Deusdedit Balile adai Ngorongoro hakuna makaburi hivyo Wamasai waondolewe Ngorongoro kuwaepusha kuendelea kuliwa na Wanyama

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Baada ya Maulid Kitenge kufanya tour na timu yake Ngorongoro watu walijitokeza nakusema alivyolipwa na kwamba ana tekeleza matakwa ya watu flani na siyo utashi wake.

Siku chache Balile kawaitisha vyombo vya habari na wanahabari kuwashawishi au kupiga kampeni kuwaondoa Wamasai Ngorongoro. Nilichochukizwa na huyu mtu ni pale alipomhusisha Mungu kwenye uongo.

Anaeleza kwamba Ngorongoro hakuna Makuburi Kwa maana Hiyo Masai akiugua wanamwacha Ndani wanafungua milango ya maboma Kisha wanafungia kondoo nje Ili fisi au mnyama mkali akija kula MBUZI ale na mgonjwa Kisha wao wanakimbia.

Naomba kumuuliza, anajua maboma ya kimasai yanafungwa na Nini? Anajua kwamba uhitaji kufunga MBUZI mlangoni Kwa sababu MBUZI na binadamu wanaishi pamoja? Anajua Ngorongoro maboma hayana hata Hiyo milango? Anaelewa kwamba suala la kuzika kwenye makaburi limeanza hivi karibuni na kwamba Wajaluo wakizika walikuwa wanapitisha mifugo kuondo kabisa kaburi Kisha wanapanda miti?

Anaelewa kwamba miaka ya zamani Kagera waliishi bila makaburi, anaelewa kwamba wapo watu wanachomwa na kwa msingi wa tamaduni zao uwezi kukuta makaburi? Anaelewa kwamba huko Longido wapo wazee wa Mila wamezikwa hata miaka ya karibuni na viongozi wa kisiasa walishiriki mazishi? Anaelewa kwamba Kila kabila Lina tamaduni zao? Amewahi kujiuliza Hadzabe wanazika VIPI? Amewahi kujiuliza wasukuma porini wanafanyaje wakipata msiba?

Huyu mtu anaishi Dar es Salaam akisubiri alipwe pesa ya safari anajulia wapi Mila na desturi za makabila mengine? Lakini anapotumia vyombo vya habari kuvictimize kabila flani Kwa sababu tu awapendi au hakuna Ndugu zake huko analiweka wapi Taifa? Kwamba alikozaliwa kuna maskini na watoto wengi awaendi shule na anaficha AIBU ya familia yake na ukoo then anaanza kutumia vyombo vya habari kudhalilisha makabila mengine, haya NDIYO aliyofundishwa?Kama ana uchungu yeye na hao waandishi wenzake kwanini wasiandike changamoto za elimi za watoto waliopo vijijini kwao?

Tunapotumia vyombo vya habari kupenyeza agenda let us be neutral. Hatuwezi kutumia vyombo vya habari kudhalilisha Masai Kwa sababu tu awajui kusoma na kuandika na sisi tumesoma. Hatuwezi kudhalilisha maginalized group kwa sababu tu tumejaliwa Kuishi maisha Mazuri na madaraka tunayo. Since 1956 Serikali haikuona hao Wamasai wanaliwa na wanyama waje waone akina Balile Leo? Miaka yote hakuna clip ya hiki anachokisema ,Hana evidence ya MBUZI aliyefungwa kwenye boma kuvutia fisi waje kumla binadamu anapata wapi ñguvu yakuwaambia wanahabari mambo ya hovyo hivi?

Nani anawalipa Hawa watu? Kwa malengo Gani? Tunakumbuka utoroshaji wa twiga? Mambo yalianza hivihivi , tuwe makini na bahasha za matajiri na tukizipokea tusimomonyoe nchi, tule tuiache nchi ikiwa salama. Serikali inaweza kabisa kuwaondoa Masai bila propaganda wala kuwadhalilisha.
 
Balile kama ni kweli umelisema hili toka hadharani uombe radhi. Ni jambo la kudhalilisha kuwaona binadamu tena watanzania wenzio kuwa wa daraja la 2. Ulikuwa na namna nyingine ya kutoa mawazo yako na ukaeleweka lakini kudhalilisha Wamasai kwa namna hiyo hapana. Otherwise uwe umesingiziwa.
 
Kuna hotel zinataka kujengwa pale ! Wamasai watachafulia hadi waone tanzania siyo nchi yao ! Duuh hii nchi ngumu sana! Tayari wanahabari walichapewa cha kwao mapema.
 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) amefichua makubwa yanayoihusu jamii ya Kimasai hasa wanaoishi eneo la Ngorongoro kwa kusema wanatweza utu wa mwanadamu hasa anapoumwa na kumuacha peke yake afe kwa kuliwa na wanyama wakali.

Balile amesema kuwa inapotokea mkazi wa Ngorongoro ameugua sana na wanandugu kupoteza matumaini ya ndugu yao kupona, basi humtelekeza ndani ya Boma baada ya kumnyoa kipara na kumpaka mafuta yao na kisha kuacha mlango wazi ambapo nje ya mlango wanamfunga KONDOO wakijua wakija wanyama wakali usiku watamla kondoo na kwa kuwa mlango uko wazi wakimmaliza kondoo wataingia ndani na kumla mgonjwa.

Mwenyekiti huyo wa TEF ametoa ushuhuda huo leo wakati wa mkutano wa pamona wa Wanahabari kujadili na kubadilishana maarifa kuhusiana na kinachoendelea Ngorongoro, mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Wanahabari watetezi wa Rasilimali na taarifa MECIRA.
 
Baada ya Maulid Kitenge kufanya tour na timu yake Ngorongoro watu walijitokeza nakusema alivyolipwa na kwamba ana tekeleza matakwa ya watu flani na siyo utashi wake...
Balile ana akili za kinyesi aanze kwa na harakati za kuigawa Kagera iko too peripheral awaze hilo, as dada zake wa uwanja wa fisi na kwa wahaya akimaliza hayo ahamie ngorongoro.

Utengano ni sumu wanaotaka kuionja waendelee Tanzania will lose Big on this issue with the wamaasai someone somewhere is provocating the wtz ili mpoteee. Envy from neighbors is alarming
 
Back
Top Bottom