Dhana ya "kusitisha au kufuta usajili wa kanisa" inahusisha nini hasa hasa ? Je, ni kutia kufuli majengo ya kanisa hilo ili asiwepo mtu ndani mle?

Dhana ya "kusitisha au kufuta usajili wa kanisa" inahusisha nini hasa hasa ? Je, ni kutia kufuli majengo ya kanisa hilo ili asiwepo mtu ndani mle?

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
3,611
Reaction score
9,269

View: https://youtu.be/8reLapCOf0s?si=d0DkYnApY4VvHj_U
Hebu msikilize vizuri Afande Jumanne Muliro, RPC Kanda Maalumu ya DSM kwenye video hiyo akielezea namna alivyokuwa very sharp yeye na polisi wake kwenda kuzingira na kuwafurusha waumini waliokuwa wakiendelea na ibada ya maombi ya siku 7 ndani ya kanisa la GCC kama walivyotangaziwa na kiongozi na mchungaji wao Josephat Gwajima....

Afande Muliro anadai, alifanya hivyo kutekeleza sheria mara tu baada ya kupokea nakala ya barua ya msajili wa vyama au taasisi za kijamii toka wizara ya mambo ya ndani chini ya Waziri Bashungwa. Na lengo la polisi kufika pale ilikuwa ni kuhakikisha hakuna "shughuli yoyote" inayoendelea ndani ya kanisa hilo la GCC au UFUFUO NA UZIMA linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima...

Kilichofanywa na polisi mara baada ya kulizingira kanisa hilo usiku wa saa 5 kuelekea saa 6 ni;

➡ Kwanza waliwakuta mamia ya waumini wa kanisa hilo wakiendelea na ibada ya maombi....

➡ Wakaingia ndani ya kanisa, kuwataka waumini wote waache ibada yao hiyo na kuwaamuru watoke waende majumbani kwao..

➡ Waumini waliwagomea polisi kwa sababu walikuwa hawaelewi nini kinaendelea na waliendelea kuwepo pale...

➡ Baada ya kuona hivi, polisi walikata umeme unaoingia ndani ya majengo ya kanisa hili na kukawa giza totoro. Haieleweki ni kwanini walifanya tendo hili la kukata umeme. Nadhani ili wawabake wanawake, watoe kipondo na unyama mwingine wowote kwa kadiri watakavyo..


MASWALI YANGU KWA WANASHERIA NI HAYA:

1. Nini tafsiri au dhana ya "kulifungia au kufuta au kusitisha usajili wa kanisa?"

2. Je, ina maana ya majengo ya kanisa hilo kufungwa kwa kufuli na asiwepo mtu kuingia na kutoka humo...?

3. Je, ina maana ya kutofanya shughuli yoyote ya kikanisa au kidini kwa jina la taasisi hiyo..?

4. Kama hiyo ya 3 ni sahihi, polisi walienda kufanya nini kwenye majengo ya kanisa la GCC au Ufufuo na Uzima usiku na kubughudhi watu waliokuwa humo ndani wengine wakiwa ni ma - homeless na walikuwa wamelala tu humo (masna majengo ya kanisa ni kwa ajili ya kila mtu), wengine walikuwa wanasali/fanya ibada nk nk...?

5. Kama ni kusitishwa kufanyika kwa shughuli za kidini kwa jina la GCC au UFUFUO NA UZIMA, Je ikitokea majengo hayo hayo kesho yakabadilishwa na kutumika na kanisa jingine mfano KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA badala ya KANISA LA UFUFUO NA UZIMA lililofutiwa usajili lakini watu au waumini wakawa walewale pamoja na Mchungaji wao yule Josephat Gwajima, huyo Civil Society Registrar atalifuta na hilo jingine? Atafanyeje eti...?
IMG_4519.jpeg
IMG_4520.jpeg

Nakala ya barua yenyewe aliyopokea Afande Jumanne Muliro ni hiyo. Haimpi maelekezo yoyote kuwa, peleka askari wako usiku huu huu na hakikisha kanisa limefungwa na hakuna muumini yeyote anasali hapo...

Mtu aweza kujiuliza, why was it so fast? Barua imetoka mchana, jioni hiyo hiyo kila kitu kisitishwe na majengo ya kanisa yafungwe? Kwanini haikutolewa notice kwanza?
 
Binadamu kuwa chini ya amri ni laana, hapendi ila atafanyeje sasa
 
Back
Top Bottom