Safi sana kaka
Lakini waislam wao wanadai kuwa tangu kuondoka kwa Mkoloni Wakristo wamekuwa kama mabaki ya wakoloni na ukoloni. Ukiondoa shule za msingi na sekondari za Kata, huko katika shule za sekondari za Serikali, vyuo vya kati na vyuo vikuu wanafunzi na wafanyakazi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80. Siku hizi katika shule za Kata wanafunzi Waislamu wameanza kuonekana. Katika taasisi za elimu mfano T.I.E, TEA, NECTA, Bodi ya Mikopo, I.A.E na vyuo vyote nchini, uongozi umekuwa ni mali ya Wakristo. Ushaidi huo hapo juu
Lakini wa kristo walijibu vilivyo hizi hoja na huko mwanzo walidai kwamba hamna Muislamu mwenye elimu ya kutosha kuongoza. Kwa siku za hivi karibuni madai yao kwa wale Waislamu wachache waliofanikiwa kupata elimu ni kuwa hawafai kwa vile wana, "udini".
Lakini ukitazama data zilizopo ukweli kunabaki kuwa katika Wizara ya Elimu (MOEVT) tangu Wizara hiyo kuundwa uongozi umekuwa mali ya Wakristo kwa zaidi ya asilimia 90. Nafasi kama ya Kamishina wa Elimu haijawahi hata kuwa na Kaimu Muislamu na wala haitarajiwi chini ya Mfumochristo. Nafasi za wakurugenzi nazo zimemilikiwa na Wakristo. Mfumokristo umejikita barabara.
Uongozi wa Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu nao umemilikiwa vilivyo. Nafasi za Maafisa elimu Wilaya na Mikoa na wakaguzi wakuu wa elimu wa Kanda kwa zaidi ya asilimia 85 zinaendelea kuwa miliki ya hawa Wakristo.
Kwenye hili, naamini waislam wanaolalamika hoja wanayo kwani kwenye elimu hili lilishapigiwa sana kelele lakini hakuna hata moja lilofanyika na matokeo yake ni hizi data zilizotolewa na wizara ya elimu zinaonyesha wazi kuna matatizo na watawala wao wamezidi kuziba masikio
Sisemi waislam wapewe kwa sababu ya imani zao lakini ninachosema kuwa kuwepo kwa fairness na hasa ukizangatia kulikuwepo kwa tuhuma zamani na juzi juzi not only wizarani mpaka kwenye idara kama NECTA.
Hans Roger Dibagula,
..wanachohitaji Waislamu ni waalimu waliohitimu, na mazingira mazuri ya ufundishaji, ktk shule zao. waziri wa elimu, katibu mkuu, kamishna wa elimu, wote hawana msaada wa moja kwa moja ktk kuwainua Waislamu kielimu.
..pia u have to consider what it takes mpaka mhusika afikie kuwa kamishna, au mkurugenzi ktk wizara ya elimu. mimi nadhani kuna watumishi wengi tu wenye sifa, Waislamu na Wakristo, lakini hawapati nafasi hizo.
..kuhusu tuhuma dhidi ya NECTA kwa kweli nimeridhika na maelezo yaliyotolewa na jinsi suala zima lilivyoshughulikiwa. kulingana na taarifa ya Waziri Dr.Kawambwa, matokeo yaliangaliwa upya kwa masomo yote na siyo somo la islamic knowledge tu. baada ya uchunguzi huo ilibainika kwamba ni matokeo yote yalikuwa safi, isipokuwa yale ya Islamic knowledge.
..kitu ambacho nimejifunza ktk sakata hii ya matokeo, na kimenisikitisha na kunikatisha tamaa, ni kwamba masomo kama, Bible knowledge, na Islamic knowledge, yanatumika ktk kuamua daraja[division] la mtahiniwa. Yaani ktk mfumo wetu wa upangaji matokeo, masomo ya dini yana weight sawa na masomo kama Mathematics,Physics,Chemistry, etc etc. Mimi nadhani mtindo huo ukome. Tunawadanganya wenetu.
..Kuhusu shule za kata, nadhani Waislamu, na wa-Tanzania kwa ujumla, wanapaswa kuwa waangalifu sana na hizo takwimu wanazopewa. Kuna kashfa za baadhi ya wanafunzi "kufaulu" kwenda sekondari na wanapofika huko inagundulika kwamba hawajui kusoma na kuandika. Tambwe Hiza alikuwa mikoa ya kusini kupiga kampeni za CCM akadai kwamba sasa hivi 97% ya wanafunzi "wanafaulu" kwenda sekondari!!!Tuangalie QUALITY badala ya QUANTITY.
NB:
..badala ya kujishughulisha na majedwali ya vyeo, ingependeza kama tungejielekeza ktk kuwatetea wanetu wapatiwe mazingira bora zaidi ya elimu.
..tuwatetee waalimu wapatiwe mafunzo ya kutosha, na mafao mazuri, ili waweze kutoa huduma bora kwa tafa letu.