Dhambi ya JW imeandikwa kwa kalamu ya chuma

Wengine tuliwaonya na kuwaambia msiamini yale maneno ya sijui kina Tesha na Mange. Nilisema sana hadi wengine wakawa wananitukana.

Nimeamini mwanamke siyo mtu wa kumsikiliza. Huyo Mange bado anaendelea kufanya makosa yale yale ya kupokea maneno ya watu na kupost kama ndiyo ukweli bila kutafakari kwa undani huo ukweli. Watu wa propaganda nao wanapita humo humo maana wameshamsoma.
Acha basi kujitwisha umuhimu usio na ulazima! Kila mtu ana uamuzi wake. Sasa wewe uliwaonya na kuwaambia hao watu kama nani?
 
Sina cha kulaumu, walaumiwe ikiwa tu maandamano yalikua ya amani, ila maandamano yaliyojaa uhalifu ni ngumu kuyalinda, unamlinda vipi mtu anaevunja maduka ya watu na kuiba? Unamlinda vipi mtu anaharibu mali za watu na miundombinu?

Kila mtu akubali makosa yake.
Hakuna Raia mwema yeyote aliyevunjiwa duka na kuibiwa, kama yupo tuwekee ushahidi hapa

Mimi nimeshuhudia ofisi za vijiji, kata, Mitaa na ofisi za CCM zikichomwa moto na Pia mali zilizodhaniwa kuwa za Viongozi

Kuna ofisi zimechomwa mbili katika vyumba vinavyoongozana halafu duka la raia lililo katikati likaachwa

Halafu kingine ni kuwa wengi waliouawa hata hawakuwepo katika Maandamano, hasa watoto wadogo

Hapa ninapoongea nimetoka kuzika mtoto aliyemaliza darasa la 7 juzi na hakuandamana

Hii DHAMBI mtailipia
 
Jw ikajifanya kuwa nyuma ya wanachi,Wananchi Vichwa vikawaka,wakajua kuwa tunaowatetezi nyuma yao,kilichokea ni MASSACRE.

Maelfu ya watu wameuawa ndani ya siku Nne tu.wakati Mama na genge lake wameua na kuteka watu zaidi ya Mia tatu kwa kipindi cha miaka miwili. wametumia muda mrefu ila matokeo hafifu wakati Jw imetumia muda mchache zaidi ila matokeo significant.

KUNA WATAKAO MSAMEHE HUYU MAMA ILA DHAMBI YA JW IMEANDIKWA KWA KARAMU YA CHUMA.

RIP WASHIKAJI ZANGU,CHATI ZENU ZA MWISHO NITAZIHIFADHI HADI NITAKAPO IRUDIA ARDHI.
Kama Amiri jeshi mkuu na CDF wapo kwenye mahusiano mazuri, ni ujinga tu ndio unaweza kumfanya mtu akaamini jeshi litakua upande tofauti na amiri jeshi.
 
Hakuna Raia mwema yeyote aliyevunjiwa duka na kuibiwa, kama yupo tuwekee ushahidi hapa

Mimi nimeshuhudia ofisi za vijiji, kata, Mitaa na ofisi za CCM zikichomwa moto na Pia mali zilizodhaniwa kuwa za Viongozi

Kuna ofisi zimechomwa mbili katika vyumba vinavyoongozana halafu duka la raia lililo katikati likaachwa

Halafu kingine ni kuwa wengi waliouawa hata hawakuwepo katika Maandamano, hasa watoto wadogo

Hapa ninapoongea nimetoka kuzika mtoto aliyemaliza darasa la 7 juzi na hakuandamana

Hii DHAMBI mtailipia
Katika vurumai za kiwango chochote tegemea itawahusisha watu wasiohusika...ili uwe salama kwenye vurumai zinazohusisha risasi baki ndani kwenye kuta za nyumba,,hata kuchungulia dirishani ili ujue kinachoendelea umejiweka kwenye hatari.
 
Mama anayefunga biashara zake gengeni na kuwahi wanae nyumbani anakaribi kufika mlangoni anapigwa risasi ya kichwa. Huyo Mwanamke ulitaka ajihami vipi Sheikh?

Mtoto wa miaka mitano ajihami vipi ilihali hajawahi kuona bunduki au kufikiri Nchi yake itafikia huku unamshaurije Ya arabi?
 
Sina cha kulaumu, walaumiwe ikiwa tu maandamano yalikua ya amani, ila maandamano yaliyojaa uhalifu ni ngumu kuyalinda, unamlinda vipi mtu anaevunja maduka ya watu na kuiba? Unamlinda vipi mtu anaharibu mali za watu na miundombinu?

Kila mtu akubali makosa yake.
Polisi walivyoanza kushambulia raia ndipo raia waliporeact mbaya zaidi hata baada ya raia kuacha kuandamana walikuja mtaani. Mimi mtaa ambapo ofisi yangu ipo Asubuhi Alhamis watu wakiwa dukani wanapata mahitaji ya kibinadamu walipigwa risasi 7 hapo hapo 4 walikata moto na mwongine alikufa siku inayofuata wawili wapo hai.

Hivyo wakuu tuachane na huu uongo wa kupotosha hakuna raia aliyefanya fujo bila sababu ilitokea baada ya askari kuanza kupiga risasi hovyo.
 
Hakuna Raia mwema yeyote aliyevunjiwa duka na kuibiwa, kama yupo tuwekee ushahidi hapa

Mimi nimeshuhudia ofisi za vijiji, kata, Mitaa na ofisi za CCM zikichomwa moto na Pia mali zilizodhaniwa kuwa za Viongozi

Kuna ofisi zimechomwa mbili katika vyumba vinavyoongozana halafu duka la raia lililo katikati likaachwa

Halafu kingine ni kuwa wengi waliouawa hata hawakuwepo katika Maandamano, hasa watoto wadogo

Hapa ninapoongea nimetoka kuzika mtoto aliyemaliza darasa la 7 juzi na hakuandamana

Hii DHAMBI mtailipia
Mimi Binafsi biashara yangu imevunjwa na nimeibiwa karibu kila kitu, kwahiyo naelewa nachoandika na nimevunjiwa tarehe 29, hiyo biashara ndo ilikua sababu ya kuilisha na kusaidia familia yangu kwa sasa nimepoteza kila kitu.
 
Walijua wewe ni Kada wa CCM
 
Jeshi la WALANCHI.... kikubwa ni kwamba wananchi tumejua hakuna wa kutukomboa bali sisi wenyewe
 
Back
Top Bottom