Dhana ya "kumbemenda mtoto"

Dhana ya "kumbemenda mtoto"

kuna mtu niliwahi kubishana nae khs h ishu, ikabidi nmuache na upuuzi wake kichwani.
 
Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni mchanga na ananyonyeshwa.

Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya mapenzi.

Je, kuna ukweli wowote?
Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa! Kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi.

Ni baada ya muda gani mwanamke aliyejifungua anaweza kufanya mapenzi?
unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kujifungua, na wewe kujisikia vizuri na kuwa tayari kushiriki katika mapenzi. pia, mnaweza kusubiri mpaka wiki 6 zipite toka ulivyojifungua.

Je, kuna athari yoyote ya kufanya mapenzi baada ya kujifungua?
Kufanya mapenzi baada ya kujifungua hakuwezi kuleta madhara kwa mtoto endapo hamna maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu). ikiwa mwanaume ana vvu anaweza kumuambukiza mama na kisha mtoto kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.

Ikiwa mnafanya mapenzi kabla ya damu damu ya ukeni kukata, maambukizi ya bakteria yanaweza kutokea kwenye tumbo la uzazi (endometritis). pia kuna uwezekano wa mama kupata ujauzito miezi 6 ya kwanza ya kunyonyesha.

Nini kinasababisha afya ya mtoto kuzorota?
Kama tulivyoona, kufanya mapenzi hakusababishi mtoto kubemendwa. afya ya mtoto inaweza kuzorota kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo;

Kukosa maziwa ya mama ya kutosha.
Mtoto kushindwa kunyonya vizuri
Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.
Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.
Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.
Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).

Kufanya mapenzi na mwenzi wako hakusababishi mtoto kubemendwa. baada ya kujifungua mtoto hutegemea kupata lishe bora kutoka kwenye maziwa ya mama, hivyo nyonyesha mtoto wako vizuri. ukiona ukuaji wake unazorota, onana na daktari.
 
Nilikuwaga nazani kubemenda mtoto ni kama vile panya anapokutafuna vidole..😂
Sikuwahi kuelewa kubemenda ndo kukoje!.. kila mtu na kichwa chake..😅
 
Umekosea dhana/Maana kuu neno “Kubemenda Mtoto “ mtu anaposema amembenda mtoto ni ile hali ya mwanamke ambaye ametoka kujifungua na angali bado mtoto ananyonya akaanza kushiriki tendo la ndoa/ngono na mwanamme ambaye si mume wake ambaye amezaa nae huyo mtoto. Au dhana hiyo pia humaanisha mwanamme aliyetoka kumzalisha mkewe ambaye bado ananyonyesha mtoto huyu mwanamme ndani ya kipindi hiki akaanza kungonoka na wanawake wengine huku pia akirudi kula mzigo kwa mkewe anaye nyonyesha!!
Hizi ndo imani zinazotawala suala hili! Ila sio mme halali kufanya ngono na mkewe wakati akinyonyesha tu! Hiyo mbona kawaida Mzee baba!! Hiyo sio kubemenda. Ila pamoja na maelezo hayo sina uhakika na dhana hii, ila kweli baadhi ya watoto hudhoofika.
 
Mi navyojua kubemenda ni mwanamke kupata ujauzito wakati bado ana kichanga bado

hii huadhiri mahusiano ya mama na mtoto..japokuwa mama anapokuwa mjamzito akiwa na mtoto mdogo bado anashauriwa kuendelea kumnyonyesha kama kawaida kama hana shida yoyote kiafya...

ile dhana ya kuwapeleka watoto kwa ndugu ukiwa mjamzito ni imani potofu na ujinga..na hili ndilo huadhori ukuaji wa mtoto
 
Umeongea vzr ila msiwe wakaidi mtasababisha watoto waharibike, mfano hii mada yako imejikita kisayansi zaidi lkn hujatumia uhalisia wa mambo hvyo kupelekea watoto wazd kuharibiwa na wazazi wao.

Ni kweli kufanya mapenzi hakuwezi kuchangia kubemenda mtoto ila tamaduni zinatuambia baada ya kufanya mapenzi baba na mama hampaswi kumshika mtoto mpk mkaoge na wala sio lishe duni km ulivyosema, cz mtoto aliyebemendwa na mtoto mwenye lishe duni ukiwaweka hapo hawafanani daima.
 
Umekosea dhana/Maana kuu neno “Kubemenda Mtoto “ mtu anaposema amembenda mtoto ni ile hali ya mwanamke ambaye ametoka kujifungua na angali bado mtoto ananyonya akaanza kushiriki tendo la ndoa/ngono na mwanamme ambaye si mume wake ambaye amezaa nae huyo mtoto. Au dhana hiyo pia humaanisha mwanamme aliyetoka kumzalisha mkewe ambaye bado ananyonyesha mtoto huyu mwanamme ndani ya kipindi hiki akaanza kungonoka na wanawake wengine huku pia akirudi kula mzigo kwa mkewe anaye nyonyesha!!
Hizi ndo imani zinazotawala suala hili! Ila sio mme halali kufanya ngono na mkewe wakati akinyonyesha tu! Hiyo mbona kawaida Mzee baba!! Hiyo sio kubemenda. Ila pamoja na maelezo hayo sina uhakika na dhana hii, ila kweli baadhi ya watoto hudhoofika.

sasa wewe ni mmoja ya watu wanaozungumziwa kwenye huu uzi......hiyo uliyo nayo ni moja ya sababu lakin haijitegemei na ndio maana kuna sababu nyingine zimehorozeshwa hapo juu
 
Nilikuwaga nazani kubemenda mtoto ni kama vile panya anapokutafuna vidole..😂
Sikuwahi kuelewa kubemenda ndo kukoje!.. kila mtu na kichwa chake..😅

tatizo wengi wetu hatupend kufanya utafiti tunasikiliza sana maneno ya mitaani..na tunaamin moja kw amoja
 
Nimehudhuria kliniki kuanzia day one mpaka mwisho.

Tendo litakua baada ya siku 40. Na siyo kwa vile kuna kubemenda ila ni kutokana na mama kurecover.

Lishe kwa mtoto ndiyo dawa akivikosa hivyo mbona raia utawasikia wanakuambia umebemenda mtoto kumbe mtoto hali.
 
Umekosea dhana/Maana kuu neno “Kubemenda Mtoto “ mtu anaposema amembenda mtoto ni ile hali ya mwanamke ambaye ametoka kujifungua na angali bado mtoto ananyonya akaanza kushiriki tendo la ndoa/ngono na mwanamme ambaye si mume wake ambaye amezaa nae huyo mtoto. Au dhana hiyo pia humaanisha mwanamme aliyetoka kumzalisha mkewe ambaye bado ananyonyesha mtoto huyu mwanamme ndani ya kipindi hiki akaanza kungonoka na wanawake wengine huku pia akirudi kula mzigo kwa mkewe anaye nyonyesha!!
Hizi ndo imani zinazotawala suala hili! Ila sio mme halali kufanya ngono na mkewe wakati akinyonyesha tu! Hiyo mbona kawaida Mzee baba!! Hiyo sio kubemenda. Ila pamoja na maelezo hayo sina uhakika na dhana hii, ila kweli baadhi ya watoto hudhoofika.
Upo sahihi.
Na pia kama ikiwa mwanamke anayenyonyesha anaweza kuzuia kimwagiwa mbegu na huyo foreign father na akaoga vizuri kabla ya kumnyonyesha mwana hatopata madhara.Na mzee pia akikoga vema mtoto atakuwa salama.Kinyume na hapo ni mtoto kudhoofu na kunyorota.
 
Je, kuna ukweli wowote?
Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa! Kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi....

Nimeishia hapa tu!
 
Back
Top Bottom