Uhifadhi na utalii, acha uwe hivyo tusiwapumbaze wananchi (Wamasai)

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Sasa ninaamini kwa nguvu zote kwamba kati ya mambo magumu kuyafanya ni kukubali mabadiliko.(change).

Wakati mmoja nikiwa mahali, nilisikia kisa Cha watu ambao walimkataa kasisi wao mpya baada ya kuondoa kibweta ambacho kilikuwa mahali pasipo sahihi lakini kwa sababu ya mazoea ( ambayo hupinga mabadiliko) yule kasisi alikataliwa na watu wakadai kile kibweta kirudishwe mahali pake pa siku zote.

Lakini ajabu ni hii, alipokuja kasisi mwingine, yeye naye alikubaliana na yule kasisi aliyekataliwa kwamba " kile kibweta kilikuwa mahali pasipo sahihi. Lakini tofauti na yule wa kwanza, huyu alikuwa anaamisha kile kibweta taratibu kadiri alivyokuwa anapata nafasi ya kusimama pale, Mwisho wa siku kile kibweta kikarudi palepale mahali yule kasisi wa kwanza alitaka kiwe na Zamu hii hakuna aliyepiga kelele maana kilikuwa kinahamishwa taratibu taratibu mpaka mahali hapo.

Baadae,watu walicheka sana na kufurahi walipogundua kibweta Kiko eneo zuri ambalo kwanza walilikataa mpaka kugharimu maisha ya kasisi pale alipofukuzwa.

Nataka nikubaliane na huu ukweli kwamba mabadiliko ( change) ni Moja ya mambo magumu kuyafanya .

Mjadala wa kuhamisha wananchi aka maasai, Kutoka hifadhini mie cjui kwa hakika tunakwama wapi?

Hifadhi ni eneo maalumu kwa ajili ya ulinzi wa raslimali asili. (Natural resources) inawezekanaje tuendelee kutetea watu kuendelea kuishi ndani ya eneo ambalo limetengwa mahususi kwa ajili raslimali asili?

Kwa kuwa wakoloni walifanya kosa (compromise) na wananchi kwa maana ya wamasai na kuamua kuwaacha hapo baada ya wamasai kukubali kutoka Serengeti, sisi wenyewe Sasa baada ya kujitawala, tunaona umuhimu wa kutunza na kuzilinda hifadhi zetu, tatizo ni Nini hapo? Je tuache watu waendelee kuishi ndani ya mbuga Ili kuwe na mgogoro wa binadamu na wanyama( human wildlife conflict)?

Hivi kweli tuna ubinadamu? Unawezaje kutetea watu kuishi hifadhini mahali ambako hawawezi kufanya hata shughuli zao za kawaida za kiuchumi? Hivi hawa si wataendelea kuwa masikini daima, ukiachia mbali kuwa wanadamu wanaohifadhiwa!!!!!

Suala la mbuga kupewa waarabu Mimi hata sioni mashiko yake kimantiki. Hivi ndo mara ya kwanza tunaona watu wakiwekeza hifadhini?

Nenda Serengeti, mikumi, hifadhi nyingine na mapori ya akiba, je hakuna wawekezaji? Au kwa kuwa hawa ni wazungu na si waarabu?

Mahotel yanayosemekana kujengwa, sijui uwanja wa ndege na nini, hivi si ndo uwekezaji wenyewe au vipi ndugu zangu?

Ninachokiona Mimi ni hofu tu ya watu kuhama( Fear of the unknown) na hofu ya mabadiliko kwa ujumla kama wale walivyodhani kwa habari ya kile kibweta.

Kama kweli tunathamini utu na maendeleo ya watu, hivi tunateteaje watu kuishi porini na wakati huohuo hawafanyi kazi zao za kiuchumi bali kutegemea misaada?

Kuhama ( immigration & migration) ni jambo la kawaida duniani kote. Wanyama uhama, ndege huama, na binadamu pia.

Hapa kwetu kuhama kulikoletwa na mpango wa vijiji vya ujamaa lilionekana jambo gumu. Lakini nambie Leo kama hatuoni matunda ya kukaa pamoja?

Nilikuwa mdogo kipindi hicho, lakini malalamiko na hofu ni kama hii hii ninayoiona kwenye suala la Ngorongoro. Hofu ya mabadiliko.

Tuwatie moyo ndugu zetu wanaoogopa kuhama. Na ukweli husemwe,serikali imejitahidi na imewajali sana wananchi wake hawa.

Tuwatie moyo Hawa ndugu kuhama na tusichanganye mada ya bandari( waarabu) na wawekezaji wa Loliondo ( waarabu)

Let's not be racists.
 
Back
Top Bottom