Dhana ya "kumbemenda mtoto"

Dhana ya "kumbemenda mtoto"

Mama bado ananyonyesha, lakini kashadungwa mimba nyingine, lazima mtoto abemendwe!

Mimba mpya ikishaingia hata maziwa yanaanza kuathirika ama kupungua.
 
Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni mchanga na ananyonyeshwa.

Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya mapenzi.

Je, kuna ukweli wowote?
Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa! Kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi.

Ni baada ya muda gani mwanamke aliyejifungua anaweza kufanya mapenzi?
unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kujifungua, na wewe kujisikia vizuri na kuwa tayari kushiriki katika mapenzi. pia, mnaweza kusubiri mpaka wiki 6 zipite toka ulivyojifungua.

Je, kuna athari yoyote ya kufanya mapenzi baada ya kujifungua?
Kufanya mapenzi baada ya kujifungua hakuwezi kuleta madhara kwa mtoto endapo hamna maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu). ikiwa mwanaume ana vvu anaweza kumuambukiza mama na kisha mtoto kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.

Ikiwa mnafanya mapenzi kabla ya damu damu ya ukeni kukata, maambukizi ya bakteria yanaweza kutokea kwenye tumbo la uzazi (endometritis). pia kuna uwezekano wa mama kupata ujauzito miezi 6 ya kwanza ya kunyonyesha.

Nini kinasababisha afya ya mtoto kuzorota?

Kama tulivyoona, kufanya mapenzi hakusababishi mtoto kubemendwa. afya ya mtoto inaweza kuzorota kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo;

Kukosa maziwa ya mama ya kutosha.
Mtoto kushindwa kunyonya vizuri
Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.
Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.
Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.
Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).

Kufanya mapenzi na mwenzi wako hakusababishi mtoto kubemendwa. baada ya kujifungua mtoto hutegemea kupata lishe bora kutoka kwenye maziwa ya mama, hivyo nyonyesha mtoto wako vizuri. ukiona ukuaji wake unazorota, onana na daktari.
Haya maelezo ni mazuri, lakini kubemenda mtoto inaeleweka ni "Mwanamke mwenye mtoto mchanga kushiriki ngono na mwanaume/wanaume ambao siyo baba wa huyo mtoto.
 
Hyo ndiyo tamaduni yetu waafrika, asilimia kubwa wanaohudhuria kliniki ni wanawake so automatically lazima uhisi hvyo.
Wanaume wa kiafrica wanabadilika siku hizi,wanazidisha upendo na kujali.Pia wameanza kujitambua kuwa uzazi ni jukumu la wazazi wote hasa huku mijini na hospitali kubwa na zile za gharama.
Pia kuna vipimo vingi vya kupima pamoja.Ila nimeelewa mshangao wake.
 
Wamama wengi wakijifungua hawali balanced diet. Mama anamtoto mdogo ati anakula kiepe
Utamuona mtoto klinik haongezek kilo kisa michips na chai vitumbua..😒
 
Haya maelezo ni mazuri, lakini kubemenda mtoto inaeleweka ni "Mwanamke mwenye mtoto mchanga kushiriki ngono na mwanaume/wanaume ambao siyo baba wa huyo mtoto.
Sio kweli mkuu ni stereotyp tu hizi...he yule mama anayefiwa na mumewe akiwa ana Mimba akajifungua akaolewa na mwanaume mwingine huyu unamuweka wapi...hakuna uhusiano .ni mama kukosa mlo mzuri..we unakesha baa u ajidunga minyagi then unadhan mtoto atakuwa ana afya?
 
Wanaume wa kiafrica wanabadilika siku hizi,wanazidisha upendo na kujali.Pia wameanza kujitambua kuwa uzazi ni jukumu la wazazi wote hasa huku mijini na hospitali kubwa na zile za gharama.
Pia kuna vipimo vingi vya kupima pamoja.Ila nimeelewa mshangao wake.
Ni kweli kwamba kwenda na mwenza hospitali ni upendo ila co kila wanachofanya wazungu basi ndiyo iwe defition ya dunia nzima, pia hayo hayafinyiki mjini tu au hospitali za bei yanafanyika popote pale anapokuwa mwanaume anayejielewa, sorry kwa kutoka nje ya mada ila nmeongea yale ambayo hukutaka kuyaongea kwa kufupisha habari.
 
lengo ni kujaribu kujadili nini hasa kinapelekea mtoto kutokuwa na afya njema..ni vema tukajifunza wote
 
Hapa ss utakuwa umebadili uzi, unaongelea afya njema au mbemendo? Cz mtoto anaweza asiwe na afya njema lkn akawa hajabemendwa.
 
lengo la uzi ni kujadili na kushauriana kuepuka kutokea kwa hiyo hali....
 
Mama bado ananyonyesha, lakini kashadungwa mimba nyingine, lazima mtoto abemendwe!

Mimba mpya ikishaingia hata maziwa yanaanza kuathirika ama kupungua.
Hii Ni Imani tu. Kisayansi hamna kitu Kama hicho. Mama akipata ujauzito mwingine wakati bado ananyonyesha anashauriwa aendelee kunyonyesha Hadi siku atakayojifungua.

Na watoto wengi tu nishawahi waona mama zao wanamimba wakiwa chini ya mwaka waliendelea kunyonya na walikuwa na afya nzuri tu.

Unaweza kushiriki ngono baada ya 6 weeks kwa waliojifungua kawaida na waliofanyiwa operation 3 months. Na hata ukishiriki ngono na mtu asiye baba wa mtoto haina madhara yoyote Kama tunavyoaminishwa kuhusu kubemenda.

Kiufupi kubemenda Ni Imani inayohusishwa na masuala ya ngono wakati si hivyo. Hayo Ni masuala ya lishe, mtoto aliyekosa lishe kwa kingereza malnutrition huku tunasema kabemendwa wakati Inabidi apewe lishe Bora, Kama imezidi Sana hata kulazwa.
 
Kinachomfanya mtoto afya izorotee ni Uchafuuu wa mamaa au baba baada ya tendoo...!! Yani watoto wapo sensitive sana wale Bacteria wanaotokana na Jasho la ngono au kushikana shikana papuchi kwa vidole kisha baba anashika matiti baadae mtoto akinyonya wale Bacteria lazima wamfanye mtoto aumwee...!! Hakuna mtoto anaebemendwa bila.kuwa na magonjwa kama Kuharishaa au kutapika ambapo hivi vitu humfanya mtoto afaya idumae sana kwa muda mfupi.. So tujitahdi kuwa wasafi ikiwezekana FANYENI NGONO SEHEMU AMBAPO MTOTO HALALI.. Kama hamna akikisha mnabadilisha mashuka baada ya mdinyoooKwa heriiii
 
Wakuu naomba kuuliza.
Je mtoto akiwa na afya njema ila amechrlewa kutembea hapo inakuaje wajuvi(mtoto ana mwaka na miezi mi wili ni wa kiume)
 
Hapa millard ayo mbona anamaana nyingine tena?
20200831_175157.jpg
 
Back
Top Bottom