Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,801
- 12,247
Nimekuwa nikijiuliza: Tanzania kama Taifa huru tunanufaika nini na uwekezaji unaofanyika Loliondo na Ngorongoro?
Najiuliza swali hili kutokana na mateso na manyanyaso ambayo inaelezwa wenzetu Wamasai wanapata kutoka kwa vyombo vyetu vya dola vikiwemo Polisi, JWTZ na Askari wa TANAPA.
Inaelezwa kuwa Wamasai wanapigwa risasi, mabomu, mijeredi na kunyimwa chakula ili kuwalazimisha kuhama katika maeneo yao ya asili! Inadaiwa Wamasai wanawindwa kama Swala mwituni, wanafungwa Magerezani, wanapotezwa kusikojulikana yaani ni mateso kwa kwenda mbele kama siyo wananchi, kama siyo watu na kama wahaini wanaotaka kupindua Serikali!
Kama ni fedha ni kiasi gani hicho ambacho Serikali ya Samia inajivua utu hadi kudaiwa kutekeleza mauaji ya kutisha kwa raia wake?
Kwamba sasa Serikali inaondoa huduma zote za jamii kama elimu, afya na utawala ili kupisha wawekezaji! Kwamba fedha na wawekezaji wana thamani kuzidi wananchi wake na utu wa binadamu?
Waandishi wa habari mna mchango mkubwa sana katika madhila na mateso yanayowapata wamasai. Mnalipwa na Serikali kuandika uongo kwa ajili ya matumbo yenu! Mmesahau majukumu yenu ya kutoa taarifa za ukweli bila upendeleo kwa sababu ya fedha! Ninyi pia ni wauaji wakubwa! Mateso ya wamasai yatawafuata na hakika malipo yenu yapo hapa hapa duniani!
Iwapo yanayodaiwa ni kweli, Serikali ya Samia acha kutoa mateso kwa raia wako. Wamasai ni raia na zaidi ya yote ni binadamu wanastahili kutendewa utu! Mbaya zaidi mnawaondoa wamasai mnapeleka watu wenu, mngeeleweka kama mngeacha mapori wazi!
Hakika Mungu yupo na anawaona!
View: https://twitter.com/BabaMwita/status/1694667616298655855?t=8MXbt0ZGvUwr2FnVCpnfpA&s=09