Dhana ya "kumbemenda mtoto"

Dhana ya "kumbemenda mtoto"

Kubemendwa ilikuwa ni janja janja ya zamani ya kutaka watu wasichepuke hasa wanaume
Lakn Lilikuwa Jambo Jema Na Pia Ni Jambo Jambo Jema Hata Leo Hasa Kwa Kilinda Heshima Ya Ndoa, na Pia Afya Ya Wazazi Husika Pamoja Na Mtoto.

Ni Mbinu Nzuri Na Naiunga Mkono Sana Kwa Mababu Zetu Kwmb Walifunza Vyema.
 
Usilete siasa katika mambo muhimu ! We mchane tu kuwa jamaa kazingua kaingia chaka ! Basi ! sio unamlambalamba hapa iliuonekane una roho nzuri ?! Huyo jamaa yako ni muongo full stop !!
Mkuu... Kwa sababu lengo ni kuelimishana, nadhani ili kuwasaidia wengine ungesema ni wapi nimeenda "CHAKA"

Kitu kinachoweza kutofautiana katika sperm ya mtu mmoja na mwingine na kufanya utofauti wa kiumbe kipya kutokana na hizo content za sperm ni DNA pekee.Nothing else.

HAKUNA UKWELI WOWOTE KUWA SPERM ZINAENDA KWENYE MAZIWA NA WOWOWO.Ili kuthibitisha hilo unaweza kuweka mechanism ya transport ya sperm kutoka kwenye vagina hadi kwenye breast na matako kama mechanism ya assimilation of food.Ninachofahamu sperm ambazo hazikurutubisha zote zinatoka nje.

Kama ukithibitisha basi itakuwa kweli.

Mkuu.. Ndo maana ukisoma vyema kwenye maelezo yangu nimetoa taadhari kabisa, kwamba sijathibitisha.

Lakini big up kwa kutuelimisha.
 
Mkuu... Kwa sababu lengo ni kuelimishana, nadhani ili kuwasaidia wengine ungesema ni wapi nimeenda "CHAKA"

Mkuu.. Ndo maana ukisoma vyema kwenye maelezo yangu nimetoa taadhari kabisa, kwamba sijathibitisha.

Lakini big up kwa kutuelimisha.
Issue ya kuwa sperms ni acidic in nature eti kwa vile tu zinakiasi kikubwa cha protein.. Sperms kama sperms zina neutral pH. Ila Kuna fluids kutoka kwenye glands mbalimbali (zikiwemo prostate, Cowper's nk.) Ambazo ndizo zinazofanya semen kuwa na alkaline pH. And this is important to neutralize the acidic conditions of the vagina...
 
Habari zenu wajameni?
Kuna hili swala la mtoto kubemendwa, na hii inasemekana hutokea pale ambapo mama anachipuka na mwanaume mwingine au pale ambapo baba anachipuka na mwanamke mwingine ambaye sio mamake na mtoto wakati mtoto bado ni mchanga.

Sasa najiuliza kuna ishara gani za kitalaam (kisayansi) ambazo zinamuwezesha mtoto kujua kwamba baba au mama katoka na mwingine?

Je, mbona hii hali haitokei pale ambapo baba ana zaidi ya mke mmoja? Kwa mfano siku ya kwanza baba kalala kwa mama Kamongo, kesho kalala kwa mama Omena na kesho kutwa kalala kwa mama Olunde (ambaye ndo mwenye mtoto mchanga). Kwa nini hapa Olunde habemendwi na huu ufuska wa baba kwa hawa mama wengine?

Kuna sababu yoyote ya kisayansi au haya ni maneno tu ya kitaa au huu ni uchawi wa kiasili? Naombeni msaada katika hili.
Naona kichwa kimwpata moto...wake zako huwezi kufanya nao ufuska..rekebisha swali lako kwanza.
 
Kabla ya kuendelea kukuhoji kuhusiana na ulichokiandika ambacho mimi nakiita ni sayansi feki,unaweza kuwataja kwa jina, hao virusi wanaotengeneza shahawa?.
Kubali ukatae hiyo ndo mantiki halisi...wewe huna ujualo zaidi ya kupinga kila kitu kwa upumbavu wako.
 
Issue ya kuwa sperms ni acidic in nature eti kwa vile tu zinakiasi kikubwa cha protein.. Sperms kama sperms zina neutral pH. Ila Kuna fluids kutoka kwenye glands mbalimbali (zikiwemo prostate, Cowper's nk.) Ambazo ndizo zinazofanya semen kuwa na alkaline pH. And this is important to neutralize the acidic conditions of the vagina...
Mkuu,unajua JF kuna watu wabishi mno mtu kitu hajui halafu haulizi,kuna mtu kaandika kazi ya asidi ni kulegeza mwili au kuchoma, yaani ni hisia tu ndio zinawaongoza kuliko uhalisia.

Unafika wakati unachoka hata kuendelea kuhoji.
 
Kubali ukatae hiyo ndo mantiki halisi...wewe huna ujualo zaidi ya kupinga kila kitu kwa upumbavu wako.
Kwa baadhi ya watanzania wa aina yako chochote kile, hata cha uongo kinaweza kikawa na mantiki halisi.

Hata babu wa loliondo aliposema anatibu magonjwa sugu na hata ukimwi kwa maji ya mti fulani watanzania wengi walimuamini na kuona ni kweli.

Hata kwa mtu kama wewe sitashangaa ukikubali kwamba composition mojawapo ya spermatozoa ni virus ambao nikikuuliza uwataje kwa jina hautaweza mpaka dunia inatoweka.

Hongera kwa kuwa mwerevu mpumbavu acha nijikalie pembeni.
 
Issue ya kuwa sperms ni acidic in nature eti kwa vile tu zinakiasi kikubwa cha protein.. Sperms kama sperms zina neutral pH. Ila Kuna fluids kutoka kwenye glands mbalimbali (zikiwemo prostate, Cowper's nk.) Ambazo ndizo zinazofanya semen kuwa na alkaline pH. And this is important to neutralize the acidic conditions of the vagina...
Mkuu.. Sijasema shahawa ni acidic in nature kwa sababu zina protein.. Nooo... Ebu soma tena comment yangu...
Mkuu,unajua JF kuna watu wabishi mno mtu kitu hajui halafu haulizi,kuna mtu kaandika kazi ya asidi ni kulegeza mwili au kuchoma, yaani ni hisia tu ndio zinawaongoza kuliko uhalisia.

Unafika wakati unachoka hata kuendelea kuhoji.
Mkuu... Usiwe na mindset ya kubishana zaidi ya kuelimishana.
Mimi ndo niliyesema kuwa acid ina asili ya kuregeza na kuchoma... Sio tu mwili bali kitu chochote... Hata chuma ukikiweka kwenye acid lazima kitayeyuka.

Next time, ukiona mtu amekosea, jenga tabia ya kumrekebisha, na sio kuanza kutoa lugha za ajabu...
 
Mkuu.. Sijasema shahawa ni acidic in nature kwa sababu zina protein.. Nooo... Ebu soma tena comment yangu...

Mkuu... Usiwe na mindset ya kubishana zaidi ya kuelimishana.
Mimi ndo niliyesema kuwa acid ina asili ya kuregeza na kuchoma... Sio tu mwili bali kitu chochote... Hata chuma ukikiweka kwenye acid lazima kitayeyuka.

Next time, ukiona mtu amekosea, jenga tabia ya kumrekebisha, na sio kuanza kutoa lugha za ajabu...
Nmesoma tena na tens na tena lakin ndivyo nilivyoelewa..
 
Mkuu.. Sijasema shahawa ni acidic in nature kwa sababu zina protein.. Nooo... Ebu soma tena comment yangu...

Mkuu... Usiwe na mindset ya kubishana zaidi ya kuelimishana.
Mimi ndo niliyesema kuwa acid ina asili ya kuregeza na kuchoma... Sio tu mwili bali kitu chochote... Hata chuma ukikiweka kwenye acid lazima kitayeyuka.

Next time, ukiona mtu amekosea, jenga tabia ya kumrekebisha, na sio kuanza kutoa lugha za ajabu...
Sawa nimekuelewa.
 
SHITA.jpg
Moja ya imani ambayo imekuwa ikileta malumbano katika jamii ni kuhusu mtoto kubemendwa, ikimaanisha mtoto aliyezaliwa kutopiga hatua za ukuaji au kulemaa viungo vya mwili.

Dhana hii iliyoonea maeneo ya Pwani hususan mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Tanga na Morogoro inaelezwa kuwa inatokana na wazazi wa mtoto kujihusisha na mapenzi pindi anapokuwa bado mchanga.

Wengine huwaita watoto hao kwa majina ya kukejeli ikiwamo ‘fundi viatu’, kutokana na mwonekano wa mtoto ulivyo, kwani huwa hawezi kutembea, kutambaa wala kuongea.

Wapo wanaosema kuwa chanzo cha watoto kupata hali hiyo, ni pale wazazi wanaposhiriki tendo la ndoa kupita kiasi wakati mtoto akiwa bado mchanga na ananyonya.

Sababu nyingine ni mwanamke mwenye mtoto mdogo kujihusisha na uzinzi nje ya uhusiano akiwa bado ananyonyesha mtoto.

Inaelezwa kuwa mwanamke anapofanya ngono huku mtoto akiwa ananyonya, mtoto anaweza kunyonya maziwa yaliyochanganyika na mbegu za kiume na hivyo kumdhuru.

Wazazi wanaokumbwa na kadhia hii huwaficha watoto wao au hata kuhama makazi kwa kuhofia aibu. Kibaya zaidi ni pale wazazi wanapotuhumiana na kisha kufarakana kwa sababu ya hali hiyo.

Upi ukweli?

Kwa namna tukio la kubebemendwa kwa watoto linavyoelezwa na wanajamii, ni dhahiri linahusiana moja kwa moja na tatizo la mtoto aliyezaliwa na kushindwa kupiga hatua za maendeleo ya ukuaji wa kimwili, kiakili na kijamii.

Pia, inahusu watoto waliopata jeraha la kudumu la ubongo na hivyo kupooza viungo au kuwa na viungo vyenye kulemaa na kuchelewa kupiga hatua za ukuaji; kitaalamu tatizo hili hujulikana kama ‘Cerebral Pulse’.

Kitabibu, mtoto mwenye ukuaji hafifu huwa na kawaida ya kuwa mfupi na uzito huwa ni mdogo, kulinganisha na watoto wengine wenye umri sawa.

Kwa wale waliofikia ujana wanaweza kuonekana wakiwa wamedumaa na huku wakiwa na mabadiliko yasiyo ya kawaida wakati wa balehe.

Kimsingi, kubemenda mtoto ni dhana na imani potofu. Kisayansi na kitiba kufanya mapenzi hakusababishi mtoto kuduma au kutokuwa na uwezo wa kukua.

Pia, sio sahihi kuwa mbegu za kiume zinaweza kupenya na kuingia katika mfumo wa damu wa mama na kufika katika vifuko vya maziwa na kisha kumwathiri mtoto anayenyonya.

Kwa kawaida mbegu hizo hubebwa na majimaji mazito na hatimaye kuingia katika nyumba ya uzazi na kubaki huko. Zinazobaki hushuka na kutoka ukeni mwanamke anapokuwa amesimama na nyingine huvunjwahuvunjwa au kuharibiwa na vimeng’enya vya mwili na kutoka pamoja na uchafu mwingine.

Inawezekana kama baadhi ya watu wanavyosema, wazee wa zamani walitunga uongo huu, ili kuwatisha watu wasishiriki tendo la ndoa baada ya mwanamke kujifungua.

Ni kweli siyo vyema kushiriki tendo la ndoa mara baada ya kujifungua. Kitaalamu tunashauri angalau zipite wiki sita au siku 40, kama ilivyozoeleka kijamii; hii inaepusha kupata maambukizi ikiwamo ya nyumba ya uzazi.

Kwa kawaida wiki za mwanzo baada ya kujifungua mazingira ya uke yanakuwa na unyevu pamoja na mabaki au majimaji yaliyochanganyika na damu ambayo yanaweza kuwa ni mazalia ya vimelea. Mabaki hayo yanaweza kuacha kutoka baada ya wiki mbili mpaka nne.

Sababu za kitabibu zinazochangia mtoto kutokukua

Watoto wenye tatizo la ukuaji, huonekana wakiwa na ukuaji hafifu kwa upande wa tabia za kimaumbile, ikiwamo kushindwa kutambaa, kukaa, kusimama na kutembea. Pia, huwa na maendeleo ya taratibu kiakili, kijamii na tabia zinazoashiria jinsia yake ikiwamo kubalehe.Kwa kawaida mtoto hupitia hatua mbalimbali za ukuaji na kila hatua huwa na tabia zake. Kwa mfano, mtoto anapokuwa mchanga ndani ya miezi miwili anatakiwa awe amekaza shingo au anapokuwa na mwezi mmoja awe anatabasamu kwa watu wa karibu.

Yapo matatizo mengi ya kitabibu yanayoweza kusababisha mtoto asiweze kupiga hatua za ukuaji kama kawaida.

Tatizo hili linaweza kuonekana zaidi katika jamii zenye hali duni za kiuchumi, ikiwamo maeneo yenye ukame, vita vya wenyewe kwa wenyewe na wakimbizi.

Mtoto kama hapati maziwa ya mama na lishe (kwa waliofikia miezi sita na kuendelea) kama invyopendekezwa, anaweza kukumbwa na tatizo hili.

Kwa mfano, mtoto mdogo wa chini ya miezi sita anatakiwa kunywa maziwa ya mama pekee; anyonyeshwe angalau mara nane mpaka 10 kwa siku.

Inawezekana mama akawa hana ujuzi wa kumnyonyesha katika mtindo sahihi, hivyo kuchangia mtoto kutopata maziwa ya kutosha. Aidha, ni makosa kuwaanzishia watoto vyakula vya kulikiza (vya kawaida) kabla ya kufikia umri wa miezi sita.

Sababu nyingine ni mtoto kulishwa chakula katika mazingira yasiyofaa kama vile kulishwa akiwa anatazama runinga, kuwa eneo lenye fujo au kutolishwa kwa ratiba.

Matatizo mengine ni pamoja na hitilafu katika chembe za urithi hali inayochangia kupata mtindio wa ubongo, kitabibu hujulikana kama Down syndrome na kuzaliwa na hitilafu katika ogani kubwa ikiwamo moyo na figo.

Pia, matatizo ya tezi zinazozalisha kichochezi cha ukuaji wa mwili, madhara katika ubongo au mfumo wa fahamu ambayo yanaweza kusababisha mtoto kushindwa kula, maradhi ya moyo na mapafu yanayoweza kusababisha utawanyaji hafifu wa oksijeni na virutubisho mwilini.

Upungufu wa damu na matatizo katika chembe za damu, matatizo sugu ya kiafya mfumo wa chakula, kupata jeraha la ubongo wakati kuzaliwa (cerebral palsy) na ujauzito kupata madhara na kujifungua njiti au uzito mdogo sana.

Sababu nyingine ni pamoja na kuumizwa kihisia kutokana na kuondokewa na wazazi, kutengwa au majanga ya kijamii.

Wito kwa jamii

Kitaalamu hakuna dhana ya kubemenda mtoto hasa tukio hilo linapohusianishwa na kitendo cha kujamiiana. Tatizo la ukuaji kwa watoto linatokana na sababu za kiafya na kimazingira.

Wazazi wazingatie elimu ya afya inayotolewa katika vituo vya huduma za afya vinavyotambulika. Kina mama wahakikishe wanafika katika kiliniki za wajawazito na kupata huduma na ushauri.

Chanzo: Mwananchi

Mambo mengine yamebase ki-imani zaidi kiasi kwamba hata wanasayansi hawawezi kutoa majibu ya moja kwa moja...Mfano hata mwanaume ukiwa na mtoto mchanga home ukaenda piga mechi ya ugenini ukaja home ukimbeba mtoto wako atadhurika...Kwa namna gani..Kiimani zaidi na inafanya kazi, Ama macho kwa watoto wachanga mtu akimwangalia mtoto mchanga tu mtoto ataumwa tumbo huku akilia sana..Kwa namna gani hii hutokea...Kiimani zaidi....
 
Naunga mkono hoja, kuna sehemu nilikua naiba mwanamke mwenye kitoto kidogo almost miezi 9.
Na hakija haribika wala nini, tena mtoto ndio ana afya kupita maelezo.
Ni kuzingatia usafi tu baada ya intercourse.
 
Back
Top Bottom