Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,825
- 730,233
POMBE
Ni kawaida kabisa kuona mtu katoka kufanya ibada kwa uchaji na unyenyekevu mkubwa na kupitia chocho ili 'apoze' koo ama kutoa lock...na inawezekana kabisa kwa imani yake kuna baadhi ya vyakula ambavyo ni kharamu...lakini akakaa pembeni yake na kupata kinywaji chake akiwa na amani kabisa moyoni (kilevi si kharamu lakini hiki kingine ni kharamu)haya ni mazoea yenye kuakisi ukengeufu wa kimaono kwa muktadha mzima wa kipi ni sahihi na kipi si sahihi
NGONO UZINZI NA UASHERATI
Mtu huyo huyo anaweza kukuona wewe ni mkosaji mkubwa kwakuwa tu umekaa bar na kunywa pombe lakini yeye katoka kufanya ibada na kuingia gesti house akiwa na mchepuko, huko anaenda kufanya zinaa. ..hili kwake si dhambi kabisa wala hajisikii kuhukumiwa na roho kwa uchafu ule anaoufanya
VILEVI VINGINEVYO
sigara na madawa...si mngonokaji si mlevi wa pombe lakini haishi kuangalia saa wakati wa ibada akitamani ibada iishe haraka akapige pafu walau moja...mazoea ni yaleyale
WIZI WA KUTUMIA KALAMU RUSHWA NA 10%
Hahaha hapo ndio kabisa hakuna aliyesalimika kuanzia kiongozi wa dini anayeheshimika sana mpaka mtu wa kawaida kabisa mtaani
Pesa nyingi tunayotumia kwenye hayo mambo yote hapo juu si halali ni pesa ya dili na mlungula
Lakini unafiki wa kibinadamu ukuwakuta wanavyijadili kuhusu vibaka na wala RUSHWA utadhani wao ni malaika toka sayari nyingine
Nyama choma unayokula bia unayokunywa gesti uliyolala jana hakuna pesa halali uliyotumia hapo...wewe ni mwizi kama wezi wengine tuu...
Kafanye ibada lakini unajua ni tani ngapi za uchafu umebeba...kama kweli wewe ni msema kweli kuwa mkweli kindakindaki hata kueleza uliyoyafanya mpaka kupata haka kacheo unakotumia kuumiza wengine. ..wewe ni mdhambi kama wadhambi wengine mwizi kama wezi wengine. ...TUSITISHANE...WAKATI SI MILELE...!