wako.

Wajumbe watakaomchagua Prof. Safari watakuwa na informed decision na siyo kama bendera fuata upepo!

Kama huwezi hata kusoma na kuelewa maandiko, basi unaweza kuangalia video ya mahojiano.

Nyumba yenye geti.JPG
 
Nini hasa nia ya hoja zako nyingi kuhusu CDM mwanaDiwani? mkuu usishindane na nafsi itii nafsi yako kama inataka kuvaa gwanda tekeleza hakuna siku umeacha kuizungumzia CDM
 
Mkuu mwana,
shida ya chadema ukiuliza ukweli au kutaka kujua jambo ambalo linatokea kwenye chama chao unatukanwa chama gani hiki kila kitu ni matusi na kejeli?
Ndugu Simiyu Yetu
Mimi ninawaogopa sana watu wenye hoja fikirishi lakini siyo watu waliojaliwa matusi kwa sababu matusi hayahitaji upeo wa juu kiakili kujifunza.

Mtu anayetumia matusi kama silaha na ngao ya kupambana na hoja mbadala lazima anakuwa hakujaliwa fikra pana zenye hoja fikirishi lakini mtu anayetumia fikra pana katika hoja anakuwa pia automatic amejaliwa uelewa pia wa matusi.
 
CCM acheni kupindisha ukweli udini,ukabila na ukanda ni ule unaopandikizwa na CCM.
Ndugu, Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa udini, ukabila na ukanda ndani ya CHADEMA umepandikizwa na CCM!.

Kama hakuna udini, ukabila na ukanda ndani ya CHADEMA, kwa nini Prof. Safari anadai anayenda kupambana nao?. Ina maana Prof. Safari ambaye ana akili timamu anataka kwenda kupambana na jambo ambalo ndani ya CHADEMA?.
Safari alimanisha kuwa CHADEMA ni chama cha watu wenye dini zote,wasiyo na dini na ni chama cha makabila yote bila kujali ukanda,tofauti na longolongo za CCM ili kuthibitisha hayo ndiyo maana kagombea.
Sasa kama Prof. Safari alimaanisha unachokisema, kwa nini anatuambia anataka kwenda kupambana nayo ndani ya CHADEMA, kwa maana kuwa hayo masuala ndani ya CHADEMA anayaona ni tatizo linalomhitaji yeye kwenda kupambana nalo kama Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Bara.
 
Mgombea yoyote hunadi Sera na husema au kuahidi atafanya nini atakapo chaguliwa na kukubali kwa prof safari kuwa atapambana na udini,ukanda na ukabila hii inadjihirisha n kweli hayo mambo ndani ya chadema
Ndugu,
Unachokisema ndiyo msingi wa hoja/maswali yangu hasa ikichukuliwa kuwa Prof. Safari ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
 
Ndugu,
Unachokisema ndiyo msingi wa hoja/maswali yangu hasa ikichukuliwa kuwa Prof. Safari ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Na kama amekiri hayo mambo ndani ya chadema mm nafkri ana elimu ya kutosha tena nzuri ,ingekuwa vizuri angegombea uenyekiti kabisa ili afanye hyo kaz yake vzri la sivyo ataishiwa kuitwa msaliti kama kweli anaenda kupambana na udini,ukabila na ukanda dhana iliyoota mizizi chadema
 
Kwani lazima achaguliwe Prof safari? Mmewaagiza wanachama wamchague?
Ndugu,
Hawa vijana wa BAVICHA kila siku ninawaambia kuwa, kazi waliyopewa ya kukitetea chama iko juu ya uwezo wao.

Kila wanalolisema ukiliangalia kwenye hoja fikirishi linaleta maswali mengi.

Inawezekana huyu kijana hafahamu kuwa anachokisema kinajenga hoja inayodhihirisha kuwa Prof. Safari ndiyo chaguo hasa anaposema sitafanikiwa kwa Prof. Safari kutochaguliwa.
 
Back
Top Bottom