Derick Gaspar Mkandala Lufufu afariki dunia

Derick Gaspar Mkandala Lufufu afariki dunia

Kwa kweli tunammis sana na zile swaga zake, hakika tutamkumbuka daima, dah nimejikuta nalia nikikumbuka those moments, maisha bhana watu tunatoka mbali mpaka kuonekana wa kishua ahahaah
 
Alikuwa anafanya shughuli gani? naona bila shaka sikuwa ktk ulimwengu wake!Simjui na ndo namsikia leo!
R.I.P.

Mkuu! Utotoni mwako ulisomea Uganda au Kenya? Huyu jamaa watu waliozariwa late 80s na early 90s wengi wanamjua, kuanzia Masaki-Dar mpaka Kashai-BK, Kishumundu-Kilimanjaro mpaka Namtumbo-Ruvuma.

Rest in peace babu Lufufu
 
Hakuna mwingine aliye Na kipaji kama yeye?? Watoto wa uswazi watammiss sana
 
hiyo movie ya mniga analiwa na mamba nilipoisoma mpaka mwili umenisisimka mdau Mzimu wa Kolelo umenikumbusha wakat nasoma primary school enzi hizo kulikua na programu ya sinema za bure ikiendeshwa na shirika la bima la taifa (NIC) KWENYE OPEN GROUNDS,kwanza mnawekewa sinema za faida ya shirika la bima,kisha mwisho mnawekewa hiyo ngoma ya 'MAKOMANDOO SITA'.
Daaaah zamani sana kwakweli
Hiyo Movie inaitwa The Hard Way The Only Way.
 
Kwa wale wapenzi movie za kitambo za actions lufufu alitusaidia sana vibanda umiza ..na kwa wapenzi wa Nigeria movies na Ghana "uncle msafiri" kiukweli alizitendea haki sema nimemis movie zake ..mwenye movie zilizotafsiriwa na uncle Msafiri tusaidiane ..
 
Habar wakuu.
Nimekua nikifuatilia sana muvi alizotafsiri dj mack na rufufu kwa muda mrefu. Ni watu ninao wakubali sana hasa dj mack maana ni mtu aliyenifanya niwe natoroka shule naenda vibandani kucheki muvi zake. Nimejaribu kumtafuta dj Mack fb na Instagram lakini sijampata,

kwahiyo mtu yoyote mwenye picha ya dj mack au rufufu aiweke hapa niwaone hao watu au kama kuna mtu anaweza jua account zao za insta or fb anuelekeze niwasakue mwenyewe. Pia hata namba zao za simu kama zinapatikana mnipe
 
wewe mtoto dj mack kaanza juzi tu hapa kutafsiri wewe ndo unatoroka shule ...
Rufufu kafa ana miaka hata mi3-4

Soma mdogo angu Elimu ni ufunguo wa maisha... hizo cheche aah cheche hazina maana yoyote.
Mkuu kwani hujui sifa ya fasihi simulizi? Lazima uongeze chumvi ila unajuaje kama mm ni mdogo kama nilianza nikiwa na miaka 12
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom