Dhana duni ya 'Mfumo Kristo'

Status
Not open for further replies.
Kweli hali ilivyo ni kuwa Wakristo wana nafasai ya kutoa wasomi wengi kuliko Waislamu, lakini kumbuka kuwa University ya kwanza kujengwa nchini ingekuwa ya Waislamu kama si EAMWS kuwekewa zengwe, ule mradi wa chuo kikuu Changombe ungefanyika kabla ya hizo Uni zote za wakristo unazozitaja na kuzijua wewe! ni nini kilichowafanya wapenda elimu Waislamu wawekewe zengwe kufungua Uni zao na shule zao huku Wakristo wakirahisishiwa?! Ni Waislamu lakini ilikuwaje Makamba Snr Muislamu kwenda kushiriki kumwaga damu ya Waislamu wenzie Mwembechai kama si kutekeleza matakwa ya mfumo Kristo ambao mtumishi yoyote yule wa serikali kutoka dini yoyote ile hana budi kuufuata?
Steang said:
NB:The stupid qustion make sens than stupid words,
Samahan kama nitakua nimekukera ila liwe fundisho kwa wenye UBAGUZI, kama wewe,kazi njema.
Silioni kuwa ni stupid question! kimtazamo wangu ni kuwa swali linalenga ku identify the problem halafu tuna offer solution, wakitaka kusikiliza na kufuata ushauri basi ni vizuri wasipotaka ndio hivyo tena, liwalo na liwe.
 
Miaka 50 baada ya uhuru bado mnawekewa zengwe?
Naam zengwe bado tunawekewa angalia sheria ya ugaidi na mfumo inavyozisitisha taasisi za kimataifa za kuwasaidia waislamu kushindwa kuwekeza katika miradi mikubwa kama ya Elimu, afya n.k.

Hii inawafanya kilichobakia kwao ni kutoa misaada kama ya tende tu, misaada kama hii nikikumbuka mmoja wao akinielezea kuwa wanatoa hali wakisikitika kwa sababu kuna mengi wanayoweza kuwafanyia waislamu ila ndio wamebanwa.

Usisahau pia Waislamu baada ya kukandamizwa kwa muda mrefu wamepoteza hali ya kujiamini kama ilivyorekodiwa kuwa mkuu fulani wa taasisi ya umma ambaye ni Muislamu alishindwa kuidhinisha upanuzi wa Shule ya Sekondari ya Waislamu kwa kuogopa kuonekana kuwa anaipendelea dini yake!.....hii ndiyo hali waliyofikia Waislamu sasa!
 
Tunaamini siku zote LISEMWALO LIPO. Kwa jamii makini na sikivu ni vizuri hisia hizi ziwekwe hadharani na kuzungumzwa kinaga ubaga na kuhakikisha kuwa jamii yote inakula keki ya taifa lenu kwa pamoja bila kuwa jamii moja kuwa superior kuliko nyengine.

Kumbukeni msipoziba ufa ...
 
Mimi huwa nashangazwa sana na habari kama hizi,ni muhimu sasa waislam wakawashika shati viongozi wao wa kiserikali,waislam ambao ndo watawala.Tumeshakuwa na marais wawili waislam, cha ajabu,wao wala hawahusishwi na matokeo ya tawala zao.

JK ana wasaidizi karibia wote wenye nafasi nyeti serikalini,jeshini, dola na bunge,kote ni waislam,nashangazwa huo ni mfumo gani?Hivi huo "mfumo islam" unaweza kucoexist na wengine?ama watu wanataka pure islamic state?

Kwa jinsi ninavyoyaona madai haya,nadhani watu wanaodai kuna mfumo kristo wao wanataka pure islamic sharia law, ama wanataka waislam peke yake wawe ndo viongozi wa serikali? ama ni kitu gani?

Yale ya mwembechai chini ya mzee Mwinyi wala hayakuonekana,ni kwasababu huwa akiwa "mwislam mwenzetu" basi ni immune na katu hana makosa!hiyo ni bias ya kidini iliyopanda hizi chuki ambazo kwa mtizamo wangu zishaota mbegu mbaya sana kwenye jamii.

Na kwakiasi kikubwa,wanaotumika ni wale wa chini wasiokuwa na elimu ya ktosha,wasijue kuwa wanatetea mafisadi na uchafu badala ya uislam.
 
Naomba niulize, Hivi huko Zanzibar ambapo viongozi wake wote 100% ni WAISLAMU, Je nako kuna mfumo Kiristo?

Je Waislamu walioko Zanzibar wanabaguliwa na kudhulmiwa na nani?

Kama mfumo unaofuatwa na serikali ya Tanzania ni mfumo kiristo, Je ni mfumo gani usio Kiristo wala islamic unaopendekezwa? naomba majibu.
 
Si waangalie nchi zinazoongozwa na mfumo Islam zilivo huku Afrika. Somalia, Zanzibar n.k.
hahaaaa na Syria,afaghainistani,libya.shida ya watu wengi hasa waislam ni walalamishi mno,please tufanye kazi tugu szanguni.huwezi kueneza dini kwa fitna na matusi,na ubaqguzi pia.
 
Jiulize kwani znz ipo ndani ya nchi gani?ndio maana sasa hivi wanataka kujinasua,viongozi walikuwa hawana sauti ndani ya selikali
 
Mimi nadhani wote wale ambao wamezungumzia hoja ya mfumo wa ukristo hawaja itendea haki hoja yenyewe. Katika jamii yeyote ile, kuna watu wanaoitwa kwa lugha ya wenzetu "opinion makers"; kwa maana kwamba, muono wa watu hao ndiyo huchukuliwa kuwa dira kwa kila kitu katika jamii husika. Kwa mantiki hiyo, katika dunia tunamoishi sasa, kwa kiwango kikubwa inaongozwa na mawazo ambayo chimbuko lake ni wagriki; mawazo hayo yalizambazwa duniani na warumi; baada ya kusambaratika kwa dola la warumi kazi ya kulinda nakuendeleza mawazo hayo yaliangukia kanisa katoliki la Roma. Kanisa hilo ndilo lililotoa mchango mkubwa katika kubuni mfumo wa utawala unao ongoza dunia hivi sasa. Hivyo wale wote wanaosema kuwa mfumo unao ongoza uendeshaji wa mambo hapa nchini ni mfumo kristo hawajakosea; kosa lao , ni kuhusisha mfumo huo na siasa za hapa ndani. Viashiria vya mfumo huo ni pamoja ni pamoja na kugawanya hesabu za nyakati kwa kigezo cha kuzaliwa kwa Yesu Kristo; kwa mantiki hiyo historia ya dunia imegawanyika kati ya kabla ya Kristo na baada ya Kristo. Aidha siku za kazi zimepangwa kuzingatia mafundisho ya ukristo katika kufa na kufufuka kwa Yesu kristo n.k. Kutokana na hayo, ni dhahiri hoja hii ni pana mno kiasi kwamba ili kuitendea haki inahitaji uchambuzi wa kina na wala siyo huu uchambuzi finyo ambao umekuwa ukifanywa katika mihadhara mbali mbali hapa nchini.
 

Ndiyo maana nikauliza , kama mnaweza kukusanyana uwanja wa taifa na kuchangishana fedha kuanzisha TV Imaan, mnashindwa nini kukusanyana na kuchanga fedha za kujengea shule? Kwanini hamjiamini kuchangia kuanzisha shule lakini kwenye kuanzisha TV mnjiamini na mnashikamana pamoja na kuchangia??
 
Wanajamii tuepuke title, heading au namna yeyote ya kukashfu itikadi. Kiukweli hizi itikadi tumeletewa na wageni, nasi wote hakuna anayezijua sana. Zisiwe silaha za kutupiganisha. Kama zina matatizo basi ni zote za Waarabu na hata za Wazungu. Mwi/Wengine tusijione kuwa safi sana. Na hata aliyeweka hiyo heading amekosea sababu naye anayumbayumba tu hajui. Kama ni kuangalia kati ya hawa marafiki/wageni wetu waliotuletea haya maitikadi nani bora basi anzia kwao huko. Je, wanaishije? Mahusiano yao na wengine, majirani hata wageni! Pia zaidi maendeleo yao, kati ya hao wageni nani kaendelea ki sayansi, maisha bora n.k. Hata mimi napenda kuchagua rafiki aliye na busara, maendeleo, asiye mvivu kazi kupiga domo, uchonganishi, dharau n.k. Sitapinda li vivu, mpiga domo, mlalamishi nk.
Jamani tupendane tusiwe na ubaguzi.
 
Hili ni suala pana! kimtazamo wangu ni kuwa waliotayarisha huu ukusanyaji wa pesa kwa ajili ya kuanzisha TV wameangalia hali ya jamii yenyewe, zama na wakati ndio wakaona ni bora waanze na habari, baada ya waislamu kupata melezo ya kutosha kurudisha kujiamini kwao kinachofuata ni hayo uliyoyataja wewe tofauti na hali ya Waislamu wa Zanzibar, wakati, zama na hali zao haviakisi kuwakusanya na kuwachangisha kwa ajili ya chombo cha habari, unatizama lile linaloakisi na hapana shaka itakuwa ni muungano.
Hali, wakati na zama ya Wazanzibari itakuwa ni tofauti na Waislamu wa Mombasa huwezi ukawakusanya na kuwaambia sasa hivi tuandikeni historia yetu upya! utatizama lile linalonasibu wakati wenyewe mahali penyewe na watu wenyewe.
Nafikiri utakuwa umenielewa
 
Sio kweli kwamba mfumo Kristo ni duni. Pia siamini kama hapa Tz tuna mfumo Kristo.
Ila wanaosema ni duni ni kwa sababu ya uelewa mdogo. Huo mfumo ndio unaotawala dunia, hata vitu vyote mnavyotumia kama vipaza sauti nguo zenu za dini, mashine ya kuchapisha katiba zenu etc vyote hivyo vimetengenezwa na mfumo Kristo. Hivyo ni mfumo ambao haubagui watu wala itikadi zao. Mbona wengine wenye mifumo ya ki maendeleo wapo kimya? Kama vile Japan, China, India (Wahindu) etc. Hivyo tutumie akili zetu vizuri
 
Unajua, ukitaka habari yoyote itiliwe maanani ni kuipa airtime ya kutosha na ndipo hata waliolala wataanza kuamka kila mtu atakuja na lake. Kitendo cha kuanza kujadili masuala ya kidini hapa JF na katika media zetu kumenongeza sana matatizo ya Siaisa za Udini na Chuki za Udini. Ni bora kukaa kimya pasipo kushadadia haya mambo. Hii haijengi!.
 


Well said. Tuna matatizo mengine ni social and economic inherent na mengine ni global oriented. Tunachoihiataji ni proper skills, knowledge, tools and empowerement to wrestle with such incumborances na sio religious differences. Uzuri ni kwamba wote tunaamini katika kuumbwa na Mungu Mmoja na tunapotofautiana ni kwenye doctrines. Wakristu wanaamini katika Utatu Mtakatifu na Waisalamu wanaamini katika Allah lakini mwisho wa siku we all claim originality from one Creator. Ugomvi wa nini.

Ebu jiulize kwanini nchi ambazo Waisalamu na Wakristu ni minority hawagombani hususani India na ambayo uchache wa Wisalamu ni kwamba wanalinganishwa na huge population ya Hindus. Lakini ugomvi uko kati ya Wahindu na Waisalamu na sio Wakristu na Waislamu. Nenda Palestina Waisalamu na Wakristu wanapendana sana na sijawahi kusikia Mwisalamu amelipua makazi ya Wakrstu au Mkristu amempiga Mwisalamu. Hawa wanashirikiana ili kuna wanaleta ukombozi wa kweli wa Palestina. Tunajifunza nini hapa. Ni kwamba tofauti zetu kiimani zinakuzwa na wanasiasa na watu wabinafsi ili waweze kufikia malengo yao lakni shida zetu za kijamii na kiuchumi haziwezi kutatuliwa kwa sababu ya ugomvi na kukashiiana
 
Nadhani sasa hivi kuna Ukweli kuwa CUF ni chama cha Waislaam na Chadema ni chama cha Wakristu.. Yalisemwa na CCM kutugawa na imeshakuwa..Tumeshakubali matokeo hivyo kila mmoja wetu atafute pa kutokea au tuungane kupoteza mgawanyo huu..
 


Nakushukuru mkuu kwa mawazo ya kistaarabu.
Ni ukweli kabisa matatizo makubwa ktk nchi yetu hayachagui dini,ni matatizo yetu wote,after all hizi dini tumezikuta tu na kila mtu siku yake ikifika ataondoka peke yake na nafsi yake tu!kama ambavyo huwezi kuhamisha maumivu toka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine hata kama unamjali kiasi gani yatabaki kuwa maumivu yanayotambuliwa na nafsi yake tu.
Wadau tuacheni hoja hizi za udini ambazo hazina faida kwa taifa letu na kwetu sisi wenyewe .
 
jukwaa la dini would have been appropriate.. hapa kwenye jukwaa la siasa naona unataka kuchafua hewa tu!!

Amelisemea hili hapa kwasababu ziku zahivi karibuni kumeanzishwa gutter politics ya kusingizia vyama vya siasa kuwa vipo dini fulani au kanda fulani, all these rubbish should end 4 the sake of our country
 
Acheni kujadili dino humu nendeni makanisani na misikitini ndio mahali husika
 

Kama hali halisi iko hivyo, nikijikumbusha na mengine kama yaliyojiri katika kampeni za urais mwaka 2010, ambapo nilishuhudia waumini wa kikristo wakatoliki wakienda kanisani huku wamevalia fulana zilizoandikwa ''VOTE FOR PEDRO'', ukitilia maanani mgombea wa cdm kwa nafasi hiyo alikuwa Wilbroad Peter (Pedro) Slaa, kuna haja ya kutafakari UDUNI WA DHANA HUSIKA au vinginevyo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…